Nikuambie kitu kimoja Tu ambacho ni muhimu.
Madhehebu hufasiri biblia wanavyotaka wao, biblia imekataza na unatakiwa ufahamu kwamba Neno la Mungu ni Neno la kinabii.
Sasa biblia imepiga marufuku kufasiri kama mtu anavyotaka
2 Petro 1:20-21
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Hivyo Neno la Mungu harifasiliwi kama mtu anavyota Bali Tu lazima uongozwe na Roho mtakatifu. Na Roho mtakatifu hamuongozi mtu ambaye hafuati neno lake,
Mfano Leo hii huwezi kuniambia hasa hawa wachungaji wa kimadhehebu wana Roho mtakatifu wakati huo wameruhusu haki Sawa kanisani
Twende kwa andiko maana daima nitatetea Neno la Mungu naomba Mungu anisaidie kwa hilo.
1 Wakorintho 14:34
Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
Haina haja ya kufasiri ni kwamba mwanamke ni marufuku kuhubiri kanisani.
Sasa je unaweza kuniambia huyu anaongozwa na Roho mtakatifu wakati ameshindwa kulifuata neno la Roho mtakatifu?
NAludia tena ndugu nakupenda mno kutoka moyoni, usijiunge na kanisa toka kwenye hiyo mifumo uludi kwenye Neno, ulitetee Neno,uliishi Neno ili uwe salama ndugu yangu[emoji120] na lazima upate ubatizo Harisi hiyo ni kweli.
ukiacha ama kuongeza neno kwenye biblia. Maana yake huifuati bible