Kwanini Hayati Dkt Magufuli aliichukia sana Kaskazini lakini sasa Rais Samia anaipenda sana hii Kanda?

Kwanini Hayati Dkt Magufuli aliichukia sana Kaskazini lakini sasa Rais Samia anaipenda sana hii Kanda?

Kuanzia Mkapa pamoja na kuwa alioa mchaga, Kikwete na Magufuli waliipa mgongo hasa Kilimanjaro.

Nyerere, Mwinyi na sasa Samia anapeleka maendeleo kila sehemu bila kubagua!!

Samia kwa kipindi kifupi sana ameisaidia sana kaskazini hasa Arusha!!
Si kweli mkuu, Mkapa, Kikwete wameleta maendeleo sana Kaskazini, nakumbuka barabara ya Lami Rombo, pamoja na umeme zililetwa na Mkapa

Magufuli alikuwa akichukia upinzani pengine ndio maana anaonekana kama aliitenga kaskazini ambayo ilichagua wawakilishi wengi kutoka upinzani
 
Ku plan mradi fulani halafu usipeleke pesa ni sawa haujafanya chochote! Huu mradi wa maji unawezekana ulikuwa ni mpango tangu awamu ya Kikwete lakini kama Samia ndo amepeleka pesa kwa asilimia 100 anafaa kupongezwa sana kwenye ili na sio awamu ya nne!!

Biashara ya utalii Arusha hata kabla ya Covid ilianza kufanya vibaya. Yule aliyekuwa DC wa hai - anayejisahidia kwenye ndoo sasa hivi - alichangia sana kuiharibu. Ulisikia alikuwa hakivamia mahoteli ya kitalii usiku na kuimiza wamiliki kutoa rushwa. Mahoteli makubwa kama Impala yalianza kufa, bureau de change zilifungwa. Jitihada nyingi zilitumika kuamishia wanyama mkoa mwingine.

Samia ameonyesha nia za kuinyanyua tena hii sekta ya utalii kupitia Royal tour na miradi aliyopeka Arusha. Lakini Changamoto bado zipo, waliopo chini yake waanze kufikiria nje ya boksi!!!!
Hivi mzee baba wewe si ulikuwa ukimsifia sana mwendazake? Au nimechanganya ID?
 
Yeye alichukia ubadhilifu ikatokea bahati mbaya wabadhilifu waliowengi wakawa wanatokea huko

Hakuna ubishi hawa jamaa walijinufaisha Sana kwakutumia nafasi zao na walitumia vema fursa zao na kuwabeba NDUGU zao.

Kilichofanyika ni kupulizia dawa ya sumu kwenye shimo walilojificha matokeo yake waliumia wadudu wanaofanana
Na sasa hivi KAFIA MBALI... Kaskazini bado inatamba
 
View attachment 2203354
Tanzania tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi miongo mitatu iliyopita,

Kanda yote ya kaskazini imeanguakia kwenye mikono ya Upinzani na wapinzani,

Hayati Rais Dkt Benjamin William Mkapa ndio Rais wa kwanza kuonja shubiri ya Upinzani na Wapinzani Tanzania,

Mpinzani wa kwanza strong wa CCM alitoka kanda ya kaskazini Mkoa wa Kilimanjaro,

Mhe Dkt Augustine Lyatonga Mrema Mchaga wa Kiraracha Vunjo ndio Mtanzania wa kwanza aliyeitikisa CCM vilivyo,

Mhe Dkt Augustine Lyatonga Mrema Mchaga wa Kiraracha Vunjo aliwahi kuwa mgombea tishio wa Urais wa JMT kupitia Chama cha NCCR -Mageuzi,

Tangu enzi za Mchaga Dkt Augustino Lyatonga Mrema hadi sasa kwa akina Freeman Mbowe wa CHADEMA mchaga wa Machame Vyama vyote 19 vya Upinzani 83% vinaongozwa na watu kutoka Kanda ya kaskazi,

Kanda nzima ya kaskazini imekuwa ikionesha Upinzani mkubwa kwa CCM karibu katika kila chaguzi tangu Uchaguzi wa mwaka 1995,

Marais wote walioiongoza Tanzania baada ya mfumo wa Vyama vingi walichagua zaidi kuitenga kaskazini licha ya kaskazini kuwa mbele kimaendeleo kulikofanywa na wamisionari hata kabla ya Tanzania kupata Uhuru wake,

Hali ilikuwa mbaya zaidi awamu ya tano pale ambapo Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli alipotamka hadharani kuwa kaskazini inapashwa kusubiri ili na maeneo mengine nayo yapate maendeleo,

Leo mambo ni tofauti sana kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwani amemwaga miradi ambayo haijawahi kushuhudiwa huko kaskazini tangu Uhuru wa nchi hii,

Kuhusu miradi lukuki ya mabilioni inayojengwa na Rais Samia Suluhu Hassan kanda ya kaskazini nadhani kila anayeishi mikoa ya Tanga, K'njaro,Arusha na Manyara atakuwa shahidi wa yeye mwenyewe,

Nilipoona Rais Samia tena ameichagua na kuiheshimisha Arusha ya kaskazini kwa kuipa heshima kubwa ya Uzinduzi wa "Tanzania Royal Tour Film " hapa Tanzania,

Huu ukawa ushahidi wangu mwingine ulioondoa chembe ya shaka kuwa Rais wa Awamu ya Sita Mhe Samia Suluhu Hassan anaipenda sana kanda ya kaskazini kuliko Marais wote waliowahi kuiongoza Tanzania baada ya mfumo wa Vyama vingi mwaka 1992,

