😁😁😁 mbona ugomvi wa ngumi umeleta panga. Calm down binti kiziwi
By the way, 2005 - 2015 kilikuwa ni kipindi ambacho nilikuwa nafuatilia sana showbiz ya Africa nzima kwa hiyo Zari nilianza kumjua kabla ya kudate na mondy, enzi hizo inasemekana ndio richest socialite in East Africa kabla ya Akothee kuja juu
Hadi Zari anafika bongo, alikuwa anakuja kwa muzamili, kitu kama hicho na alikuwa close sana na sintah,
Alipoingia kwenye mahusiano na mondy, alikuwa anambully sana Wema kwa sababu tu ya "kutokuzaa" na kucomment kwenye kila move yake kwa kuonesha she is better than her, kitu ambacho wema alikilalamikia sana. mwanamke gani mwenye decency anaweza kufanya hivyo
She tried the same thing kwa Sharon O na Fabiola, uliona reactions za waganda
Alijaribu kwa Huddah, uliona reactions za wakenya
Alijaribu kwa huyu lady wa Ghana kwenye ile show ya juzi kati hapo, uliona reactions za waghana
Ushawahi ona Waganda wakihangaika nae hata kwenye mass media, social media au hata kwa mastar wenzie wa Uganda
Ila Tanzania akifanya chochote na lolote lile, she gets away with it na anapata support na endorsements juu.. Hiyo ni love au obsession
Huh! I didn’t know if it is this serious!!!! Again, uko biased 90% Yaani uko serious kum-paint everyone as innocent isipokuwa Zari. Why? Is it personal????? Kwamba hao watu wote Zari aliamua tu kuanza kuwaatack wao wakiwa kimya wametulia, I hope this is a joke.
Bahati nzuri mimi na wewe sote hatujachelewa kuja mjini, ni hivi Diamond kuanza kudate na Zari hakuna kati yao aliyeweka wazi wenyewe waliita “Project “ Zari hakuanza “kujishaua” kama unavyojaribu kutuaminisha hapa, alikuwa normal, anadate zake mtandale bila hili wala lile. Kesi zilianza kwa timu Wema kuanza kumuattack Zari, (kumbuka timu kajala ilikuwepo) ndiyo iliyokuja kumpa Backup Zari ikatengenezwa Strong hive “Timu Zari” na watandale wakiwemo humo nadhani lengo lao lilikuwa kumrusha roho Wema, Ndipo mwanzo wa maugomvi ya haya matimu.
It was funny and games until Ilivyosemekana Zari ana mimba, kwanza kuna watu wakakataa kuwa hana mimba at first, kwa kile kilichoitwa kuwa kaka yetu Simba la masimba 😀 hana uwezo wa kushikisha mwanamke ujauzito, mimba haijifichi miezi ikaenda stori ikabadilika kuwa mimba si ya Diamond bali ya Ivan, siku hazigandi mtoto akazaliwa ikasemekana mtoto wa Ivan, zikajiunga timu ya anti Diamond wa Bongo, na anti Zari wa Uganda kudai mtoto si wa Dai ni wa Ivan, You see?
Siku zinaenda fasta, picha ya mtoto ikapostiwa ni “our very own Wema” ikabambwa comment yake mahali akiwa amecomment “Mtoto ni mbaya” na pia tunaomba DNA !!!!! We ni mwanaume sitakuuliza ungekuwa mama Tifa ungereact vipi. I hope unaona sasa Why Zari started to slap back.
Ikaenda mtoto wa pili, huyu ndio kabisa wakasema ni wa Ivan, wakati kwa ground wadada wa bongo “hao wa insta” wakaanza kumuona Diamond mcharo kutaka kumzalia (usitake nikawataja majina), hao wote akina Huddah unadhani ugomvi wao na Zari ulitokea wapi, ikiwa mwanzo walijaribu kumfriend zone Zari ili wapate access kwa mtandale, which waliipata wakalambwa Zari kama mwanamke aliyekuwa kwa mahusiano na Dai akigundua kuna mtu kanizunguka why asifight? Mbona ni kitu kinaeleweka tu vizuri. Bora ye anatukana/chamba binafsi ningemfuata kumdunda kabisa hehe 😂
Halafu comeon, Fantana? That was reality show, lazima kuwepo drama na mtu wa kuinstigate drama lazima apatikane, usiniambia hujui how these things work!
Kuhusu waganda kuhangaika nae au kutokuhangaika nae: kwanza lazima uelewe kati ya taifa lina shobo na ujinga Tz inaongoza Africa nzima, tuna muda wa kuwaintertain hawa insta celebs kwa viwango vya juu sana kiasi kwamba kila mtu akitaka umaarufu bongo inakuwa target kwake, its no different with Zari, halafu unasemaje waganda wana muignore wakati we umemjua before hajaja bongo? Nani alimpa hiyo fame kama sio hao waganda wenyewe? Ni vile tu nchi za wenzetu ziko tofauti, people are real busy, ukisikia msanii yuko mall hakuna mwenye ataenda kukusanyika kushangaa, hakuna mtu atamfata msanii AirPort kumpokea, again its no different with Zari.
Meanwhile in Bongoland, hata bodaboda wakigongana watu watajaa kushangaa, sijui nani yuko AirPort watu wataenda kumpokea, sijui msanii gani kaonekana mall watu wataacha manunuzi yao wakae kushangaa na kuomba picha, hakuna utofauti uliofanyika kwa Zari. There’s crowd for everyone in Bongoland.
Excuse my gazeti, nilikua najaribu kuweka narration kwa namna ninavyoielewa, by the way it is weekend 🥂