Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni wivu tu.Nani amekwambia mizigo inayosafirishwa na mabasi shekilango inatokea sinza? Asilimia 90 ni kariakoo..? Kwasababu ya ukaribu wa shekilango na sinza usidhani inatokea sinza...watu wengi wa kariakoo wanaleta hapo shekilango kwasababu ndio Kuna mabasi ya kwenda almost mikoa yote.
Watu waliolezea habari za sinza usidhani wametunga , wengi tumeishi Sinza miaka nenda Rudi na wengine tumekuwa na biashara....pita Leo kuanzia shekilango Hadi bamaga note maduka yote next year utakuta mengi mapya...watu wengi wakiona hizo frem na biashara wanajua biashara ipo at the end wanafungua after a year wanafunga , wachache wapo wanaokamaa ku try mwaka mwingine ,wapo pia wanaokuja kuzugia na kupoteza muda ..inshort sinza hakuna biashara Kwa mfanyabiashara serious ...wanaofanya biashara na kumake money ni almost 10% ya biashara zote...wengine waliosali ni kujaribu biashara ,kuzugia, Dili chafu etc ..
Ukishawahi kujiuliza watu wafanyao biashara haramu huwa wanajificha kwenye biashara gani?
Hii ndio Genuine. Badala ya mwanamke kushinda nyumbani unamweka busy kwenye biashara yake unampunguzia muda wa kuzurura na kukucheat na hata kukufuatilia pia since yuko kwenye biashara zake na akili yake inakuwa na jambo la kuiweka attention.
Nimecheka sana aisee. Huwa nafikia Sinza Mugabe kila nikija Dar kibiashara kuna mshikaji huwa nakaa dukani kwake ukweli unaweza kukaa pale hadi jioni bila kuona mteja ila kila siku anapost mzigo mpyaMimi hii naweza kubaliana na wewe japo sikuwa na mawazo hayo kabla, Kuna sehemu nimekaa tokea asubuhi mpaka saa 6 wameingia watu wawili tu.
Hao Wana mambo Yao nadhani wameweka pale kuzuga tu.Sister angu alijichanganya akachukua fremu hapo sinza inatizama barabarani 350k. Akaikarabati vizuri aluminum, Ac shelf za nguo za kisasa.
Aseee miezi 6 tu akafunga biashara, Yaani Hakuna wateja kabisa inaweza pita wiki hujauza nguo hata moja.
Biashara ni wateja sinza , kinondoni ukienda kuanzisha biashara sijui nguo una 99.9% ya kuchoma mtaji.
Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Ni wivu tu.
Yapo maduka zaidi ya 50 naweza kukutajia ni ya miaka nenda rudi na yapo hiyo njia ya Bamaga - Shekilango. Utafiti wako kwamba maduka yote huwa mapya kila mwaka ni uongo wa mchana kweupe.
Kusema tu mizigo mingi ya kkoo inakuja shekilango ndio nikakuona hola! Mabasi ya mikoa karibu yote yana ofisi za mizigo kkoo achilia mbali ya nje ya nchi kama vile Mombasa nk. Pia jangwani pale na baadhi ya mitaa kkoo kuna tandam zinafunga mizigo ya mikoani. Wafanyabishara wengi wanaonunua mizigo kkoo wa mikoani wanafunga mizigo mikubwa hawaipakii kwenye mabasi wengi wanapakia Fuso.
Sinza kuna biashara kwa sababu kuna soko. Wateja wengi ni wanafunzi wa vyuo na wengi wanapendelea kununua online. Hilo eneo la sinza limezungukwa na vyuo kibao kuanzia udsm, ardhi, ustawi, maji, law school, takwimu, tudarco, tax. Wengi wa hawa wanafunzi wanakaa Sinza na ndio wateja wazuri kwenye haya maduka. Na sio biashara za maduka ya nguo na viatu tu bali biashara zote kuanzia vyakula, sehemu za starehe kama mabar nk. Sinza kunachangamka kila baada ya siku. Kodi ni kubwa sio tu kwenye maduka bali mpaka nyumba za kupanga maana demand inakuwa kubwa kila siku.
Hoja ninayoipinga ni kwamba wenye maduka wengi Sinza ni a. Wauza Unga b. Wanatakatisha fedha kupitia maduka yao c. Wanajiuza hivyo maduka yao wanazugia tu.
Hoja hii naipinga maana imekaa kinaa na wivu tu na haina ukweli wowote
A. Biashara ya unga sio biashara rahisi kusema kila mtu anaweza kuifanya. Kuanzia shekilango mpk bamaga mpk mwenge kuna mamia kama sio maelf ya maduka. Huwezi kusema hawa wote ni wauza unga. No way! Ina maana DEA wamelala kiasi wauza unga wanajikusanya sehemu moja namna hiyo wanauza mihadarati kama peremende!? Na unga hauuzwi kama bidhaa za kawaida. Kila maeneo yana wenyewe na taratibu zao huko kwenye ulimwengu wao wa madawa. Wewe ndenda kauze mzigo eneo sio 'territory' yako ndio utajua. Sisemi hakuna wanaofanya biashara hizo hapo Sinza wapo ila ni kwa % ndogo sana maybe less than 10. Huwezi kusema wafanyabiashara wote maelf ni drug dealers.
"Never sell no crack where you rest at, I don't care if they want an ounce tell em to bounce"
Unauzaje unga unapokaa!? Mahali ilipo biashara yako!?
B. Money laundering.
Pia hili sio rahisi. Na ili uhitajike utakatishaji wa fedha ni lzm iwe fedha hiyo ni chafu/imepatikana kiharamu. Na unatakatishaje fedha kupitia biashara ya nguo/viatu!? Very hard!! Wafanya biashara wengi sio tu sinza bali kote nchini hawawezi tu kuweka record za biashara zao vzr ndio wawe watakatishaji wa hela!?
- Mtu mwenye club anaweza kupata waingiaji 500 kwenye club yake usiku yeye akarekodi wameingia 2000. Hakuna atakayehesabu kuhakikisha hawa ni watu 500 na sio 2000. Kama kiingilio ni 10000 tayari anaweza kusafisha milioni 15 kutoka kwenye pesa zake chafu akazipeleka bank kama pesa safi (kama pato halali la club). Akiwa anafanya hivyo mara 2 kwa wiki ina maana ndani ya mwezi anaweza kutakatisha 120m. Na hii ni rahisi kwa biashara zote za huduma (sio bidhaa za kushikika) kama vile saloni/barbershop, kumbi za starehe, carwash etc.
- Ukija kwenye bidhaa kama nguo/viatu ugumu unakuwa kwenye kubalansi figures. Utawezaje kusafisha milioni 120 kupitia duka la nguo la sinza!? How!? Sinza hapo ukiacha mabigi kama VunjaBei maduka mengine turnover zake ni za kawaida sana around piece 5 mpk 10 kwa siku. Yaani hata kontena moja 40ft yenye piece 30k za viatu huwezi kuiuza ikaisha kwa mwaka. Unawezaje kutumia slow business hivyo kusafisha mamilioni ya pesa za haramu yanayokuja kila siku!? Labda kama unataka kusafisha as kusafisha lkn kama unataka kuwa smart abt it fashion shops in Sinza isn't the way to do it
C. Kujiuza/umalaya
Hii biashara ni overrated. Hailipi kihivyo. Biashara mtu anafanya wiki 2 kwa mwezi na mapumziko ya wiki 2. Na kwenye hizo wiki 2 sio kila siku atapata danga la maana. Wafanyabiashara hii wapo wengi sana na wengi bado ni waganga njaa. Mpk uwe na uwezo wa kupanga fremu sinza na kulipa kodi ya mwaka, bills kama umeme, ulinzi, uwe na file TRA unalipa kodi na efd unayo, leseni, gharama za kuendesha biashara kila siku km nauli, chakula nk. Bado hela ya kuagiza mzigo au kwenda kuufuata nauli ggarama za kuishi nk. Hiyo kitu itakuwa inapiga mluzi ukitembea.
Vijana wa sinza wanajitahidi na mambo yanaenda. Ujanja mwingi wanafosi huku na kule biashara zinapushiwa mitandaoni na kila mahali zinasonga ijapokuwa mdomdo. Wapo wanaofeli wengine wanaingia kujaribu wanafanikiwa au nao wanafeli na siku zinaenda. Hakuna uchawi wala ndumba wala kujiuza wala madawa wala bangi wala nn. Tuache wivu watanzania.
Kwakweli jamaa kaweka maelezo meeengi ambayo sioni hoja ndani yake.Mdau umetumia nguvu nyingi sana kumpinga mtoa mada. Tuna nyumba ya urithi maeneo hayo na ina frame kali tu na bei ya frame moja ni laki tano. Naandika hapa kwa experience. Hayo yote yaliyosemwa hapo ni kweli tupu. Kila baada ya miezi Sita ni kawaida tu kupata mpangaji mpya, wapangaji wengi ni wadada warembo wenye masponsa ndio wanawafungulia,
Biashara kubwa ni nguo, mikoba, mawigi, makava ya simu, kifupi hakuna biashara siriaz ya kumtoa mtu. Hao uliosema wanafunzi ndio hawawezi kabisaa ku afford bei za kule. So no customers no business.
Kaige na wewe ufungue tuone utasavaive kwa muda gani.
Tulia weweWivu
Gambino family Mzee lazima kuwe na mabucha ya uongo na ukweli kuficha magendo zinaitwa petrol station kubarishia mzigo na kuvusha mzigo, hujaelewa hujaelewaSinza kudanga kwingi aisee kila baada ya frame 2 au 3 unakutana na duka la nguo, sijui wanamuuzia nani
Katika jamii yetu iliyojaa watu namna yako/yenu kutoboa ni ngumu sana. Watu wakiendelea kdg mnakimbilia kudai ni wadangaji/wauza Unga/matapeli nk. Wivu tu na husda. Hebu danga na wewe basi ufungue duka tukuone!!Kwakweli jamaa kaweka maelezo meeengi ambayo sioni hoja ndani yake.
Anasema kuishi sinza ni expensive, sinza kwanza. Tatizo watu wakipanga mtaa fulani huwa hawazunguki, sinza vyumba vya bei rahisi vipo na vya bei ya juu vilevile vipo inategemea wewe unataka sinza ipi.
Hao wanavyuo anaosema ni wateja wakubwa wengi ungaunga mwana tu na labda wa Udsm japo nao wengi wanaendaga mwenge na sio sinza.
Hata kupanga wanafunzi wa udsm wanapanga hukohuko karibu na chuo chao. Sinza kudanga kwingi aisee kila baada ya frame 2 au 3 unakutana na duka la nguo, sijui wanamuuzia nani
Hizo fremu zimejaa misukule na vibwengoo,
Niliiba jeans week iliyopita, humu ndani Unga haukai, usiku ukishtuka unaona vimbilikimo vimeshikana vinatembea, Kesho nairudisha nikainunue upya.
Ndevu, iPhone, Crocs
Kwani kusema kile ulichoona ni wivu na husda?? Aloandika kua wanadanga ni nani? Mbona una makasiriko kijana au na wewe una frem yako sinza hapo, unauza nini huko mtandaoni tukuungishe, si mnafanya biashara kidigitali maduka ni gelesha tu 😄😄Katika jamii yetu iliyojaa watu namna yako/yenu kutoboa ni ngumu sana. Watu wakiendelea kdg mnakimbilia kudai ni wadangaji/wauza Unga/matapeli nk. Wivu tu na husda. Hebu danga na wewe basi ufungue duka tukuone!!
Kama haya maelezo yako ndio hoja basi wewe hujui hata hoja ni nini achilia mbali kuweza kuitoa.