Kwanini CHADEMA wanaonekana wa muhimu kuliko vyama vingine awamu ya sita?

Kwanini CHADEMA wanaonekana wa muhimu kuliko vyama vingine awamu ya sita?

Chadema ni chama makini na mahiri.
Wamepitia machungu mengi na hili ndilo limewapa krediti kuwa pamoja na mateso na vifungo bado wako imara.

Kuhusu vyama vingine ccm haiwezi kuwapa umuhimu sawa na chadema kwasababu wana ndimi mbili.

ACT hawakljulikani wanasimamia nini.
Mbatia alianza usaliti enzi za jiwe.
Cuf tayari waneanza na kampeni Samia ashinde.

CCM ni kama shetani.
Shetani huwa hapambani na wenye dhambi anajua ni watumishi wake bali hupambana na watakatifu na wacha Mungu.
Mshana Jr jr
Well
 
Mpaka mwezi uliopita Chadema ilikuwa na zaidi ya Wanachama mil 12 , hii ni kwa mujibu wa Chadema digital
habari njema. Erythrocyte , jaribu kutafuta namna ya kumjibu Slaa maana hili lizee linaonekana kuota mapembe. Mjibuni kama chama kieleweke. FACTS!
 
Chadema wamesimama imara na misimamao Yao imewafanya waitwe ikulu Kwa heshima na siyo kwenda tu: lakini pamoja na nguvu waliyonayo kwanini wanavifanya vyama vingine kama siyo wapinzani? Akina Lipumba na Zito hata Mbatia wamepotelea Wapi kwenye ramani ya siasa?

Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?

Nasikia ACT cha Zitto ndio chama kikuu cha upinzani
 
Hao wengine sio wapinzani ni wenzao wanaojivika upinzani.

Tuliwambia siku ya kukutana na Rais hakuna mtu mwingine atajichomeka mkabisha.

Chadema ndio kiboko yao.

Chama la watu
Hata CUF ya Lipumba wameenda ikulu wenyewe, hakuwepo wakujichomeka.
 
Uamuzi wa busara wa Mh.Rais kuzungumza na Wapinzani wake ni Muhimu sana kwa maslahi ya Nchi na wananchi wake

Mahusiano mema ya Mh.Jakaya na Chadema yalisaidia sana utawala wake kuwa rahisi na kumaliza kwa mafanikio

Mh.Mbowe na Chadema yote wanatambua Siasa za masikilizano huimarisha sana chadema kuliko Siasa za nginja nginja
Sawa kabisa
 
Tanzania inazidi kusikiliza hoja za CHADEMA kuhusu haki, kupitia ushawishi wa hoja za CHADEMA serikali ya Mh. Rais Samia Hassan inazidi kutoa ahadi kwa taasisi za kimataifa kuwa taifa letu linaelekea tofauti na kipindi cha 2015 - 2021

Mhe. Balozi Maimuna Tarishi akutana na Rais wa Baraza la Haki za Binadamu​

  • 29 Apr 2022


Tarehe 28 Aprili 2022, Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu Geneva alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Haki za Binadamu, Balozi Federico Villegas (Mwakilishi wa Kudumu wa Argentina).

Pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi alimpongeza kwa mara nyingine tena kwa kushika madaraka ya Rais wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa; pia kwa kuendesha na kusimamia kwa umahiri mkubwa kikao cha 49 cha Baraza hilo.

Aidha, Mhe. Balozi alimuhakikishia kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Uwakilishi Geneva itaendelea kushirikiana na Baraza la Haki za Binadamu na kwamba nchi ipo makini na imedhamiria kwa dhati kuendelea kutekeleza wajibu wake wa kusimamia misingi ya Haki za Binadamu kwa wananchi wake.

Kwa upande wake, Balozi Villegas alipongeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushiriki wake kwenye tathmini ya hali ya haki za binadamu na hususan kwa kuidhinishwa kwa Taarifa ya hali ya haki za binadamu na kwa kukubali kutekeleza mapendekezo mengi yaliyotolewa na wadau.

Aidha, ameelezea kuwa tayari kushirikisha Uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa majukumu na kazi mbalimbali za Baraza hilo.

Source : Mhe. BaloziTarishi akutana na Rais wa Baraza la Haki za Binadamu | Tanzania Mission to the UN, Geneva
 
Sera za Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu za chama cha CHADEMA zinazidi kuishawishi serikali ya CCM awamu ya 6 ibadilike na kurahishisha serikali ya Tanzania kuanza kuaminika na kusaidiwa na jumuiya za kimataifa pamoja na wadau wa maendeleo wa kimataifa



Tanzania Mission to the United Nations
Geneva, Switzerland

Tanzania yahudhuria Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu​


Picha : waziri wa sheria na katiba Mh. George Simbachawene akiwa Geneva alipokwenda kuelezea hali ya kisiasa na haki za binadamu iliyopo Tanzania ktk awamu ya 6 .



