FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
- Thread starter
- #101
Nafikiri hitimisho ni kuwa mataifa yote hayo yana madini mengi na yote ukiangalia wana dhahabu, almasi na uranium pamoja na copper
Wazungu waligawana mataifa yetu ili wanyonye rasilimali zetu ila kidogo waingereza wana heshimu kidogo utu kuliko wafaransa na wabelgiji
Wafaransa wao mbinu za kuchonganisha bado wanaendeleza mpaka sasa
Nimeangalia nchi zote hizo zimeshiba madini na ndio chanzo cha kuwachonganisha ili waibe kiulaini
Wanatengeneza waasi na kuwapa silaha huku wakijifanya urafiki na serikali
Lazima kuna sababu za msingi sana kwa Msumbiji kuomba msaada wa kijeshi Rwanda kukabili waasi badala ya Tanzania ambao wana undugu nao wa damu
Kuna wakati Tanzania ilijulikana kwa umahiri katika mapambano ya kivita, na jeshi letu JWTZ liliaminika sana katika uwanja wa mapambano. Hata waasi sehemu kama DRC walikuwa wakisema wazi, kwamba hawakuogopa kukabiliana na jeshi jingine lolote isipokuwa JWTZ ndio waliwaogopa sana. Tulijenga sifa...