Naona mnachanganya historia ya mziki wa bongo fleva na waimbaji wa mwanzoni wa bongo, ni kweli Dully Sykes alikuja kubadilisha mahadhi ya mziki wa bongo baada ya waliotangulia kua walifocus sana na umarekani mwingi,
Nakumbuka neno bongo fleva linaanza kuna wakongwe walikua wanakataa mziki wao kuitwa wa bongo fleva kwa sababu bongo fleva ulionekana ni mziki wa mabishoo, wabana pua n.k
Dully ndio maana akawa anajiita bishoo, brazameni, Mr. Misifa n.k
Humo utakuta nyimbo kama,
Hi,
Handsome,
Ladies free,
Ili mradi kuwakera tu wapinzani wake ndio baadae wakamuelewa na jina la bongo fleva likaota mizizi,
Tumpe maua yake Legendary brazameni Dully Sykes mwenye Zali lake limeshikilia namba 3 mjini Youtube na ilikaa namba 1 kwa wiki 2 na nusu.