Kwanini CHADEMA wanaonekana wa muhimu kuliko vyama vingine awamu ya sita?

Kwanini CHADEMA wanaonekana wa muhimu kuliko vyama vingine awamu ya sita?

Mbona mama anakutana na wote, habagui mama yetu, juzi tu alikuwa na zitto baadae akukutana na lipumba
 
Ukweli mtupu. Zile siasa za huko nyuma ni hayawani tu anaweza kuzifurahia. Dunia tunapita tutende yanayofaidisha jamii
Wakati Mbowe yupo ndani Samia alipokuwa anapost kitu Tweeter, 90% ya comments zilikuwa Mbwowe sio gaidi[emoji3]
 
Ukitaka kujua nguvu ya chadema waulizeni ccm nyakati za uchaguzi wanachokipitia huko majimboni na ndio maana zaidi ya miaka kadhaa chadema kimekua bara barani hakijaigia gereji,sasa wengine wanaobeza wanafikiri wanaweza kuwa chama kikuu cha upinzani tanzania,kumbuka wao wanaserekali Zanzibar lkn bado serekali na ccm wanaihofia chadema na sio wao kwahiyo wanapobeza tunawaona ni watu walioshindwa tu
 
Lissu anaviita vyama vya makaratasi

20220512_231057.jpg


20220318_182516.jpg
 
Chadema ni chama makini na mahiri.
Wamepitia machungu mengi na hili ndilo limewapa krediti kuwa pamoja na mateso na vifungo bado wako imara.

Kuhusu vyama vingine ccm haiwezi kuwapa umuhimu sawa na chadema kwasababu wana ndimi mbili.

ACT hawakljulikani wanasimamia nini.
Mbatia alianza usaliti enzi za jiwe.
Cuf tayari waneanza na kampeni Samia ashinde.

CCM ni kama shetani.
Shetani huwa hapambani na wenye dhambi anajua ni watumishi wake bali hupambana na watakatifu na wacha Mungu.
Mshana Jr jr
Duuuh shikamooo
 
Chadema ni chama makini na mahiri.
Wamepitia machungu mengi na hili ndilo limewapa krediti kuwa pamoja na mateso na vifungo bado wako imara.

Kuhusu vyama vingine ccm haiwezi kuwapa umuhimu sawa na chadema kwasababu wana ndimi mbili.

ACT hawakljulikani wanasimamia nini.
Mbatia alianza usaliti enzi za jiwe.
Cuf tayari waneanza na kampeni Samia ashinde.

CCM ni kama shetani.
Shetani huwa hapambani na wenye dhambi anajua ni watumishi wake bali hupambana na watakatifu na wacha Mungu.
Mshana Jr jr
Hili jibu zuri sana
 
Chadema wamesimama imara na misimamao Yao imewafanya waitwe ikulu Kwa heshima na siyo kwenda tu: lakini pamoja na nguvu waliyonayo kwanini wanavifanya vyama vingine kama siyo wapinzani? Akina Lipumba na Zito hata Mbatia wamepotelea Wapi kwenye ramani ya siasa?

Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?
Ukijiheshimu lazima utaheshima tu hakuna namna tofauti na yale mazwazwa kama Zito na genge lake
 
Baada ya wadau lukuki wa kimataifa kuibana Tanzania katika nyanja mbalimbali, sasa serikali imeona umuhimu wa wapinzani wa kweli kushirikishwa, na sasa tunaona CHADEMA wakiitwa Ikulu kusaidia mustakhabali wa nchi


TOKA MAKTABA :

25 April 2022

TANZANIA KUPIMWA , HIVYO TUME YA UMOJA WA MATAIFA (UN) HAKI ZA BINADAMU YATUA TANZANIA


Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya UN yatua nchini; hiki ndio wanachofanya kufuatilia ahadi ilizotoa Tanzania, pia serikali yabanwa na UN kuwa iwe wazi waTanzania wafahamu serikali yao iliridhia nini ktk masuala 252 iliyosaini na kuikubali kwa niaba ya wananchi



