Haya tujuze wenzio kama Kuna conflict of interest au hakuna ili tuelimike sote. Ni wapi bakheresa, Uhai, Azam FC, mo, Masafi, Simba SC wanakutana au hawakutani na Haji Manara kwenye kazi zake kama msemaji wa Simba na muuzaji wa maji ya Uhai.Kwani Haji ana mkataba na Mo au na Simba?
Umenichekesha kichizi.Nakubali!Kwa maisha ya Manara unavyoyaona unadhani 700000 kama mshahara inamtosha??
Wacha apige hela mzee unataka azeeke kama Mzee Mpili kuongelea uchawi uchawi tu wa kumaliza mechi nje ya uwanja[emoji16]
Lakini Nike na Adidas wahamiliki timu zao. Unaonaje kama Adidas wangekuwa wana timu Yao halafu Barcelona ikawa na mechi na timu ya adidas na Messi akiwa mchezaji wa Barca. Hapa Mo ana timu na Azam ana timu na zote ziko kwenye ligi moja.Nike wana mkataba wa kutengeneza jezi na barcelona lakini lionel messi ana mkataba binafsi na adidas kama nitakuwa sahihi.
Manara hana mkataba wa kazi na yeyote hapo juu, kwani Kathibitisha hilo kwenye voice note zake kwamba anafanya kazi bila mkataba na analipwa laki sabaKwani Haji ana mkataba na Mo au na Simba?
Kwani maji ya Mo yana mkataba na Simba, anachokosea Haji Manara ni kushindwa kutofautisha ajira yake na mikataba yake binafsi. Bakhresa na Gsm wanatamani kutangaza bidhaa zao kupitia washabiki wa Simba lakini wanajua itakuwa vigumu kupata hiyo nafasi
Bakhresa sababu mwekezaji wa Simba ana bidhaa shindani dhidi yake wakati Gsm anajulikana ni mshabiki na mfadhili wa yanga walichofanya ni kumtumia Haji ama kwa kujua au bila kujijua.
Mfano halisi ni siku Simba wanapokea kombe baada ya mechi na Namungo badala ya Haji kuizungumuzia Simba anaanza kupromot bidhaa za Azam.
Haji akifukuzwa au kujitoa Simba dili zote zitakufa maana walengwa watakuwa hawapatikani na ndio maana alikuwa na kiburi cha kukataa kusaini mkataba wa mshahara wa milioni 4akijua fika atakosa malupulupu mengine.
Kipindi kile anapelekwe Spain wakati kaajiliwa alichukua likizo au alikuwa akitumikia mabwana wawiwi.
Kipaumbele kwasasa ni mechi ya kesho.. Mkakati ni kumuandhibu UTO FC..kwa kumdunga magoli ya aibuKuna kitu kinaitwa "conflict of interest"
Je, inaswihi kwa Haji ambae Boss wake mo ana biashara ya Maji na wakati huohuo Haji kwenda kutangaza biashara ya Maji kwa Azam? mo ana maji ya masafi na Azam ana maji ya Uhai. Mo ana timu ya Simba na Azam ana timu ya Azam.
Hii imekaaje kikanuni?
Kushoto mkataba wa kazi kulia mkataba wa biasharaKwani Haji ana mkataba na Mo au na Simba?