mkuu wa kijiji
JF-Expert Member
- Apr 7, 2017
- 966
- 1,052
Kuna tofauti kati Waarabu na Uislam, Na Kuna viashiria vya baadhi ya wachangiaji wana waadhibu Waislam Kwa makosa ya waarabu, si Sawa . Waarabu wapo mpaka walokole kama si Othodox au Roma.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Gavana, kwanza pole kwa madhila ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kwa hayo unayoyasema, kila binadamu mwenye utu, yatamgusa, hata nilipokisikia kisa cha Hamudi iliyemuua Karume, nikaelewa.
Hili la ubaguzi Zanzibar lipo, tena sio tuu ni ubaguzi wa kutubagua Wabara, hata nyinyi wenyewe kwa wenyewe mnabaguana, Luna Wanzanzibari na Wazanzibara. Ndani ya Wazanzibari pia mnabaguana kuna Waunguja na Wapemba. Kwa vile Pemba haikushiriki yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Wanamapinduzi kindakindaki waliwahi kujiapisha " Zanzibar imepatikana kwa Mapinduzi, Pemba haikushiriki Mapinduzi, hivyo Mpemba kamwe hawezi kupewa urais Zanzibar kwenye karatasi ".
Baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Wamatumbi ndio waliruhusiwa kujitwalia vibinti vya Kiarabu, na ilikuwa ni marufuku kukataa.
Mpaka leo, mpaka kesho, baadhi ya Waarabu wanajisikia wao ni bora zaidi, na baadhi ya Wamatumbi wanajisikia wanyonge.
P
Mkuu Gavana, kwanza pole kwa madhila ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kwa hayo unayoyasema, kila binadamu mwenye utu, yatamgusa, hata nilipokisikia kisa cha Hamudi iliyemuua Karume, nikaelewa.
Hili la ubaguzi Zanzibar lipo, tena sio tuu ni ubaguzi wa kutubagua Wabara, hata nyinyi wenyewe kwa wenyewe mnabaguana, Luna Wanzanzibari na Wazanzibara. Ndani ya Wazanzibari pia mnabaguana kuna Waunguja na Wapemba. Kwa vile Pemba haikushiriki yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Wanamapinduzi kindakindaki waliwahi kujiapisha " Zanzibar imepatikana kwa Mapinduzi, Pemba haikushiriki Mapinduzi, hivyo Mpemba kamwe hawezi kupewa urais Zanzibar kwenye karatasi ".
Baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Wamatumbi ndio waliruhusiwa kujitwalia vibinti vya Kiarabu, na ilikuwa ni marufuku kukataa.
Mpaka leo, mpaka kesho, baadhi ya Waarabu wanajisikia wao ni bora zaidi, na baadhi ya Wamatumbi wanajisikia wanyonge.
P
Dos ...
Hata mimi sijui kwa nini ilikuwa hivyo.
Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja Nabii Abraham, (Ibrahim). Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismael (Ismaili) aliyezaa na mtumwa mjakazi wa Kimisri, Hajir (Hagai). Wakristo ni uzao wa mwanae wa pili Isaac (Isiaka).Kuna tofauti kati Waarabu na Uislam, Na Kuna viashiria vya baadhi ya wachangiaji wana waadhibu Waislam Kwa makosa ya waarabu, si Sawa . Waarabu wapo mpaka walokole kama si Othodox au Roma.
Ndivyo alivyoanza katika ngano ya Sykes kwa kumfanya Nyerere si lolote si chochote na kuzua yale ya bandiko#39 kuhusu ujio wa Nyerere Dar."Pascal Mayalla, post: 33648454, member: 17813"]Hii hoja ya kumleta Okello na kusema Okello sii lolote sii chochote ni tuu kuhalalisha ile hoja yake ya zile ngano za Kipumbwi ili kuonyeshea waliompindua Sultan, sio Wanzanzibari bali ni Wanzanzibara.
Ndiyo maana katika picha ya Okello isiyo na tarehe, mahali na majina ya washiriki ametumia neno ''Wazanzibar Khalisi''Zanzibar kuna ubaguzi sana wa matabaka, tabaka la juu walikuwa Wazungu, Europeans, wakafuatia Indians, Arabs, Washirazi na machotara, tabaka la mwisho ni Wamatumbi, ndio wanaitwa Africans, sasa katika ujumla wake, wanahesabu wenye halali ya kuwa Wanzanzibari halisi ni Wahindi, Waarabu na Machotara, ambao kwao hao ndio Wazanzibari wale Africans wanawaita Wanzanzibara.
Hapa anapata wakati mgumu sana.Sasa ili kuyadogosha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hatua ya kwanza ni kumdogosha kiongozi wa Mapinduzi yale Okello kuwa sii lolote sii chochote.
Kisha kuweka picha ya Wajumbe wa Baraza la kwanza la Mapinduzi, ndio waliopindua ili kuonyeshea sio Wanzanzibari, bali ni watu wakuja wakishirikiana na Wanzanzibara.
Lengo ni juhudi za kuya discredit Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ili wayaite mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Wanzanzibara kuwateketeza Wazanzibari.
Nguruvi 3,Ndivyo alivyoanza katika ngano ya Sykes kwa kumfanya Nyerere si lolote si chochote na kuzua yale ya bandiko#39 kuhusu ujio wa Nyerere Dar.
