Hapa labda niulize tunazungumzia "guest houses" zile za Uchochoroni - similar to some Cheap Motels au kumpeleka mtu kwenye Hoteli ya kiukweli. Maana wengine kutokana na uduni wa makazi yao wanaona yule mdada hastahili kuingia kule kwetu Uswahilini hivyo ni bora aende wakajirushe Zanzibar au Morogoro au Arusha kwenye mojawapo ya Mahoteli fulani.. Hili la nadhani itakuwa ni kuwa amekuheshimu sana..
Tatizo liko kwenye vile vya chap chap ambapo mtu anajua kabisa kuwa haka ni kaswali ka mlo wa jioni na hana mpango wa kuendelea zaidi kwa hiyo anaona kuleta nyumbani inaweza kuleta ugomvi na mtu fulani ambaye aidha ana mpango naye au yuko naye serious.. Ila, pia kwanini hao kina dada wanakubali kwenda Guest? Mimi nadhani msichana anayekubali kwenda guest na kijana wake anakuwa amekubali masharti yake....
Lakini, kama wengine walivyodokeza, wengine wanaheshimu vizuri tu huyo mwenzake lakini kutokana na "logistical challenges" na labda "security issues" inabidi wakutane mazingira fulani mbali na nyumbani ila mambo ya kiiva vizuri basi anaweza kumleta nyumbani. Hii zaidini kwa wale ambao hawako huru hivyo katika nyumba au vyumba vyao.