Tatizo watu mnaangalia zaidi leo na hamjui historia kwani kila nchi imekuwa na matatizo katika kipindi fulani.
Kuna kipindi hiyo hali ilikuwa ikizikabili hata mataifa yaliyotawaliwa na Uingereza, Spain na hata Ureno vilevile.
Tuliona Sudan na hadi leo hii bado tunaona Sudan ni shida tupu, tuliona Uganda, Ghana, Nigeria, Sierra Leone, Gambia, Zimbabwe, vurugu za Kenya kila baada ya uchaguzi.
Hata hapa Tanzania hamna amani yoyote ila kuna ka utulivu tu lakini huko tuendako tusitegemee hali hii kuendelea kwa aina ya utawala huu tulio nao, safari bado ndefu sana.
Mataifa yaliyotawaliwa na Ureno kama Guinea Bissau, Msumbiji na Angola yamekuwa kwenye vurugu kwa muda mrefu sana.
Tukiangalia mataifa yaliyotawaliwa na Ubelgiji kama Congo, Rwanda na Burundi ni yale yale, hivyo kusema vurugu ni kwa mataifa yaliyotawaliwa na Ufaransa tu ni kutokujua wapi tumetoka na bado kuna mataifa mengine ambayo hayakutawaliwa na Ufaransa wala nani kama Ethiopia na Liberia wote wana changamoto hizo hizo.
Bado Somalia iliyotawaliwa na Uingereza, Ufaransa na Italia ndio shida kabisa. Hivyo huwezi kusema ni mataifa yaliyotawaliwa na Ufaransa tu ndizo zenye shida labda kwa sasa na mifumo ya jeshi katika nchi hizo ni tofauti sana na nchi kama Tanzania ambapo jeshi linakuwa ni kitengo cha chama tawala.