Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Mleta mada;
Kwanza nikupongeze kwa sawali lako zuri, iwapo kweli unahitaji kufahamu ili kuongeza maarifa. Lakini kama dhamiri yako kejeli, nikupe pole.
Mimi nachukulia unahitaji kujifunza na kuongeza maarifa zaidi. Hivyo nitajitahidi kadri roho wa Mungu atakavyoniongoza kueleza hoja hii, pamoja na nyingine ambazo zipo humu kwenye uzi wako.
Nianze na hoja niliyoona kuwa Biblia ni hadithi za kutungwa zilizotungwa na watu.
Hoja hii ina ukweli na uongo ndani yake.
Ukweli wake ni kwamba, ni sahihi mtu akisema kwamba, maneno yote yaliyonenwa kwenye biblia yalinenwa na wanadamu. Yaani kila kitabu cha Biblia kina mwandishi/waandishi wake.
2 Petro 1:21
[21]Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu;
bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Uongo wa hii hoja ni kuwa, mambo yaliyonenwa kwenye biblia ni ya kutunga. Hii ni hapana na ni upotoshaji mkubwa. Angalia mstari nilioweka hapo juu, inasema, hao wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na roho mtakatifu. Ina maana kuwa, hayo sio maneno yao, bali ni maneno ya Mungu, na wao (kwa sababu wakati mengine yanatokea baadhi hawakuwepo, mfano musa hakuwepo wakati dunia inaumbwa, aliongozwa na roho Mtakatifu kuyajua hayo).
Sasa hapa kama hujui roho mtakatifu ni nini na kazi zake ni zipi, you've a work to do.
Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Jibu la hili swali ni kwamba;
Mke wa Kaini alitoka miongoni mwa watoto wa Adamu na Hawa.
Biblia inasema hivi; Hawa ni mama wa wanadamu wote.
Mwanzo 3:20
Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.
Sasa unaona, kama biblia inasema Hawa(Eva) ni mama yao wote walio hai, hivyo na mke wa Kaini alizaliwa na Adam na Eva pia.
Je, kama mke wa Kaini alizaliwa na Adam na Hawa, alizaliwa wakati gani?
Kabla sijajibu swali hili, inafaa uelewe kuwa, biblia haina utaratibu wa kutaja watoto wote wa mzaliwa wa mtu. Walitajwa wachache tu, kwa makusudi maalim tena ya kufundishia kibiblia.
Kwa mfano, Suleiman alikuwa na wanawake 700 na masulia wanaofikia 300. Lakini Biblia haikutaja uzao wa Suleiman kwa kila mke na kila suria.
Hata Adam na Hawa wenyewe, walizaa watoto wengi sana. Na biblia haiwataji. Badala yake inasema, Adam akazaa watoto wengi, waume kwa wake.
Mwanzo 5:4
Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
Sasa basi, kwa kuzingatia maelezo hapo juu, kuwa sio watoto wote biblia inazungumzia kuzaliwa kwao;
Mke wa Kaini huenda alizaliwa kabla ya kuzaliwa kwa Kaini au baada ya kuzaliwa kwa kaini.
Sababu za kusema hivyo ni kuwa;
1. Wakati kaini anafukuzwa, alisema watu wakimwona watamwua. Hii ina maana, tayari kulikuwa na uzao wa watoto wengine wa Adam na hawa. Kumbuka, kama tulivyoona huko juu kuwa, hawa ni mama wa kila mtu.
Mwanzo 4:14
[14]Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
Hapa unaweza kuniuliza kuwa, kwa nini ndugu wa uzao wa adam wamwue kaini ndugu yao?
Jibu ni kuwa, kama vile ambavyo kaini alimwua Habili nduguye, ndivyo na wao wangemwua. Pia kama walikuwa wanaweza kuoana, sembuse kuuana?
Pia, wakati nasema kuwa; mke wa Kaini alitokana na uzao wa Adam na Hawa, nimesema kuwa huenda alizaliwa kabla au baada yake, maana biblia imenyamaza hapo kuhusu nafasi yake.
Na ni utaratibu wa kawaida kabisa umeonekana kwingi.
