Kwanini CHADEMA wanaonekana wa muhimu kuliko vyama vingine awamu ya sita?

Kwanini CHADEMA wanaonekana wa muhimu kuliko vyama vingine awamu ya sita?

Rudi kwenye speech ya Freeman Mbowe kwenye mkutano wa baraza kuu majibu yote ya maswali yako alishayajibu kwenye ile speech.

Dunia inakwenda mbele wewe unarudi nyuma, wengine tupo mwaka 2035 ila wewe upo mwaka 2016.
Hata juzi nimemsikia Tundu Lissu akilisemea hii.

Chadema tukijibrand vizuri sana.

Kama chama kinaweza kusalitiwa na Makatibu Wakuu Wawili mfululizo na bado kikabaki imara unawezaje kukipuuza?
 
Akienda Zitto msaliti, Lipumba msaliti ila akienda Mbowe na Mnyika wao ni wapinzani wa maana?

Hii siasa ya wapinzani wa CCM ni ya kipumbavu sijawai kuona akili na mawazo yao ni kuitwa Ikulu tu
Hao wengine sio wapinzani ni wenzao wanaojivika upinzani.

Tuliwambia siku ya kukutana na Rais hakuna mtu mwingine atajichomeka mkabisha.

Chadema ndio kiboko yao.

Chama la watu
 
Chadema wamesimama imara na misimamao Yao imewafanya waitwe ikulu Kwa heshima na siyo kwenda tu: lakini pamoja na nguvu waliyonayo kwanini wanavifanya vyama vingine kama siyo wapinzani? Akina Lipumba na Zito hata Mbatia wamepotelea Wapi kwenye ramani ya siasa?

Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?
Rejea kauli ya Mbowe ambayo ndiyo hali halisi... Unapotaka maridhiano ya kudumu tafuta muda kutana na yule uliyemdhulumu. Usikutane na wapambe au wasindikizaji ambao hawana kumbukumbu ya kudhulumiwa chochote!
CDM walipokuwa wakidhulumiwa wengine walikuwa upande wa mdhulumaji!
CDM na ccm muhimu sana kwenye mchakato wa maridhiano!

SSH na Kinana wanazidi kuirejesha nchi kwenye ramani ya dunia.
Big up sana Mbowe! Great politician... very principled! Ni wajinga tu ndo hawaelewi mchango wake!
 
Sasa kwa mfano CUF unaweza kukiita chama cha kisiasa tena cha upinzani hali mwenyekiti wake Lipumba anampa mbinu za ushindi mwenyekiti wa chama tawala!? Na wanachama na viingozi wenzake wako kimya tu hawasemi lolote kweli utaamini hicho ni chama cha siasa? Chama kinachoongozwa na Profesa kimekata tamaa kiasi cha mwenyekiti wake kukipa mbinu za ushindi chama shindani kwake hii haiingii akilini kukiita chama cha upinzani. Kwa sasa japo mimi si mwanachama wa chama chochote ninaona only CDM ndo chama kinachopigania kushika dola baada ya CCM. Vingine havijajiandaa kushika dola na vimekata tamaa hata kupigania mazingira bora na ya usawa kisiasa ili viweze kukua.
 
Chadema ni chama makini na mahiri.
Wamepitia machungu mengi na hili ndilo limewapa krediti kuwa pamoja na mateso na vifungo bado wako imara.

Kuhusu vyama vingine ccm haiwezi kuwapa umuhimu sawa na chadema kwasababu wana ndimi mbili.

ACT hawakljulikani wanasimamia nini.
Mbatia alianza usaliti enzi za jiwe.
Cuf tayari waneanza na kampeni Samia ashinde.

CCM ni kama shetani.
Shetani huwa hapambani na wenye dhambi anajua ni watumishi wake bali hupambana na watakatifu na wacha Mungu.
Mshana Jr jr
Wakiitwa wengine msianze matusi.
Kuweni na siasa za uvumilivu
 
Chadema wamesimama imara na misimamao Yao imewafanya waitwe ikulu Kwa heshima na siyo kwenda tu: lakini pamoja na nguvu waliyonayo kwanini wanavifanya vyama vingine kama siyo wapinzani? Akina Lipumba na Zito hata Mbatia wamepotelea Wapi kwenye ramani ya siasa?

Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?

Chadema ndio chama kikuu Cha upinzani, ndio wamebeba hatima ya mama. Wakimshambulia Mama atapata wakati mgumu.
 
Watu ambao walipata 40% ya kura za urais huwezi kuwadharau, labda uwe kichaa kama Jiwe
 
Chadema wamesimama imara na misimamao Yao imewafanya waitwe ikulu Kwa heshima na siyo kwenda tu: lakini pamoja na nguvu waliyonayo kwanini wanavifanya vyama vingine kama siyo wapinzani? Akina Lipumba na Zito hata Mbatia wamepotelea Wapi kwenye ramani ya siasa?

Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?
Chadema inaifanya CCM izibe masikio kila neno 'Katiba Mpya' linapotajwa.
Chama cha Mapinduzi kinaamini kwamba hakiwezi kuishinda Chadema katika Uchaguzi huru na wa haki.
Kwa hali hiyo, kamwe, nchi yetu haitopata Tume Huru ya Uchaguzi!
Nani anakubali kuachia Kitumbua mdomoni?
SSH ana Hesabu kali.
Kui-'contain' Chadema Tanganyika kama CCM ilivyo-i-'contain' CUF (na sasa ACT) Zanzibar.
 
Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?

WaTanzania akiwemo Mh. Rais Samia Suluhu Hassan wameona kuwa wananchi wanahitaji mabadiliko, Rais Samia Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM pamoja na safu ya juu ya sasa ya uongozi wa CCM wakiwemo makamu mwenyekiti wa CCM Abdulrahaman Kinana, katibu mkuu Daniel Chongolo, waziri wa katiba George Simbachawene, katibu uenezi Shaka na wengine ndani ya CCM wamebaini mabadiliko hayo hayawezi kusimamiwa na CCM wananchi wakayabariki hivyo kuamua lazima chama kikuu cha upinzani Tanzania kishirikishwe

Toka Maktaba :

Toka Maktaba :

17 Feb 2020
Samia Suluhu : "Napenda mawazo ya wapinzani, huwa wanajenga hoja vizuri, walini 'inspire' niingie siasa"

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefunguka kuhusiana na historia ya maisha yake ambapo ameeleza siri ya mafanikio na chanzo kilichomvutia kuingia kwenye siasa. Samia Suluhu anaona hoja za upinzani ni moto, zimejaa mantiki kuliko za mawaziri wa serikali ya CCM , hivyo walinivutia / inspire, mimi ni activist ... kuingia siasani baada ya kuona majibu na hoja za upande wetu (CCM) hazina uhalisia na hazijibu maswali ya wananchi ....

Chadema wamesimama imara na misimamao Yao imewafanya waitwe ikulu Kwa heshima na siyo kwenda tu: lakini pamoja na nguvu waliyonayo kwanini wanavifanya vyama vingine kama siyo wapinzani? Akina Lipumba na Zito hata Mbatia wamepotelea Wapi kwenye ramani ya siasa?

Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?
chama kikuu cha upizani. Beatrice chama gani kina wanachama zaidi laki moja Tanzania? CUF?, ACT?, Chauma? It is only Chadema with a few millions.
 
16 Fevrier 2022
Brussels, Ubelgiji

Hongera mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuishi katika imani kuwa Tanzania ni ya wote bila kujali tofauti za kiitikadi na vyama

1653099721178.png

Picha : Mh. Rais Samia Hassan alipokutana na Tundu Antipas Lissu makamu mwenyekiti wa CHADEMA anayeishi uhamishoni jijini Brussels Belgium.
 
20 May 2022
Dodoma, Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo mei 20, 2022 ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino

Kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma, Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho. Aidha pia viongozi wa CCM wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Abdulrahman Kinana, katibu mkuu Daniel Chongolo, katibu uenezi Shaka walishiriki kikao hicho
 
21 May 2022
Dodoma, Tanzania

Furaha na bashasha zaonekana ktk nyuso za viongozi wa CCM na CHADEMA walivyokutana Ikulu ya Chamwino

Chadema wamesimama imara na misimamao Yao imewafanya waitwe ikulu Kwa heshima na siyo kwenda tu: lakini pamoja na nguvu waliyonayo kwanini wanavifanya vyama vingine kama siyo wapinzani? Akina Lipumba na Zito hata Mbatia wamepotelea Wapi kwenye ramani ya siasa?

Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?
Mahaba yako tu kijana.
Aliekuambia wameitwa kwa heshima ni nani?
Wangeitwa kwa heshima ndio Mbowe angeenda Ikulu peke yake masaa manne tu baada ya kutoka jela? Yaani kapewa muda wa kuoga na kunyoa na kubadili nguo tu?
Lissu mwenyewe ndio aliomba kuonana na Bi mdashi kule Ubelgiji.
Je hapo wameitwa au waliomba kuitwa?
Isitoshe wameitwa na mwenyekiti wa CCM sio Rais manake simuoni Makamu au Waziri Mkuu au Katibu Kiongozi au Mwanasheria Mkuu au oficer yeyote wa serikali zaidi ya
Mwenyekiti wa CCM SSH
Makamu Kinana
Katibu Chongolo..
Wamedanganywa na Jengo la Ikulu tu basi.
CDM WAMEITWA NA CCM WAKAENDA KWA HESHIMA ZOTE
 
CHADEMA ni wadau muhimu ambao bado mpaka sasa hawajajiunga na Kikosi kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vya Siasa nchini Tanzania

Katika ripoti hii tunakuletea orodha ya wajumbe wa Kikosi kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vya Siasa nchini Tanzania kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Lengo ni kutafuta muafaka wa kitaifa kuhusu masuala ya siasa, haki na demokrasia. Wajue wanaokuwakilisha katika makala hii.

Back
Top Bottom