Kwanini hakuna usawa Ujenzi wa Majengo ya Shule, Kati ya Tanganyika na Zanzibar?

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡UPUUZI
Bajeti kubwa ya muungano inaenda Zanzibar na Tanganyika inabaki ukiwa kwenye suala la ujenzi wa majengo ya elimu.
πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†
HAYA TUPE NA UWIANO WA MAFISADI TOKA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.
 
Na bado hiyo ni trailer bado picha kamili.
Ikifika 2030 kwa hali hii ya Saa100 zanzibar itakuwa Dubai.
 
Nauchukia Muungano.Naitaka Tanganyika yangu.
 
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.

1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?

2. kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.

3. wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.

4. mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?

nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.
 
Ndugu Yesu Anakuja jana hapo nilikuwa Dodoma kwenye mkutano wa mzee Kinana na wanahabari nasi wanaCCM kama kawa hatuna jambo dogo tulijazana.

Katika kuongea kwake mzee K aliongea mengi sana alipofika kwenye muungano hakujua anaongea nini, alisema "kulikuwa na nchi mbili moja ni Zanzibar ..."

Hiyo nyingine hakuitaja, hapo lazima aliongea akijua woote tulikuwa pale ni zero kichwani.

Kwenye hiyo nchi ambayo hakuitaja ndimo kuna vugu vugu la kutaka mabadiriko ya kinyonyaji ambayo Yesu Anakuja umeyahainisha, matatizo kukiko ambavyo wanasiasa wanahubiri.
 
Naunga mkono Hoja kwa 100%
 
Acheni kusambaza propaganda za uwongo zinazo zalisha chuki, Hizo shule zimekuwa zikijengwa Zanzibar kwa muda mrefu sana na sio baada ya Samia kuwa Raisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…