Sababu ni nyingi,
Kwanza lazima ufahamu China wana msingi mkubwa wa uvumbuzi na ubunifu wa miaka mingi. Dira, gunpowder, karatasi na mashine za kale za kuchapa ziligunduliwa China.
Pili udikteta wa China ni udikteta wa mfumo wa meritocracy, sio udikteta kama wa Waafrika wa "unanijua mimi ni nani" au baadhi ya familia kuhodhi utawala wa nchi.
Lingine demokrasia ni muhimu sana lakini haikupi kila kitu, ili demokrasia ikusaidie inahitaji mazingira wezeshi pia ambayo hayako kwa nchi nyingi za Africa.
Mfano ni kutokuwepo utamaduni wa rushwa, nepotism, ukabila, raia wengi wajinga n.k