Timu ya umoja wa mataifa inayoshughulikia Haki za Binaadamu na utawala bora imekuja nchini kujadiliana na Tume ya Haki za Binaadamu na utawala bora juu ya masuala mbalimbali yanayohusu haki za binaadamu ikiwemo haki za binaadamu katika wananchi kufahamishwa ni mikataba gani inayohusu haki za binadamu iliyoridhiwa na serikali ya Tanzania iliyoridhia huko Geneva Uswisi Ofisi za Kamishina wa UN wa Haki za Binadamu kama anavyotueleza Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala bora Nchini Tanzania Human Rights Council Adopts Outcomes of Universal Periodic Review of Saint Vincent and the Grenadines, Papua New Guinea, Tajikistan and Tanzania
 
Kwa nchi ya Tanzania chama cha CHADEMA ndiyo habari ya sasa kubwa katika kurasa za mbele za magazeti, mitandao, mabaraza, radio, televisheni, makongamano, kubadilishana mawazo, sera mbadala za kiuchumi, katiba mpya n.k soma zaidi source: CHADEMA | DW | 17.05.2022

 
Ukweli ni kwamba bila CHADEMA hakuna jambo la kisiasa hapa Tanzania litakuwa halali.

Walipoanza kukutana kwenye "semina" zao, wakaanza kupiga madongo eti "wamesusa sisi twala", wenzao wanajua nini wanafanya.

Kwa ufupi CHADEMA wamekataa kuwekwa kundi moja na vibaraka.
 
09 March 2022
Iringa, Tanzania

Mbowe ateta na RC, RPC Iringa​


MBOWE PIC

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa (RC), Queen Sendiga


Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa (RC), Queen Sendiga na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa (RPC), Allan Bukumbi.

Amesema mazungumzo yao yalihusu yale ambayo walizungumza na Rais Samia Suluhu Hassan hasa kuhusu mshikamano, kusaidiana, upendo na kuheshimia ili kuifanya Tanzania kuwa mahali bora pa kuishi.

Soma zaidi : Source : Mbowe ateta na RC, RPC Iringa
 
TOKA MAKTABA :

12 April 2021

CHADEMA YATAKA KUONANA NA RAIS

1653132816313.png

Chadema kimeomba kuonana na rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan, kiongozi mkuu wa Chadema ameeleza.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema amemuandikia Rais Samia barua kumuomba kuonana naye ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali utakaoliletea taifa furaha, haki na ustawi.

Akizungumza na vyombo vya habari Jumapili Bw Mbowe alisema "Wote tumejifunza, serikali ikiharibikiwa, nchi yote inaingia simanzi. Hii haina maana sisi wa Chadema tumegeuka waimba mapambio wa Rais Mama Samia. Inatupa sisi changamoto ya kuongeza juhudi za kuboresha sera zetu na kuongeza ushindani wa hoja."

Bw Mbowe amesema wanategemea kumweleza Mama Samia na kumkabidhi mapendekezo yao kadhaa ya kina ya namna bora ya kuanza upya katika azma ya "kujenga utengemano wa nchi" na akaongeza kuwa wanaamini atatambua nafasi ya vyama vya upinzani.

"Hatupaswi kumtakia mabaya kwa sababu tu ni zao la CCM. Bali tunatakiwa kuongeza juhudi na maarifa kumkabili kwa ushindani wenye kujenga na siyo kubomoa. Tunamwombea afanye mema wakati wa utawala wake ili kupata ustawi wa taifa letu."

Bw Mbowe amesema kuwa: "kauli za rais, Mama Samia Suluhu Hassan zinatuchanganya na anapaswa kulijua hili. Anapoongea nia yake ya kuenzi sera, mipango na tabia ya Magufuli, taifa linasinyaa na kuhuzunika."

Source : https://www.bbc.com/swahili/live/habari-56714475
 
Back
Top Bottom