Kwanini Hayati Dkt Magufuli aliichukia sana Kaskazini lakini sasa Rais Samia anaipenda sana hii Kanda?

Kuanzia Mkapa pamoja na kuwa alioa mchaga, Kikwete na Magufuli waliipa mgongo hasa Kilimanjaro.

Nyerere, Mwinyi na sasa Samia anapeleka maendeleo kila sehemu bila kubagua!!

Samia kwa kipindi kifupi sana ameisaidia sana kaskazini hasa Arusha!!
Si kweli mkuu, Mkapa, Kikwete wameleta maendeleo sana Kaskazini, nakumbuka barabara ya Lami Rombo, pamoja na umeme zililetwa na Mkapa

Magufuli alikuwa akichukia upinzani pengine ndio maana anaonekana kama aliitenga kaskazini ambayo ilichagua wawakilishi wengi kutoka upinzani
 
Hivi mzee baba wewe si ulikuwa ukimsifia sana mwendazake? Au nimechanganya ID?
 
Na sasa hivi KAFIA MBALI... Kaskazini bado inatamba
 
Kusini kwa ujumla tutafute Rais wetu,hatuna chetu Tanzania hapa.
 
Mkuu sichekeshi Niko serious Sana kwa hili..

Ni vile wapinzani ni pimbi hata hawasomeki ila hii ilitakiwa kuwa fursa kwao na kuanzisha strong hold kubwa kwa kuwaeleza watu wa huku Kusini kwamba licha ya umuhimu wao kwenye kuzalisha chakula Tzn ila mgawanyo wa rasilimali wanapunjwa na kupuuzwa na viongozi..

Inayoitwa Tanzania ya awamu ya 5 na awamu ya 6 ipo kwa ajili ya Dar, Zanzibar,Arusha,Dodoma na Mwanza yaani Kanda ya Mashariki/Pwani ya Kaskazini,Kaskazini,Kati na Lake zone..

Lakini Kanda ya Kusini,Nyanda za Juu Kusini Magharibi na Magharibi hatuna chetu.
 
Tanzania Upinzani utoke wapi?

CCM tutatawala miaka 100 ijayo, truest me
 
Kuna miaka nilipita uko uchagani Marangu nikaona mapipa ya lami yameozea kando kando ya barabara ya vumbi.
Hii inakupa picha kama waliweza kudiriki kusimamisha ujenzi ambao walikuwa wameshaingia gharama na ungechangia katika sekta ya utalii. Je kuna mambo mangapi ambayo walizuia kimya kimya!

Pia ile barabara ya Rombo nasikia ilikuwa delay sana na ilikuwa inatafutiwa sababu!!
 
Rais Samia ndio mtu Sahihi 2025 kama kweli tunahitaji na sisi wa kaskazini kutambulika kama WATANZANIA,

Hii tupende tusipende, Ila tukiendelea na ma-CHADEMA yetu tutabaki wa hivi hivi tu,
CM 1774858 CCM we proud on you,
 
Ndugu mradi wa maji Arusha upo financed by AfDB 100% hakuna hela inayotoka serikalini direct, pili mradi huu tangu uanze haujawahi kukwama kwa ajili ya fedha acha kuwaambia watu oungo.
 
Ukweli ni kwamba mama anawapenda watanzania wote bila kujali makabila wala dini zao. Ni jambo zuri sana katika kutuunganisha Watanzania. Hata kanda nyingine ameenda. Huyu ndio aina ya kiongozi tunae mhitaji.
 
Pigeni kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…