Kwanini historia anayosimulia Sheikh Mohammed Said haipingwi hadharani?

Haina mashiko na umuhimu kihivyo mwanangu. Nadhani hakuna watu wenye muda wa kujadili manung'uniko na udini mwanangu.
 
Ipingwe hadharani na nani??
Hao unaotegemea waipinge hadharani hawasomagi hata vitabu vyovyote.
 
Tukiacha ushabiki wa kidini
Kuna sehemu yeyeto ya eneo la Tanzania lilikuwa na wakiristo waliopigana na wakoloni kuanzia wajerumani na mpaka Waingereza? zaidi ya kuwa vibaraka na matarishi wa wakoloni
Ukimtoa Nyerere kama Nyerere aliyeona mbali ya kwamba wenzake wamekuwa brainwashed mpaka akatoka alikotoka na kuja mjini kwenye vuguguvugu la kutafuta uhuru ambapo wengi aliokutana nao tunajua walikuwa wenye asili ya wapi na ni dini gani? kwanini asipiganie kupinga ukoloni hukohuko aliko kama kina Mkwawa
Na alipitia usaliti mwingi sana na vibaraka wa wakoloni ambao wengi walikuwa wakiristo walioogopa kupoteza kazi au kufungwa kwa kuuza nyaraka mipango yote ya harakati za uhuru kwa wazungu?
Fuatilia migomo ya wafanya kazi iliyokuwa inavurugwa na kina nani wakati wa kupigania uhuru ?

Hii ni tovuti ya JK NYERERE inayotambulika kimataifa, lakini imeandika hii article. kwa hiyo nyinyi vilaza muache kukaza fuvu kama kimba la asubuhi...








 
Kuwa kwao mbele ni sababu ya utanganyika wao na sio uislamu ndicho tunachopinga
 
Kwahiyo unataka kusemaje?
 
HASWAAA
 
Ushawahi kupinga historia ambayo hukuwepo?

Wote aliokua nao wameshakufa
 
Story za kwenye vigenge vya kahawa vya kariakoo tangu 1980's 🤣🤣🤣
 
Kuwa kwao mbele ni sababu ya utanganyika wao na sio uislamu ndicho tunachopinga
Inside10,
Hili la Uislam ndiyo chanzo cha tatizo la uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika.
TANU chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika waasisi wake hawakupata kutajwa katika historia rasmi.

Mimi nayajua majina ya waasisi wote.

Nayajua kwa kuwa yaliandikwa katika mswada wa kitabu alioandika Kleist Sykes kabla ya kufariki kwake mwaka wa 1949.

Mswada huu alikuwanao Abdul Sykes had mwaka wa 1968 alipompa mwanae Aisha ''Daisy'' Sykes aliyekuwa mwanafunzi wa Education and History University of East Africa na akaandika seminar paper akieleza maisha ya babu yake.

Hii seminar paper iko Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam East Africana: ''The Life of Kleist Sykes'' (1968).

Semina Paper hii ina majina tisa ya waasisi wa African Association: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisi, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Katika paper hii inaelezwa kuwa Wakristo walikuwa wanaonywa kanisani wasijiusishe na mambo ya siasa.

Hii ndiyo sababu ukiangalia hiyo orodha ya waasisi wa African Association utaona wengi wao ni Waislam.

Baada ya kuunda African Association 1929 Waislam hawa wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.

Naamini umeelewa hoja.
Angalia picha hiyo hapo chini:


Kulia Haruna Iddi Taratibu, Saadani Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafongo Dodoma Railway Station 1955/56​
 
Enzi za ujinga zilifika mwisho , uchifu ,udini , ubarbari ,utumwa ,ukoloni pia zilifika mwisho , suali la kujiuliza ;JEE HUU UTAWALA WA UHURU UTAFIKA MWISHO ???!
 
WAtu wapo busy na mambo ya msingi. Huoni hata nyuzi zake nyingi siku hizi watu wame ignore?
 
Kuna videos zina 1Milion views na ni za hovyo tu zinatokana na title inayosoma kwenye video huko youtube. Ningekuonesha moja sheikh yangu ambayo ina views 3,890,027 mpaka hii leo lakini wengi walivutiwa na nlichoandika kama title.

Watu wapo busy. Recently nimejaribu hata kufuatilia maandiko yako JF ni kama watu wanaona hakuna kipya. Unakosa comments sheikh wangu. Au zinakuwa chache sana. Watu wameshachoka wanataka mambo mapya na si yale yale ya MALALAMIKO NA LAWAMA.
 
Minjingu...
Umesema kweli kabisa.
Lakini mimi si katika kundi la "ovyo."

Nimeshirikishwa katika miradi kadhaa ya elimu na vyuo vikuu vingi.

Ninapoandika au kuzungumza hao ndiyo wasomaji na wa watazamaji wangu.

Hawa si watu wa ovyo.
Hili ni kundi la watu makini.

Kama unavyoona hapa JF nimekuwa Mwandishi Bora mara mbili mfululizo 2022 na 2023.
 
Hata Yericko amepewa tuzo nyingi za undishi huko tanzania na someplaces ila sometimes anaandika pumba sana.

Mi nakupongeza hukati tamaa.na usikate tamaa hata iweje. Endelea kuwaaandikia watu.
 
Hii komenti imenichekesha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…