Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

Pwani ni kubwa sana hiyo ndio iliktakiwa kugawanywa. Wanaenda kuunda mkoa ambao hata wilaya hazijitoshelezi wanaziomba mikoa mingine. Huu ni ujinga n upuuzi.
 
Naona unachanganya vitu hapa, kama ilivyopendekezwa mkoa wa chato hauzalishwi kutoka mkoa wa geita kama unavyodai bali ni kutoka mikoa mitatu ya Kagera, Kigoma na geita. Kwa hiyo madai yako hayana msingi kabisa, labda kama kuna hoja nyingine
 
Mkuu huwezi kumega mkoa kwa kuangalia ukubwa tu, tuangalie na idadi ya watu pia. Kwa mfano mkoa kama Tabora ni mapori tu. Mikoa ya kanda ya ziwa imekuwa na ongezeko kubwa la watu mfano mkoa wa Kagera ni halali kuupunguzia mzigo maana ni wa tatu kwa idadi ya watu Tanzania nyuma ya Dar na Mwanza
 
Kwani wenyewe kakonko wamesema hawataki kutenganishwa na ndugu zao?? Au ni mawazo yako??? Mbona kuna uzi humu wakiomba mkoa wa nyakanazi kwa sababu kwenda Kigoma mjini ni mbali sana??
 
1. Morogoro
2. Pwani
3. Tabora
4. Lindi hii ni ya kukata kwanza kabla ya Geita iyo changa na ndogo
Hivi mbona mnaisena geita tu wakati inamegwa mikoa mitatu?? Hivi population ya Lindi ukiitenga si utaunda mkoa wa mapori tu??
 
" The United States of America (U.S.A. or USA), commonly known as the United States (U.S. or US) or America, is a country primarily located in North America. It consists of 50 states, a federal district, five major unincorporated territories, 326 Indian reservations, and some minor possessions.[g] At 3.8 million square miles (9.8 million square kilometers), it is the world's third- or fourth-largest country by total area.[c] With a population of more than 331 million people, it is the third most populous country in the world. The national capital is Washington, D.C., and the most populous city is New York City".
Nimekuwa najifikiria sana tena sana ukubwa wa USA na nchi yetu nani zaidi? Sijasikia USA wakianzisha majimbo kwa kumega jimbo jengine kwa kigezo cha kusogeza maendeleo, sie hatulali kwa kufikiria kubuni mikoa. AIBU tupu.
 
Labda angefanya ushawishi makao makuu ya mkoa wa Geita yawe Chato. JPM alikuwa na mazuri pamoja na mabaya yake baba yetu. RIP Mr. president.
Hii imekaa poa sana. Pana mikoa ambayo makao makuu yake ni tofauti kwa jina; mfano Mara ( Musoma ), Kilimanjaro ( Moshi ), Pwani ( Kibaha ) na kadharika.
 
Tatizo Jina au eneo? Basi mkoa uundwe haalafu uitwe mkoa wa Kasomi na wilaya zake pendekezwa ikiwemo Chato. Hapo vipi
 
Hatutakiwi kuyakataa maendeleo, hata kama yanakuja kwa wale tusiowapenda.

Mada yako ilitakiwa kujikita kutoa ushauri kama ifuatavyo. Wakati serikali ikifikiria kuunda mkoa mpya wa Chato, iangalie namna ya kuunda mikoa mipya kwa kugawanya mikoa (taja) .... kwa madhumuni yaleyale ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.

Hatutakiwi kupinga kila kitu.
 
Chukua pepsi baridi nalipa
 
Halafu hao huyo mkuu wa mkoa wa Geita anatoa mapendekezo hadi ya Kigoma ,Kagera na Mwanza kama nani? Yeye ajiongelee ya Geita kuhusu kuitohoa Chato, na Busanda sijui Mbogwe, ya Kigoma,Kagera na Mwanza awaachie RCC husika. Je kama nawao wakizikatalia wilaya zao kama wao geita walivozikatalia zao na wamekataa hadi kutohoa kata kuunda wilaya ya Katoro/Buselesele.
 
Hawabuni mikoa wanabuni ulaji
 
Hii imekaa poa sana. Pana mikoa ambayo makao makuu yake ni tofauti kwa jina; mfano Mara ( Musoma ), Kilimanjaro ( Moshi ), Pwani ( Kibaha ) na kadharika.
Ingefaa sana mkuu, alafu baada ya kuwa makao makuu ya mkoa wa Geita kwa miaka labda 25, sasa baade ndio anaomba sasa Chato kuwa mkoa kamili kwa maana unakuwa umechangamka kibiashara.
 
Tatizo la viongozi wakishashiba ndio hilo. Hawatumii akili zao vizuri kufikiri badala yake wanatafuta kiki kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…