Kwanini flyover Ubungo haimalizi tatizo la foleni?

Tumetumia gharama kubwa bure pale ubungo, toka walivyoondoa mataa wakaweka round-about foleni ilisha isha amini usiamini. Ni km pale Moro foleni historia.
 
Leo kuna mwenzio kaja anaisifia humu mpaka anasema Lissu aende akashuhudie maendeleo ya flyover ya Ubungo imepunguza foleni, Kulikoni tena..?
 
tusiwatupie lawama hawa planners wa miundombinu yetu mimi naamini ni wasomi na pia sio peke yao wanaofanya planning ya hii miradi mikubwa ya nchi, kuna pia mawazo ya wataalamu wengine wa nje na wanaelewa kabisa kinachotakiwa kufanyika lakini siasa na ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya haya tunayoyaona leo
 
Kwa mji mkubwa kama Dar foleni haiwezi kukosekana,pia changamoto huwa zinatatuliwa taratibu na kwa mipango.
Mbezi mwisho na Shekilango pakitatuliwa pia tatizo litaamia pengine napo patarekebishwa.
hivyohivyo mdogomdogo mpaka tutafika.
Mbezi mwisho na shekilango pakitatuliwa watarudi humu kulalamika kua foleni imehamishiwa sehemu nyingine...Kifupi binadamu hajaumbiwa kuridhika...Always ni mtu wa lawama.
 
Mbezi mwisho na shekilango pakitatuliwa watarudi humu kulalamika kua foleni imehamishiwa sehemu nyingine...Kifupi binadamu hajaumbiwa kuridhika...Always ni mtu wa lawama.

ni bora mtu alalamike mtu mwenye maumivu ya kweli lakini sio hawa wahuni wanaotafuta karata za siasa.
 
ni bora mtu alalamike mtu mwenye maumivu ya kweli lakini sio hawa wahuni wanaotafuta karata za siasa.
Wazungu wanasema "The loudest person in a room is weak one"....hawa wanaoshupaza shingo humu kupinga pinga siku ukifanyikiwa kukutana nao wakakupeleka wanapoishi utabaki kujiuliza huyu ndo yule Mjuaji kule JF au? wanaifanya flyover issue ya kisiasa while makao makuu ya chama ni tatzo...waanze kutuonesha mfano wa Ujenzi wa HQ yao kabla ya kuanza kukosoa walivyojenga wenzao...
 
Ok kumbe mheshimiwa leo kakosea kusema tatizo la foleni limeisha
Argument yangu imebase kwenye Objective truth,Kama mada yako ipo kwenye context ya kisiasa au unatumia kauli za wana siasa ku bias akili yako nje ya ukweli,hilo ni tatizo jengine
 
Yaan hamna cha fly over wala nn sasa kasheshe nyingine inahamia bagamoyo road, ninakuambia kwasasa kutoka tegeta mpka mwege tu unatumia saa moja na nusu ngoja daraja lifungulie uone kitakachotokea mwenge pale, siasa za tatizo ni sera mbovu watu wanafikiria pafupi kwa kuangalia mpinzan wake, matokeo ndo hayo.
 
Tutajenga flover nyingine pale pamoja na Morocco, Magomeni usalama,uhasibu kurasini,karume/ilala pamoja na mataa ya chan'ombe kulekea veta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…