Kwanini dhehebu la SDA huwa wanalishambiulia zaidi Kanisa Katoliki na siyo madhehebu mengine?

Utakapojua siku ya Saba ya juma ipi hautabishana sana.maandiko yanasema ht baada ya uumbaji Mungu alipumzika yaani siku ya Saba (JUMAMOSI),hata siku ya kwanza ya juma (JUMAPILI) Yesu alifufuka yaani JUMAPILI.
Siku ya saba alipumzika. Je Siku ya nane akaendelea na kazi gani?
 
Kumbe Moravian ina umri mkubwa kuizidi Lutheran!
 
Na jipya likishaanza kazi, kuukuu hukaa pembezoni.

Wakristo wanaishi katika Agano Jipya, Agano lililo bora zaidi ambalo Mdhamini wake ni Yesu Kristo.
 
Yule mwana mpotevu alieenda kuchunga nguruwe, hao nguruwe walikuwa wanafugwa kwaajili ya nini?
Swali zuri Sana😂😂😂,ndo maana mimi sinaga dini zenu hizo, good question to a wrong person....mtajiju na mavitabu yenu😂
 
Naona umekazana kutoa hoja hiyo ya kukataza wanawake kuhubiri kanisani.Sasa hebu soma hii kisha uniambie hapa wanaambiwa wakristo gani."Bali kila mwanamke asalipp,au ANAPOHUTUBU bila kufunika kichwa,yuaaibisha kichwa chale;kwa maana ni sawa na yule aliyenyolewa.(1 wkorintho 11:5)".
*Sasa hapo ni yule yule Paulo akiwaambia makanisa.Hebu nipe elimu kidogo hapo.
 
Kabla Musa hajapanda mlimani Sinai kuandikiwa amri na MUNGU,sabato ilikuwa inatunzwa.Ukisoma (kutoka 16:1,),utaona walifika katika bara ya Sinai tarehe 15 ya mwezi wa 2 tangu watoke misri.Na aya ya 23 wanaambiwa waendelee na taratibu ya kuitunza sabato.Ukisoma (Kutoka 19:1-3) utaona waisrael walifika katika mlima Sinai mnamo mwezi wa tatu baada ya kutoka misri,Ndipo Musa akapanda mlima Sinai kuandikiwa amri na MUNGU.Hii ni kuonesha amri za MUNGU ikiwemo amri ya nne ya kutunza sabato zilikuwa zikitunzwa hata kabla ya waisraeli kuwepo duniani.Kipindi hiko haizikuwa zimeandikwa,ila walizisikia zikitamkwa na MUNGU.SOMA MWANZO 26:5 inasema:"Kwa sababu Ibrahim alisikia sauti yangu akayahifadhi maagizo yangu,na AMRI ZANGU,NA HUKUMU ZANGU NA SHERIA ZANGU."Kwo hakuna sabato ya wayahudi bwa shee.Nikikuambia utoe aya inayosema sabato ni ya wayahudi hutatoa hadi Yesu anarudi.Sabato ni ya BWANA MUNGU(Kutoka 20:10).Ile ile ya uumbaji.
 
Nashukuru Kwa kuungana na Mimi kuwa Yesu hakuwahi kuwa na sheria wala hakuleta SHERIA.

Unaweza nitajia hao watunzi hata mmoja ambaye anaziita hizo sheria za Kristo?
Kisha unitajie na hizo sheria ambazo zinaitwa za Kristo.
Utashitakiwa Mtibeli.Unatoaje nondo namna hii?Sasa swali kama hili kwa nini umwambie atoe kwenye Biblia?Ungemwambia atoe kwenye vitabu vya historia ya watakatifu wa kikatoliki bwa shee
 
Mkuu biblia haijawahi kujipinga kwenye hicho kifungu twende sawa sasa. Hapo fasiri ya Kiswahili imekosea kidogo hutaweza kunielewa 1corinthians 11:5 but any woman who prays or prophesies with her head unveiled........ Hapo unaona prophesies ama kutoa unabii na tunajua kuna manabii wa kike kama Miriam,Anna na wengine. Lakini si kufundisha kanisani biblia inakataza Jambo hilo mwanamke kufundisha pia inakataza kua na cheo kanisani, hapo Paulo anaongea juu ya mwanamke kusali ama kutoa unabii. Shikilia hilo. Kaka kamwe Paulo hawezi akasema Jambo hili hapa na Jambo jingine pinganishi kule haiwezekani. Bible inasema ndio yenu iwe ndio na sio iwe sio hilo NI Neno la Mungu. Naomba namba yako mkuu kuna mengi ya kuzungumza
 
Nimekaa na kutafakari sana Kwa nini wasabatho wanalipiga vita sana kanisa katoliki na hiyo vita siyo kwa makanisa mengine?

Wajuzi mnijuze!

View attachment 2757316
Kwa kuwa lina wafuasi 1.2 Bilion duniani kote na ndiyo Kanisa Takatifu la Mitume lililoanzishwa na Yesu Kristo mwenyewe (Mathayo 16:1) "Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda"

Achana na vikundi vya ki-itikadi (cult) kama SDA vilivyoanzishwa na mwanamke mtabiri nyota mwaka 1844.

Watu walitaka wasafiri kwenda Ufaransa kuhubiri injili bila kuwa na passport wala tiketi, hao ndiyo washindane na RC?
 

Yesu hakuoa msio tambua hili ndio mtabaki kuleta mihemko,RC iko strong kwa sababu hii ya maaskofu wake kuwa watawa,makanisa mengi ambayo maaskofu wameoa na familia taaaisi zao zimejaa migogoro ya kila aina kwasababu mwanaume aliyeoa ni mwanaume dhaifu hawezi simamia taaisis vyema kwa sababu lazima ataweka mbele maslahi ya familia yake.

Wakatoliki sio wajinga wanajitambua na wanajua nini wanafanya,bila ukatoliki ukristo usingekuwepo duniani.
 

Unajikanyaga sana,hujui kila mtumishi kabeba maono makubwa kwa kazi ya Mungu au wewe unaweka mpaka katika utumishi?
 

Hongera kwa kuliacha kanisa na kufuata illuisions,uzuri ni kwamba kanisa katoliki haliyumbishwi lina misingi imara ya kujisimamia milele zote.
 
sio wasabatho wanawapinga wakatoliki hata waislamu hawawapendi wakatoliki tena afadhali ya sabatho

Waislamu wanaliogopa kanisa katoliki kama ukoma mana walileta ujinga ujinga crusade war ili wanyoosha,hadi leo papa anaingia msikitini na viatu,thubutu shehe au muumini wa kawaida kuingia msikinitni na viatu kama hawajakupopoa[emoji28]
 
Usijibariki, twende kwenye neno usimfananishe Yesu na askofu ama papa, huyo papa mnayedai ni petro alioa, kila kitu nenda Neno la Mungu.

Unaposema askofu akioa hahudumii majukumu yake ipasavyo, Una maana kwamba Roho mtakatifu alikosea kusema "askofu imempasa awe na mke mmoja" si ndio maana yako.

ndugu yangu tetea Neno la Mungu na sio kuleta mbambamba hapa nimekuwekea kifungu ambapo Roho mtakatifu ndani ya Paulo anasema askofu imempasa kuoa
 
Naomba niwaulize wa sababto ambao mnasema Yesu hakutengua torati ya musa bali alikuja kuikamilisha,je ukiondoa suala la amri 10 za Mungu,ni vitu gani vingine mliovichukua agano la kale na vitu gani mlioviacha agano la kale na kwanini?
 
Hongera kwa kuliacha kanisa na kufuata illuisions,uzuri ni kwamba kanisa katoliki haliyumbishwi lina misingi imara ya kujisimamia milele zote.
Lina misingi imara ipi ndugu, misingi imara ya kanisa ni Neno la Mungu, je unakumbuka mnamo 1500s Martin Luther aliorodhesha makosa 95 ya kuyafanyia masahihisho kwa sababu yamepingana na Neno la Mungu, unalijua hilo. Na je kama wameliacha Neno linakuaje na misingi imara ama je ni Bora liwe na misingi imara ya kibinadamu au Neno la Mungu.

Kanisa katoliki lilikua na misingi imara kabla ya mwaka 325 baada ya mwaka huo Tu na kuanza vikao vya kujadili Neno la Mungu liwe wanavyotaka lilianguka. Sasa biblia inasema kanisa likianguka hakuna tena neema ya kusimama

Waebrania 6:5-6
na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
 
Utashitakiwa Mtibeli.Unatoaje nondo namna hii?Sasa swali kama hili kwa nini umwambie atoe kwenye Biblia?Ungemwambia atoe kwenye vitabu vya historia ya watakatifu wa kikatoliki bwa shee

Unajua kuna Watu wanashindwa kutofautisha mambo
 

Usijichanganye Mtume Paulo alikua natoa maoni yake katika masuala mengi sana,hili la kuoa ama kutokuoa ni ushauri tu,ila kama unataka utende vyema kazi ya kristo ni vyema usioe kabisa ila kama utawaka tamaa basi ao ila ndoa ya mke mmoja tu.

Kwakuliona hilo kanisa la RC lenye mfungamano na kristo na mitume wake likaona ni vyema maaskofu wake wasioe ili wawe imara katika kutenda utume wa injili kama kristo mwenyewe.

Narudia tena RC ndio taaisis ya kidini imara kuliko zote ulimwenguni moja ya sababu kuu ni sera ya utawa,siku ukiona kanisa limeondoa sera hii ndio anguko la kanisa hili na kwa hili sahau kama itakuja tokea mana RC nia kanisa linalojitambua.
 
Mkuu Mimi nataka andiko sitaki maneno yako tupu, kumbuka Neno la Mungu linasema Neno la Mungu liwe kweli na mtu Tu iwe uongo nayo Neno la Mungu ni kweli, njoo na andiko.

Kumbuka Paulo baada ya kuandika hayo amesema hivi katika
1 Timotheo 3:15
Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.

kwamba hivyo ndivyo iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu yaani kanisa, unaona hili ni Neno la Mungu sio ushauri ndio maana amesema askofu imempasa na pia anasema hivyo ndivyo iwapasavyo watu kuenenda shikilia iwapasavyo maana ni wajibu ni lazima na sio wakipenda wafanyaj hivyo hapana. Hivyo ndivyo iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu. Shikilia hilo haliwezi kubadilika hata kidogo na hii ni injili kumbuka.

NAOMBA andiko maana kwa andiko utakua salama Lakini kwa maneno kutoka katika kanuni mlizojitungia kutoka katika mitaguso hiyo itakupeleka kuzimu. Maana imeandikwa mnaliharifu Neno la Mungu kwa mapokeo ya wanadamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…