Kwanini CHADEMA wanaonekana wa muhimu kuliko vyama vingine awamu ya sita?

Chadema hawanunuliki Kama kina Zitto,Lipumba,shibuda ,Chiyo na wengineo.Ngogwe walikuwa wanajipa umuhimu ambao hawana,ndiyo maana wanaishia kwenye Fiesta.

Wanasiasa wananunulika Sema na nani? ndo swali.
 
Hizi sera ndio zilifanya US, German, UK zifike hapo zilipo.
 
Mbowe ni noma. Ni Jembe
 
hakina umuhimu wowote, na wanajifanya wa muhimu kwenyw hamna, nilichogundua viongozi wote wa upinzani walimmis sana kwenda ikulu enzi za JPM kumbe wanapapemda bwana
Popomalism....
 
Lipumba ameshatoa msimamo wake kuwa amesoma alama za nyakati,Mbatia anapambania uenyekiti wake dhidi ya wasaliti waliopandikizwa chamani ili kumsambaratisha Mtoto wa Mama Tanzania.Zitto ni mwanatimu iliyopendekeza kuwa Katiba Mpya ya wananchi wa Tanzania ya Tanganyika na Zanzibar iandikwe baada ya uchaguzi wa 2025.Je,ulitaka CDM iwasubiri watu hao kudai Katiba Mpya?
Tuache kudandia mbeleko la CDM,wamesimamia msimamo wa kudai Katiba Mpya usiku na mchana bila kujali maumivu waliyopitia.
 
Chadema ni chama makini na mahiri.
Wamepitia machungu mengi na hili ndilo limewapa credit kuwa pamoja na mateso na vifungo bado wako imara.

Jambo usilolijua ni kwama; mateso huimarisha na ukiimarishwa huja heshima.
[emoji1534][emoji1534][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji626][emoji95]
 
23 May 2022
Makao Makuu ya CHADEMA
Mtaa wa Ufipa
Kinondoni DSM


Katibu mkuu wa CHADEMA kamanda John John Mnyika anazungumza


KATIBU Mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) John Mnyika, leo Mei 23, amezungumza na wanahabari kuhusiana na kikao walichokifanya na Rais Samia Suluhu, ikulu Chamwino jijini Dodoma.
 
Sawa mlinda ligase. Unafahamika kwa kutema pumba jukwaa nzima. Unajipendekezaga upate teuzi. Hovyooooo. Ptuuu mate usoni
Teuzi zina wenyewe mkuu. Maoni yangu tu labda yanakuwa tofauti na ya wengine ndio maana wapo wanaodhani kuwa navizia teuzi au najikomba.
 
Cdm ni chama pekee hapa Tanzania chenye kusimamia haki na ndiyo chama pekee cha upinzani.
 
Akienda Zitto msaliti, Lipumba msaliti ila akienda Mbowe na Mnyika wao ni wapinzani wa maana?

Hii siasa ya wapinzani wa CCM ni ya kipumbavu sijawai kuona akili na mawazo yao ni kuitwa Ikulu tu
Wewe ndiye utakuwa ni mpumbaf
 

01 September 2022

Masuala ya haki jinai (criminal justice), kituo cha Sheria na Haki za Binadamu

Kituo cha #Sheria na #Haki za #Binadamu (#LHRC) kimesema kwamba kauli na dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuona mageuzi kwenye mfumo wa utoaji haki jinai nchini #Tanzania ni vya kupongezwa huku kikibainisha hatua kadhaa ambazo #Serikali inaweza kuchukua kufanikisha mageuzi hayo. Ikumbukwe kwamba hii siyo kauli ya kwanza kwa Rais Samia kuhusiana na masuala haya ya haki jinai, kwani mnamo Agosti 2021, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alisema kwamba uwekaji wa mahabusu kizuizini kwa muda mrefu siyo tu unaleta mzigo kwa Serikali, bali pia ni ukiukwaji wa haki zao za msingi

Source : Haki TV
 
Ni kwa sababu baadhi yao ambao ndio wako madarakani kwa sasa walikuwa ni washirika wa siri na chama hicho enzi za utawala wa JPM ndio maana wanafanya kila wawezalo kuhakikisha hawawajeruhi kisiasa wasije wakaanika wazi maovu yao
 
WaTanzania waiangukia CHADEMA, waililia iseme jambo kuhusu tozo .

Kilio hicho kinaonekana ktk mitandao ya kijamii kutokana na suala la tozo kuleta ugumu katika akiba zao za fedha ktk mabenki na akiba za fedha ktk simu zao .

Hii imekuja baada ya kuiona serikali inaburuza miguu yake kuchukua hatua kuwanusuru wananchi na mzigo mkubwa wa kodi unaolenga pato moja mfano mishahara yao inayopitia benki au mikopo ya elimu ya juu ya wanafunzi inayopitia benki kuanza kukamuliwa tozo kila wanapokwenda kuchukua chanzo hicho za fedha zao na hii inakuwa mara kadhaa akauti zao kukatwa kodi hivyo kuleta athari kubwa ktk maisha yao ya kila siku yaliyolazimisha kutumia huduma za miamala ktk benki na miamala ya simu.
 
WANANCHI WAKATA TAMAA JUU YA WABUNGE WALIOSHINDA UCHAGUZI 2020

Wananchi sasa wahisi na kuamini kuwa bungeni hawana ushawishi wala hawana matumaini kuwa tarehe 13 September 2022 Bunge litapokutana watajadili suala la tozo / kodi au kuibana serikali ya CCM.

Ndani ya bunge la chama kimoja hakuna wale backbenchers wanaokisukuma chama chao kuhusu hoja tata kama tozo, inaonekana wamefungwa minyororo ya kisiasa kiasi hata nje ya bunge hawana utashi wala msukumo wa kutoa mawazo mbadala kama kubana matumizi ya kifahari na anasa ya uendeshaji serikali na marupurupu ya watumishi vigogo wa serikali n.k ili fedha hizo pia ziindizwe kwenye solidarity fund


TOKA MAKTABA
BUNGE LAAHIRISHWA HADI SEPTEMBER 13, 2022


Bunge Laahirishwa Hadi Tarehe 13 Septemba 2022

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa 7 wa Bunge ....source : Parliament of Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…