1. Tanzania yahudhuria Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu, ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanyiwa tathmini ya Haki za Binadamu. 2. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (Mb.) ameongoza Ujumbe wa Tanzania ambapo ameeleza hatua mbalimbali zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye masuala mbalimbali ya Haki za Binadamu nchini Tanzania ikiwemo Elimu, Afya, Haki za Watoto, Wanawake, wenye ulemavu, Haki za Kisiasa na mengine mengi. 3. Tathmini ya Tanzania imekubaliwa na Baraza hilo, nchi 23 zilizoizungumzia Tanzania kwa hatua nzuri zilizofanyika katika kuhakikisha Haki za Binadamu zinazingatiwa. Pia wamekumbusha Tanzania kuendelea kutatua changamoto zilizobaki.
 
HAKI NA UWAZI WANAYOIPIGANIA CHADEMA YAKUMBATIWA NA SERIKALI YA AWAMU YA 6 YA CCM NA KURAHISISHA MAHUSIANO YA TANZANIA KIMATAIFA

KIKAO CHA 49 CHA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU : WAZIRI SIMBACHAWENE AZUNGUMZA NA TUME YA HAKI ZA BINADAMU, 'UHURU WAONGEZEKA SHERIA ZAIDI YA 400'



Tarehe 2 March 2022 Tanzania kupitia waziri wa Katiba na sheria Mh. George Simbachawene aliwasilisha ripoti ya nchi ya kukuza na kulinda haki za binadamu na uwazi zilizopo nchini Tanzania.
 
Unadhani ukiwa msaliti utapewa jina gani zuri zaidi la msaliti mtu anaitwa msaliti si kwa sababu ya kwenda Ikulu mtu anaitwa msaliti kwa matendo yake. Na siku zote wasaliti huja kuabika kwa aibu

Akienda Zitto msaliti, Lipumba msaliti ila akienda Mbowe na Mnyika wao ni wapinzani wa maana?

Hii siasa ya wapinzani wa CCM ni ya kipumbavu sijawai kuona akili na mawazo yao ni kuitwa Ikulu tu
 
Chadema wamesimama imara na misimamao Yao imewafanya waitwe ikulu Kwa heshima na siyo kwenda tu: lakini pamoja na nguvu waliyonayo kwanini wanavifanya vyama vingine kama siyo wapinzani? Akina Lipumba na Zito hata Mbatia wamepotelea Wapi kwenye ramani ya siasa?

Lakini pia kuitwa kwao ikulu kimkakati Toka Lisu akutane na Mhe. RAIS mbona kama kunawafanya akina Mdee waonekana kama wanadhalilika? Vyama vingine vitajikwamua vipi mikononi mwa CCM kama Chadema itaamua kusimana yenyewe kama inavyofanya Sasa?
ACT wako na chama tawala kwa misingi inayotia shaka sana. Mwaka 2005 CUF ilifanya vizuri sana kwenye uchaguzi na kupata kura takriban 800,000 ukanda wa pwani. Mwaka 2010 kura hizo zilihamia ccm katika mazingira ya kutatanisha. Kwa sehemu kubwa hiyo CUF ndiyo imegeuka kuwa ACT na mikakati hiyo tata inaendelea kushamiri. Angalau hivi karibuni NCCR baada ya kushuhudia ni kwa kiasi gani watawala wako tayari kuumiza wanasiasa wa ushindani amejaribu kujirudi na kuungana na Chadema. Hata hivyo yaliyotokea juzi ni dalili kuwa watawala hawalali.
 
Tundu Antipas Lissu akitoa muhadhara katika skuli ya The Elliot ya masuala ya kimataifa iliyojikita kuhusu mambo ya Afrika ktk Chuo Kikuu cha George Washington nchini Marekani

George Washington University
The Elliott School of International Affairs' Institute for African Studies



The Elliott School of International Affairs' Institute for African Studies welcomed Tanzanian opposition leader and chief whip Tundu Lissu for a conversation with students, faculty, and the community.
 
Akienda Zitto msaliti, Lipumba msaliti ila akienda Mbowe na Mnyika wao ni wapinzani wa maana?

Hii siasa ya wapinzani wa CCM ni ya kipumbavu sijawai kuona akili na mawazo yao ni kuitwa Ikulu tu
Zitto anajulikana ni kibaraka tangu enzi za JK. Huyo lipumba ndio kabisa alitumika na ccm kuigawa cuf mpaka maalim na wafuasi wake hasa Zbar wakaamua kuanua tanga na kuhamia kwa Act.
Chama Pekee makini cha upinzani ni Chadema. ✌️✌️
 
Nairobi, Kenya

#MboweInKenya #MwanzoTv Mahojiano maalum na Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)



Katika mahojiano haya maalum Mwenyekiti Freeman Mbowe akizungumza kama mwana filosofia anayelingalia changamoto zinazolikumba taifa la Tanzania kiundani na kutoa mbadala wa jinsi ya kuyatatua masuala ya kiuchumi, kukuza biashara baina ya mataifa ya kiafrika za kuvuka mipaka, masuala ya kijamii, kidemokrasia, ujenzi wa taifa, mahusiano ya kimataifa na umuhimu wa kuwa na mihimili ya dola iliyo huru pamoja na taasisi zinazotekeleza sera za nchi bila kuingiliwa sana na wanasiasa bali zinazoweza kuwashauri viongozi ili nchi za Afrika hususan Tanzania iwe bora zaidi katika nyanja zote.
Source : Mwanzo TV
 
Back
Top Bottom