maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,311
- 15,640
Naipongeza Serikali yetu kwa juhudi kubwa za kutuletea maendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu yetu. Leo daraja la juu pia limefunguliwa kwa magari yanayotokea mwenge kuelekea Riverside lakini kinachonishangaza ni kwanini foleni bado ni kubwa sana kwa magari yanayotokea Kimara?
Huenda hawajamaliza upanuzi wa barabara ila ni wazi kwa ramani hii wameamua tu kupunguza tatizo la foleni badala ya kulimaliza pamoja na kutumia billions za kutosha.
Nachojiuliza walishindwa vp kuongezea bilioni zingine wakajenga kitu cha kuishi miaka yote kitakachomaliza tatizo? Na hii hali inajirudia pale mbezi mwisho licha ya mapesa mengi yanayotumika ila hakuna dalili za kumaliza tatizo la foleni sana sana ni kama foleni ya Ubungo wanaihamishia Mbezi Mwisho.
Tuna watu wanaofikiri sawasawa? Hawatembei nchi nyingine? Wakitembea huko hawajifunzi wenzetu wanafanyaje?