Kwanini Dully Sykes anasema yeye ndiye Mwanzilishi wa Bongofleva?

Kwanini Dully Sykes anasema yeye ndiye Mwanzilishi wa Bongofleva?

Julietha
Nakupenda kwa dhati
Lakini maisha yangu sijuii ..(nimesahau mistari)
Naapia kwa Mola haki ya Mungu sikuachi!

Ebhanaa eeh! Kitambo Mzee!
Hii Julietha ndo aliyotoka nayo Dully baadae zikafuata nyambizi na nyingine nyiiiiingi
 
Nimekuwa nikimsikia mara kwa mara akijigamba hivyo kwenye media, na sielewi anamaanisha nini maana maandiko mbalimbali ya historia ya bongofleva hayatambui hilo. Kama anamaanisha 'kuimba' mbona kina Unique Sisters, Mr Paul, Jide, n.k walikuwepo kabla yake?!
Ni kweli zamani walikuwa wanafoka foka yaani wanaimba kihuni huni..
Sasa yeye akaanza kuimba kwa kuregeza sauti na alitoa hits watu wakawa wanapenda sana julieta, salome then TID nae akaja na zeze hapo ndio bongo fleva ilipoanza kunoga.
nakumbuka nilikuwa darsa la 3 au 4 hizo nyimbo zinatoka basi tunaimba sana sana.
 
Nadhani alitoboa na " Salome juu ya kaburi lako naliaa......." Mwaka 2002 kama sikosei. Kwa umri wangu najua wasanii wote wa Bongoflava miaka waliotoboa na nyimbo walizohit nazo...
Julietha ilitangulia kabla ya salome na ilihit kuliko salome
 
Naona mnachanganya historia ya mziki wa bongo fleva na waimbaji wa mwanzoni wa bongo, ni kweli Dully Sykes alikuja kubadilisha mahadhi ya mziki wa bongo baada ya waliotangulia kua walifocus sana na umarekani mwingi,
Nakumbuka neno bongo fleva linaanza kuna wakongwe walikua wanakataa mziki wao kuitwa wa bongo fleva kwa sababu bongo fleva ulionekana ni mziki wa mabishoo, wabana pua n.k
Dully ndio maana akawa anajiita bishoo, brazameni, Mr. Misifa n.k
Humo utakuta nyimbo kama,
Hi,
Handsome,
Ladies free,
Ili mradi kuwakera tu wapinzani wake ndio baadae wakamuelewa na jina la bongo fleva likaota mizizi,

Tumpe maua yake Legendary brazameni Dully Sykes mwenye Zali lake limeshikilia namba 3 mjini Youtube na ilikaa namba 1 kwa wiki 2 na nusu.
 
Tatizo humu mitandaoni wengi ni watoto wa juzi. Ukitaja miaka ya 1998 wengi wao hawajazaliwa
 
Nadhani alitoboa na " Salome juu ya kaburi lako naliaa......." Mwaka 2002 kama sikosei. Kwa umri wangu najua wasanii wote wa Bongoflava miaka waliotoboa na nyimbo walizohit nazo...
Unazingua wewe dully katoka na Salome..
Alafu unasema unasema unaijua bongo fleva
2002 dully supa star mkubwa t kashatoboa Miaka minne kama so mitano nyuma
 
Nyimbo ya juzi hiyo!

Hapo tayari alishatoa ladies free!

Alishatoa nyimbo ya Hi!

Aliahatoa ile nyimbo aliyotoa na mtoto wa kiarabu.

Alishatoa Salome! n.k

Alishatoa nyambizi!

Alishaimba na wale wanawake wawili sijui raha ya tunda.
Ila mwamba alikuwa akitoa hit songs sana [emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom