Ni wivu tu.
Yapo maduka zaidi ya 50 naweza kukutajia ni ya miaka nenda rudi na yapo hiyo njia ya Bamaga - Shekilango. Utafiti wako kwamba maduka yote huwa mapya kila mwaka ni uongo wa mchana kweupe.
Kusema tu mizigo mingi ya kkoo inakuja shekilango ndio nikakuona hola! Mabasi ya mikoa karibu yote yana ofisi za mizigo kkoo achilia mbali ya nje ya nchi kama vile Mombasa nk. Pia jangwani pale na baadhi ya mitaa kkoo kuna tandam zinafunga mizigo ya mikoani. Wafanyabishara wengi wanaonunua mizigo kkoo wa mikoani wanafunga mizigo mikubwa hawaipakii kwenye mabasi wengi wanapakia Fuso.
Sinza kuna biashara kwa sababu kuna soko. Wateja wengi ni wanafunzi wa vyuo na wengi wanapendelea kununua online. Hilo eneo la sinza limezungukwa na vyuo kibao kuanzia udsm, ardhi, ustawi, maji, law school, takwimu, tudarco, tax. Wengi wa hawa wanafunzi wanakaa Sinza na ndio wateja wazuri kwenye haya maduka. Na sio biashara za maduka ya nguo na viatu tu bali biashara zote kuanzia vyakula, sehemu za starehe kama mabar nk. Sinza kunachangamka kila baada ya siku. Kodi ni kubwa sio tu kwenye maduka bali mpaka nyumba za kupanga maana demand inakuwa kubwa kila siku.
Hoja ninayoipinga ni kwamba wenye maduka wengi Sinza ni a. Wauza Unga b. Wanatakatisha fedha kupitia maduka yao c. Wanajiuza hivyo maduka yao wanazugia tu.
Hoja hii naipinga maana imekaa kinaa na wivu tu na haina ukweli wowote
A. Biashara ya unga sio biashara rahisi kusema kila mtu anaweza kuifanya. Kuanzia shekilango mpk bamaga mpk mwenge kuna mamia kama sio maelf ya maduka. Huwezi kusema hawa wote ni wauza unga. No way! Ina maana DEA wamelala kiasi wauza unga wanajikusanya sehemu moja namna hiyo wanauza mihadarati kama peremende!? Na unga hauuzwi kama bidhaa za kawaida. Kila maeneo yana wenyewe na taratibu zao huko kwenye ulimwengu wao wa madawa. Wewe ndenda kauze mzigo eneo sio 'territory' yako ndio utajua. Sisemi hakuna wanaofanya biashara hizo hapo Sinza wapo ila ni kwa % ndogo sana maybe less than 10. Huwezi kusema wafanyabiashara wote maelf ni drug dealers.
"Never sell no crack where you rest at, I don't care if they want an ounce tell em to bounce"
Unauzaje unga unapokaa!? Mahali ilipo biashara yako!?
B. Money laundering.
Pia hili sio rahisi. Na ili uhitajike utakatishaji wa fedha ni lzm iwe fedha hiyo ni chafu/imepatikana kiharamu. Na unatakatishaje fedha kupitia biashara ya nguo/viatu!? Very hard!! Wafanya biashara wengi sio tu sinza bali kote nchini hawawezi tu kuweka record za biashara zao vzr ndio wawe watakatishaji wa hela!?
- Mtu mwenye club anaweza kupata waingiaji 500 kwenye club yake usiku yeye akarekodi wameingia 2000. Hakuna atakayehesabu kuhakikisha hawa ni watu 500 na sio 2000. Kama kiingilio ni 10000 tayari anaweza kusafisha milioni 15 kutoka kwenye pesa zake chafu akazipeleka bank kama pesa safi (kama pato halali la club). Akiwa anafanya hivyo mara 2 kwa wiki ina maana ndani ya mwezi anaweza kutakatisha 120m. Na hii ni rahisi kwa biashara zote za huduma (sio bidhaa za kushikika) kama vile saloni/barbershop, kumbi za starehe, carwash etc.
- Ukija kwenye bidhaa kama nguo/viatu ugumu unakuwa kwenye kubalansi figures. Utawezaje kusafisha milioni 120 kupitia duka la nguo la sinza!? How!? Sinza hapo ukiacha mabigi kama VunjaBei maduka mengine turnover zake ni za kawaida sana around piece 5 mpk 10 kwa siku. Yaani hata kontena moja 40ft yenye piece 30k za viatu huwezi kuiuza ikaisha kwa mwaka. Unawezaje kutumia slow business hivyo kusafisha mamilioni ya pesa za haramu yanayokuja kila siku!? Labda kama unataka kusafisha as kusafisha lkn kama unataka kuwa smart abt it fashion shops in Sinza isn't the way to do it
C. Kujiuza/umalaya
Hii biashara ni overrated. Hailipi kihivyo. Biashara mtu anafanya wiki 2 kwa mwezi na mapumziko ya wiki 2. Na kwenye hizo wiki 2 sio kila siku atapata danga la maana. Wafanyabiashara hii wapo wengi sana na wengi bado ni waganga njaa. Mpk uwe na uwezo wa kupanga fremu sinza na kulipa kodi ya mwaka, bills kama umeme, ulinzi, uwe na file TRA unalipa kodi na efd unayo, leseni, gharama za kuendesha biashara kila siku km nauli, chakula nk. Bado hela ya kuagiza mzigo au kwenda kuufuata nauli ggarama za kuishi nk. Hiyo kitu itakuwa inapiga mluzi ukitembea.
Vijana wa sinza wanajitahidi na mambo yanaenda. Ujanja mwingi wanafosi huku na kule biashara zinapushiwa mitandaoni na kila mahali zinasonga ijapokuwa mdomdo. Wapo wanaofeli wengine wanaingia kujaribu wanafanikiwa au nao wanafeli na siku zinaenda. Hakuna uchawi wala ndumba wala kujiuza wala madawa wala bangi wala nn. Tuache wivu watanzania.