Sasa, hao jamaa mbona kimaendeleo wako mbali sana kinyume kabisa na wengi wanavyoamini kwamba, Demokrasia ndiyo huleta maendeleo?
Ni chaguo la nchi mfumo gani wanautaka kuna nchi tajiri zina demokrasia na nchi maaikini dikteta. North Korea wana dikteta na ni masikini . Mfumo wa kidemokrasia nchi yetu ndiyo imeona unatufaa na kama tumeamua hili tufuate misingi yake na sio kujichanganya. Kama hatutaki demokrasia basi tubadilishe katiba na kufuata misingi ya hiyo system nyingine lakini hatuwezi kuwa na katiba ya kidemokrasia na utekelezaji ukawa udikteta hapo ndipo unapata tabu