Mtakumbuka Rais Samia baada tu ya kuapishwa alikwenda Arusha na akatoa zaidi ya TZS 520BL sawa 80% ya bajeti nzima ya Wizara ya Maji ya Tanzania nzima akawapatia Arusha kwaajili ya Mradi mkubwa wa maji uliokwama tangu enzi za Rais Jakaya Kikwete,

Haya yote yawafungue macho wananchi wa mikoa ya Tanga, K'njaro, Arusha na Manyara kuwa CCM ya Awamu ya Sita Chini ya Mkt wake na Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan inawapenda sana,

Lazima Wafahamu kuwa hivi vyama vya Upinzani wanavyovikumbatia ndio haswa mchawi wao kwenye maendeleo yao hasa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi,

Kaskazini msipomuunga mkono huyu Mama itawachukua miaka mingi sana kupata mtu wa msaada kwenu kama huyu Mama,

NB, Ifikapo 2025 kaskazini haina chaguo zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan hii ni ndani na nje ya CCM, Kama kweli tunatamani kuiona kaskazini yetu inamea kwa kasi,

"Nani kama Samia? "
Kusini kwa ujumla tutafute Rais wetu,hatuna chetu Tanzania hapa.
 
Mkuu sichekeshi Niko serious Sana kwa hili..

Ni vile wapinzani ni pimbi hata hawasomeki ila hii ilitakiwa kuwa fursa kwao na kuanzisha strong hold kubwa kwa kuwaeleza watu wa huku Kusini kwamba licha ya umuhimu wao kwenye kuzalisha chakula Tzn ila mgawanyo wa rasilimali wanapunjwa na kupuuzwa na viongozi..

Inayoitwa Tanzania ya awamu ya 5 na awamu ya 6 ipo kwa ajili ya Dar, Zanzibar,Arusha,Dodoma na Mwanza yaani Kanda ya Mashariki/Pwani ya Kaskazini,Kaskazini,Kati na Lake zone..

Lakini Kanda ya Kusini,Nyanda za Juu Kusini Magharibi na Magharibi hatuna chetu.
 
Tanzania Upinzani utoke wapi?

CCM tutatawala miaka 100 ijayo, truest me
 
Si kweli mkuu, Mkapa, Kikwete wameleta maendeleo sana Kaskazini, nakumbuka barabara ya Lami Rombo, pamoja na umeme zililetwa na Mkapa

Magufuli alikuwa akichukia upinzani pengine ndio maana anaonekana kama aliitenga kaskazini ambayo ilichagua wawakilishi wengi kutoka upinzani
Kuna miaka nilipita uko uchagani Marangu nikaona mapipa ya lami yameozea kando kando ya barabara ya vumbi.
Hii inakupa picha kama waliweza kudiriki kusimamisha ujenzi ambao walikuwa wameshaingia gharama na ungechangia katika sekta ya utalii. Je kuna mambo mangapi ambayo walizuia kimya kimya!

Pia ile barabara ya Rombo nasikia ilikuwa delay sana na ilikuwa inatafutiwa sababu!!
 
Rais Samia ndio mtu Sahihi 2025 kama kweli tunahitaji na sisi wa kaskazini kutambulika kama WATANZANIA,

Hii tupende tusipende, Ila tukiendelea na ma-CHADEMA yetu tutabaki wa hivi hivi tu,
CM 1774858 CCM we proud on you,
 
Ku plan mradi fulani halafu usipeleke pesa ni sawa haujafanya chochote! Huu mradi wa maji unawezekana ulikuwa ni mpango tangu awamu ya Kikwete lakini kama Samia ndo amepeleka pesa kwa asilimia 100 anafaa kupongezwa sana kwenye ili na sio awamu ya nne!!

Biashara ya utalii Arusha hata kabla ya Covid ilianza kufanya vibaya. Yule aliyekuwa DC wa hai - anayejisahidia kwenye ndoo sasa hivi - alichangia sana kuiharibu. Ulisikia alikuwa hakivamia mahoteli ya kitalii usiku na kuimiza wamiliki kutoa rushwa. Mahoteli makubwa kama Impala yalianza kufa, bureau de change zilifungwa. Jitihada nyingi zilitumika kuamishia wanyama mkoa mwingine.

Samia ameonyesha nia za kuinyanyua tena hii sekta ya utalii kupitia Royal tour na miradi aliyopeka Arusha. Lakini Changamoto bado zipo, waliopo chini yake waanze kufikiria nje ya boksi!!!!
Ndugu mradi wa maji Arusha upo financed by AfDB 100% hakuna hela inayotoka serikalini direct, pili mradi huu tangu uanze haujawahi kukwama kwa ajili ya fedha acha kuwaambia watu oungo.
 
Ukweli ni kwamba mama anawapenda watanzania wote bila kujali makabila wala dini zao. Ni jambo zuri sana katika kutuunganisha Watanzania. Hata kanda nyingine ameenda. Huyu ndio aina ya kiongozi tunae mhitaji.
 
Mkuu sichekeshi Niko serious Sana kwa hili..

Ni vile wapinzani ni pimbi hata hawasomeki ila hii ilitakiwa kuwa fursa kwao na kuanzisha strong hold kubwa kwa kuwaeleza watu wa huku Kusini kwamba licha ya umuhimu wao kwenye kuzalisha chakula Tzn ila mgawanyo wa rasilimali wanapunjwa na kupuuzwa na viongozi..

Inayoitwa Tanzania ya awamu ya 5 na awamu ya 6 ipo kwa ajili ya Dar, Zanzibar,Arusha,Dodoma na Mwanza yaani Kanda ya Mashariki/Pwani ya Kaskazini,Kaskazini,Kati na Lake zone..

Lakini Kanda ya Kusini,Nyanda za Juu Kusini Magharibi na Magharibi hatuna chetu.
Pigeni kazi
 
Back
Top Bottom