A
Anonymous
Guest
Naomba kuwasilisha kero kuhusu uwekaji wa dampo la takataka kwenye njia ya watembea kwa miguu katika barabara ya kuelekea U-turn ya Daraja la Mirongo, Jiji la Mwanza.
Uamuzi huu umeleta usumbufu mkubwa kwa watembea kwa miguu, kwani njia hiyo sasa imezibwa na kuwalazimisha baadhi ya watu kutembea karibu na barabara kuu, hali inayoweza kuhatarisha usalama wao kutokana na magari yanayopita.
Tunaomba uongozi wa Jiji la Mwanza ufanyie kazi suala hili na kuliondoa dampo hilo katika eneo la njia ya watembea kwa miguu. Ni muhimu kuhakikisha miundombinu ya watembea kwa miguu inabaki salama na inatumika kwa madhumuni yake.