Kwa mfano, Yese baba yake Daudi alikuwa na watoto wengine wakubwa, lakini ambaye yuko recognized ni daudi ambaye alikuwa mdogo. Hata daufi, watoto wake wakubwa hawako recognized kwenye kuendeleza kizazi, isipokuwa Suleiman ambaye alikuwa mdogo tena katoka kwa mchepuko.
Mathayo 1:6
Yese akamzaa mfalme Daudi.
Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;
Pili, mke wa kaini hakuandikwa kuzaliwa kwake kwa sababu hapo zamani za kale za biblia, wanawake walikuwa hawahesabiki. Walikuwa wanahesabika wanaume tu. Hivyo, hata kuzaliwa kwa mke wa kaini hakukusemwa kwa sababu alikuwa mwamake, yeye na watoto wengine wa kike wa adam, na wengine wa kiume (isipokuwa watatu tu) hawakusemwa. walisemwa Kaini, Habili na Seth. Seth naye alisemwa sababu ya habili kufa na kaini kukataliwa, otherwise biblia huenda isingemtaja.
Soma Mathayo 1:1-16. Utaona hapo biblia inataja vizazi kuanzia cha Ibrahim hadi Yesu, hakuna mwanamke kaongelewa hapo.
Swali Jingine ni je; Kaini alimwoa dada yake? Je, ilikuwa inaruhusiwa hiyo?
Jibu ni kwamba, pamoja na kwamba haikutamkwa, lakini mazingira yanaonyesha hivyo kuwa kaini na mkewe walikuwa ndugu.
Unachopaswa kufahamu hapa ni kuwa, kabla ya sheria za Musa, ambazo alipewa na wana wa Israel katika mlima Sinai, wakati ambao waisrael walikuwa Jangwani wakifoka Utumwani Misri kwenda kamaani, hakukuwa na katazo lolote la ndugu kuona.
Vizazi vyote vilivyoishi kuanzia adam hadi kuja kwa wairael kabla ya kutoka misri, walikuwa hawafungwi katika jambo hili.
Mfano.
1. Watoto wa Lutu walimnywesha mvinyo baba yao, wakalala naye na wakapata mimba. Wala Mungu hakuwaadhibu.
Soma Mwanzo 19:30-28
2. Ibrahim alimwoa Sarah (Sarai) ambaye alikuwa ni dada yake mtoto wa baba yake mkubwa.
Mwanzo 20:12
[12]Naye kweli ni ndugu yangu, binti wa baba yangu ila siye mwana wa mama yangu, ndipo akawa mke wangu.
3. Isacka mtoto wa Ibrahim, alimwoa mkewe Rebeca aliyekuwa ni nduguye upande wa mama yake, ikiwa ni maelekezo ya Mungu mwenyewe, kwamba asije akaoa mke kutoka jamii nyingine.
Mwanzo 24:1-28
4. Yakobo (Israel) alioa mtu na mdogo wake, wote wakiwa ni watoto wa mjomba wake (Labani). Kumbuka Mungu aliwaambia wasioe watu wa jamii nyingine, isipokuwa jamaa ya Ibrahimu, na ukumbuke Ibrahim na mkewe pia walikuwa ndugu. So hapo ilikuwa ni intermerriage ya kutosha, na Mungu aliruhusu.
Mwanzo 29:1-35.
Mungu wakati huu hakuwa amezuia kabisa suala hilo, na inaonekana madhara yake hayakuwepo.
Hata hivyo, baada ya Mungu kuwatoa waisrael utumwani misri, (kumbuka waliotolewa huko ni wajukuu, vitukuu, vilembwe na vilembwekazi vya yakobo), ndipo hapo Mungu akaweka sheria ya kutooana ndugu kwa ndugu, kupitia kwa Musa.
So sheria hii ikukuja baadae sana.
Soma Mambo ya walawi 18:1-29
Maagizo haya yalitolewa na Mungu kwenda kwa wana wa israel kupitia kwa Musa, katika mlima Sinai.
Ubarikiwe sana mpendwa, unapoendelea kujifunza na kutafakari neno la Mungu.