Kwanini Demokrasia ilishindwa kuleta maendeleo China?

Kwanini Demokrasia ilishindwa kuleta maendeleo China?

Kilombelo

Member
Joined
May 27, 2021
Posts
98
Reaction score
127
Bila shaka majibu yatapatikana hapa,

Unadhani ni kwa nini Wengi huamini maendeleo makubwa hutokana na Ustawi mkubwa Democrasia

Kama ni ukweli, Ni kwa nini sasa Democrasia ilishindwa kuleta maendeleo China?

Mwingine atauliza, ni lini China imewahi kuwa na Demokrasia na hata ikaamua kuivunja, nami nitauliza, ni kwanini tunaojaribu kutembea kwenye Demokrasia ndio tunaendelea kuwa masikini wa kutupwa?

Natamani sana nchi zetu za Afrika na hasa Tanzania, tufunge ndoa na china katika kuendesha nchi yetu.

Ninauhakika, itakuwa ni miaka michache sana kufikia uchumi mkubwa na tutaondokana na umasikini.

Demokrasia ndiyo inayowafanya watu washinde kutwa nzima wamejifungia kwenye kumbi mbalimbali kuwasikiliza wanasiasa kwa mambo ya kipuuzi huku hawaingizi chochote na hawafanyi kazi.

Demkrasia, ndiyo hiyo inayowafanya watu waache shughuli zao wakandamane kwa faida ya wanasiasa siyo?

Ole, siku moja niwe Rais wa nchi hii, mabeberu wataninyonga mapema asubuhi nakwambia.

Ni mara tano ya JPM kwa mwendo wake

Mungu bariki Viongozi wote Jasiri
 
Shida ya hio mfumo wa china ya afrika, watawala ni mungu watu hata wapige dili vipi,wajenge vijijini kwao awashughulikiwi, uhamishwa tu alikuwa mbunge kesho anapewa uwaziri.

Ni rahisi kwa mtumishi wa kawaida kufukuzwa Kazi kwa sababu kapewa asante ya sh 2000 na Yale majizi makubwa sugu uhamishwa tu vitengo.

China hakuna aliyejuu ya Sheria
 
Kwa uelewa wangu China walikuwa na utawala wa KIFALME ambao ulipinduliwa ndipo ukaingia utawala wa mfumo walionao leo hii.

Labda ungepima maendeleo ya China vs Taiwan. Mataifa hayo yalikuwa nchi moja, lakini yalikuja kutengana ambapo Taiwan ilifuata demokrasia na ubepari, na China ilifuata ujamaa na ukandamizaji.
 
Ukisema China haina Demokrasia, jibu kwanza hili swali. Demokrasia ni nini?
 
Ukisema China haina Demokrasia, jibu kwanza hili swali. Demokrasia ni nini?
Ni pamoja na kukuta jamaa linavunja pale BoT linaiba matrioni ya fedha, haupaswi kulipeleka jera moja kwa moja, ila hadi lishitakiwe miaka na miaka likizitumia hizo fedha kuhonga wanasheria njaa na mahakimu na wananchi wakiendelea kukosa huduma mhimu.

huo ni mfano mojawapo wa Demokrasia, najaribu tu mkuu
 
Ni pamoja na kukuta jamaa linavunja pale BoT linaiba matrioni ya fedha, haupaswi kulipeleka jera moja kwa moja, ila hadi lishitakuwe miaka na miaka likizitumia hizo fedha kuhonga wanasheria njaa na mahakimu na wananchi wakiendelea kukosa huduma mhimu

huo ni mfano mojawapo wa Demokrasia, najaribu tu mkuu
Demokrasia huwa Hakuna viroba baharini
 
..Kwa uelewa wangu China walikuwa na utawala wa KIFALME ambao ulipinduliwa ndipo ukaingia utawala wa mfumo walionao leo hii.

..Labda ungepima maendeleo ya China vs Taiwan. Mataifa hayo yalikuwa nchi moja, lakini yalikuja kutengana ambapo Taiwan ilifuata demokrasia na ubepari, na China ilifuata ujamaa na ukandamizaji.
Taiwan haikufuata na demokrasia wala ubepari jinsi ulivyo.

Taiwan ilikuwa ni nchi ya kidiktekta mpaka miaka ya 90 ndio demokrasia ilianza, yaani umri WA demokrasia WA Taiwan na Tanzania haupishani sana.
 
Unamaanisha maendeleo makubwa ndani ya Demokrasia ni yataka moyo siyo?
 
Ni pamoja na kukuta jamaa linavunja pale BoT linaiba matrioni ya fedha, haupaswi kulipeleka jera moja kwa moja, ila hadi lishitakuwe miaka na miaka likizitumia hizo fedha kuhonga wanasheria njaa na mahakimu na wananchi wakiendelea kukosa huduma mhimu

huo ni mfano mojawapo wa Demokrasia, najaribu tu mkuu
Kwa hio china hakuna mahakama?
 
Kwa hio china hakuna mahakama?
Zipo za walevi, wazinzi na wagomvi, ila siyo wezi, wahujumu uchumi, wala rushwa, wauza ngada, wavunja sheria, wandamanishaji n. k, ukibisha waulize msoga watakupa utamu wa China
 
Ingependeza kama ungeanza kwanza kueleza, China kipindi cha Democracy, ilikuwa lini na Uchumi ulikuwaje. Na ukalinganisha na kipindi hiki.
Halafu ndio ukauliza swali lako.

JF, Home of Great Thinkers.
 
Zipo za walevi, wazinzi na wagomvi, ila siyo wezi, wahujumu uchumi, wala rushwa, wauza ngada, wavunja sheria, wandamanishaji n. k, ukibisha waulize msoga watakupa utamu wa China
Umeshaishi China au Kufika China? unaweza kutupa mfano wa wachina 2, walihujumu uchumi,wala rushwa,wauza ngada,wandamanishaji nk, ambao walihukumiwa nje ya mahakama
 
Back
Top Bottom