Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na bado hiyo ni trailer bado picha kamili.Majuzi kati hapo nilifika kisiwani Unguja nilishangaa sana kupita huku na huko katika pilika pilika za maisha.
MADA; Ukweli Zanzibar pamoja na sensa iliyopita kuonyesha kuwa na watu 1,8mil ambao kwa muktadha wa wingi wa watu na waliopo Tanganyika ni chini ya mkoa wa Manyara yenye watu 1.9mil kiuwiano.
Katika kuangalia maendeleo ya maisha kwa ujumla inaonekana si kwa kiwango kikubwa wananchi wakiwa na kipato kikubwa kutokana na maisha ya kila siku.
Naona Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafanya uwekezaji mkubwa sana kwenye ujenzi wa shule, ambapo nyingi ya Shule hizi huwezi kuikuta popote nchini Tanganyika landa iwe ya binafsi.
Ujenzi wa hizi shule ni kama hauendani na wingi wa wanafunzi waliopo Zanzibar, tofauti na wingi wa wanafunzi waliopo Tanganyika.
View attachment 2670179
Hiyo juu ni moja ya skuli ya sekondari ambayo kwa sasa ipo asilimia (kwa kukadilia) 90% kukamilika na pembeni yake kuna jengo lingine kubwa kama hilo, hapo naambiwa yapo majengo mengine sehemu nyingine kama hilo yanajengwa.
Ukija hapa Tanganyika, sijui serikali inawaza nini na ndiyo maana hatuwezi kiwa sawa.
View attachment 2670185
Bajeti kubwa ya muungano inaenda Zanzibar na Tanganyika inabaki ukiwa kwenye suala la ujenzi wa majengo ya elimu.
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.Majuzi kati hapo nilifika kisiwani Unguja nilishangaa sana kupita huku na huko katika pilika pilika za maisha.
MADA; Ukweli Zanzibar pamoja na sensa iliyopita kuonyesha kuwa na watu 1,8mil ambao kwa muktadha wa wingi wa watu na waliopo Tanganyika ni chini ya mkoa wa Manyara yenye watu 1.9mil kiuwiano.
Katika kuangalia maendeleo ya maisha kwa ujumla inaonekana si kwa kiwango kikubwa wananchi wakiwa na kipato kikubwa kutokana na maisha ya kila siku.
Naona Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafanya uwekezaji mkubwa sana kwenye ujenzi wa shule, ambapo nyingi ya Shule hizi huwezi kuikuta popote nchini Tanganyika landa iwe ya binafsi.
Ujenzi wa hizi shule ni kama hauendani na wingi wa wanafunzi waliopo Zanzibar, tofauti na wingi wa wanafunzi waliopo Tanganyika.
View attachment 2670179
Hiyo juu ni moja ya skuli ya sekondari ambayo kwa sasa ipo asilimia (kwa kukadilia) 90% kukamilika na pembeni yake kuna jengo lingine kubwa kama hilo, hapo naambiwa yapo majengo mengine sehemu nyingine kama hilo yanajengwa.
Ukija hapa Tanganyika, sijui serikali inawaza nini na ndiyo maana hatuwezi kiwa sawa.
View attachment 2670185
Bajeti kubwa ya muungano inaenda Zanzibar na Tanganyika inabaki ukiwa kwenye suala la ujenzi wa majengo ya elimu.
Naunga mkono Hoja kwa 100%Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.
1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?
2. kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.
3. wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.
4. mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?
nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.