Kwanini French speaking African nations ndio zina vita tu?

Usikute kaweka tu hiyo Avatar tegesha kwani sio ya kwake. Angalia usije ukauziwa mbuzi ndani ya gunia.
Napenda your humor, ndiyo maana nimemtania nikijuwa fika si yeye kwenye avatar. Kwa taarifa yako, mpaka leo hajanijibu kwa sababu anajuwa si yeye kwenye avatar.
 
 
Because they're free to resist any oppression lodged by their oppressors. However, English speaking African countries are no better.
 
Wafaransa waliwalea hivyo kwa vita vita tu
Waingereza ni tofauti sana
Angalia mpaka leo wafaransa wachokozi hata kwenye bahari kutwa wavuvi wao kupigana na wavuvi wa uingereza kisa samaki tu [emoji23]
 
 
Sababu kubwa ninkuwa mkoloni mfatansa kwenye political administration yuko dhaifu sana

Mifumo ya kisiasa ya mkoloni.mwingereza aliiweka mizuri mno kuliko mfaranda
 
Sababu kubwa ninkuwa mkoloni mfatansa kwenye political administration yuko dhaifu sana

Mifumo ya kisiasa ya mkoloni.mwingereza aliiweka mizuri mno kuliko mfaranda
Nadhani Ufaransa pia ana sera ya ‘destabilization’ ili kuweza kufanya unyonyaji wa makoloni yake ya zamani kirahisi. Hii ni moja ya sababu
 
Tatizo watu mnaangalia zaidi leo na hamjui historia kwani kila nchi imekuwa na matatizo katika kipindi fulani.

Kuna kipindi hiyo hali ilikuwa ikizikabili hata mataifa yaliyotawaliwa na Uingereza, Spain na hata Ureno vilevile.

Tuliona Sudan na hadi leo hii bado tunaona Sudan ni shida tupu, tuliona Uganda, Ghana, Nigeria, Sierra Leone, Gambia, Zimbabwe, vurugu za Kenya kila baada ya uchaguzi.

Hata hapa Tanzania hamna amani yoyote ila kuna ka utulivu tu lakini huko tuendako tusitegemee hali hii kuendelea kwa aina ya utawala huu tulio nao, safari bado ndefu sana.

Mataifa yaliyotawaliwa na Ureno kama Guinea Bissau, Msumbiji na Angola yamekuwa kwenye vurugu kwa muda mrefu sana.

Tukiangalia mataifa yaliyotawaliwa na Ubelgiji kama Congo, Rwanda na Burundi ni yale yale, hivyo kusema vurugu ni kwa mataifa yaliyotawaliwa na Ufaransa tu ni kutokujua wapi tumetoka na bado kuna mataifa mengine ambayo hayakutawaliwa na Ufaransa wala nani kama Ethiopia na Liberia wote wana changamoto hizo hizo.

Bado Somalia iliyotawaliwa na Uingereza, Ufaransa na Italia ndio shida kabisa. Hivyo huwezi kusema ni mataifa yaliyotawaliwa na Ufaransa tu ndizo zenye shida labda kwa sasa na mifumo ya jeshi katika nchi hizo ni tofauti sana na nchi kama Tanzania ambapo jeshi linakuwa ni kitengo cha chama tawala.
 
Ni Mataifa Yanayozungumza Kifaransa sio yaliyotawaliwa na Mfaransa, japo si yote.
 


ASSIMILATION ☝

Assimilation: inahusisha mabadiliko ya jumla kwenye maisha ya binadamu na mitizami yake.

Walipoondoka wakawaacha wale ambao ni assimilated na non assimilated.

Goma ndo huchezwa hapo, mmoja anamuona mwenzie ni mbwiga vs yeye assimilated ni mjanja/ubaguzi wa kutokubaliana na kuwa na mapatano. Mkiwa mnafahamu wa upande huu mlipinga au hamkuiva kwenye assimilation.

Tukumbuke assimilation inaanzia kwenye kila hali ya ubinadamu: uchumi, uongozi, utamaduni, nk.
 
Sababu mojawapo ni Waingereza walijitahidi kuhakikisha kuna serikali na taasisi za kueleweka katika makoloni yao kabla ya kuwapa uhuru, Ufaransa wao walikuwa wanaondoka tu wanaachua madaraka kama gombania goli katika makoloni yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…