Miaka 10 iliyopita aliweka picha za Nyerere akiwa na Kaptula yake kama Mwl katika jitihada za kumfanya si lolote si chochote. Tunazo kumbu kumbu hapa JF
Kwa Okello, picha aliyoweka haina maelezo, ni jitihada tu za kumfanya si lolote si chochote
Kuhusu ngano za Kipumbwi, bandiko hili limeibua mengine.
Mzee kafanya kitu tunaita ''self inflicted wound'' katika bandiko#125 alipodai kwamba Abdallah K Hanga ndiye kiongozi wa Mapinduzi.
Kwa mantiki hiyo ni Hanga aliye organize Kipumbwi. Nyerere kasamehewa
Ndiyo maana katika picha ya Okello isiyo na tarehe, mahali na majina ya washiriki ametumia neno ''Wazanzibar Khalisi''
Kwamba ana challenge watu waonyeshe ''Wazanzibar khalisi'' kwa maana uliyoeleza hapo juu
Hapa anapata wakati mgumu sana.
Kusema Mapinduzi ni haramu ataudhi jamii ile inayoamini katika mapinduzi daima.
Kusema ni halali, ataudhi Wazanzibar anaoita ''khalisi''
Hayo yanamweka njia panda kwasababu kuna kitu ''common' kwa makundi 2 na yeye
Mshtuko mkubwa kwangu ni pale anaposema Sultan hana damu mikononi.
Yaani soko la binadamu walotengwa na familia zao, wanaokwenda kuhasiwa na kuteswa liwe chini ya usimamizi wa Sultan halafu mikono iwe safi! I mean duh! ngumu sana hii
Ndiyo! tunasema kuhasiwa kwasababu hakuna mabaki ya Waafrika middle east(Uarabuni)
Hata hoja ya TransAtlantic ni mufisili kwasababu, biashara hiyo imetokea tena ikiongozwa na Wamishenari wakiombea watumwa katika ''Door of no return''
Tofauti na Waarabu, Wazungu wanakiri unyama huo na leo kuna mjadala wa ''reparations''
2008 John McCain na Obama waliulizwa tukio baya la kiroho lililofanywa na Wamarekani
Wote walizungumzia mambo nje ya jambo moja, Utumwa.
Siku iliyofuata iliandikwa wazi kwamba hawakujibu sawa sawa, tukio baya la kiroho ni biashara ya utumwa.
Kasome maandiko na habari za Watumwa katika maktaba zao
Mabaki ya Watumwa yapo hadi leo, si Uarabuni.
Utumwa ni unyama tu uwe umefanywa na yoyote yule, tunachoshindwa kuelewa baadhi yetu ni jinsi watu wanavyotafuta uhalali wa biashara ya utumwa Zanzibar !!!
Tafadhali na haraka sana weka hiyo picha na ushahidi kuwa imewekwa kwa ajili ya kumdhalilisha Nyerere.
Sishinikizwi kama weweNguruvi 3,Mimi huwa sishinikizwi.Hupenda kufanya mjadala wa kistaarabu.
Wala sioni shida kujibu swali lolote kwani kama sijui nitakwambia.
Nguruvi3,Sishinikizwi kama wewe
Mohamed, wapo wanaokuambia kuwa historia yako ina tatiza watu.Muhimu ni huku mimi kueleza jinsi historia niliyoandika mimi ilivyotofautiana na historia rasmi iliyozoeleka.Mmesoma historia na matukio hamkupatapo kusoma popote.
Hapa ndipo panapowatatizeni.
Akili inataabika kuamini kuwa haya usomayo ni kweli na yale uliofundishwa shule hayakuwa yamekamilika.Lakini ikiwa utaiuliza akili yako kwa nini iwe hivi, haitakuwa tabu kupata jibu.
Nguruvi 3,Mohamed, wapo wanaokuambia kuwa historia yako ina tatiza watu.
Pengine wanafanya hivyo kukupendeza!
Binafsi nikueleze sitatiziki na historia yoyote , nina tatizika na facts.
Swali ninalojiuliza baada ya kutuliza akili yangu ni moja, hivi kuna motive gani ya kubadilisha historia au kuzua au kupotosha?
Mfano, kwanini mtu anajua Nyerere alifika Dar mwaka 1948, lakini anakataa hata pale penye ushahidi. Nini motive ya mtu huyo! Hivi ndivyo vina tatiza wengi
Tena vina tatiza kwasababu kama ukweli mdogo kama huu unakataliwa, ukweli usiohitaji hata dakika ya fikra, yale wasiyoyajua watu yana ukweli kiasi gani? Hili lina disturb sana
Tangu mkutano wa Arnatouglo hadi 1961, Abdul alikuwa na ushiriki gani wa siasa za Tanzania? Kwanini alotoweka katika uongozi baada ya muda huo"Mohamed Said, post: 33689460, member: 12431"]
Nimepata kuulizwa kwa nini nadhani historia ya TANU pale chama chenyewe ilipoamua iandikwe na Abdul Sykes na Dr. Wilbard Klerruu wakaanza hiyo kazi iliingia katika matatizo na Abdul Sykes akajitoa?
Hassan Upeka kajaliwa Umri? Kwa maana nzuri tu ya kuelewaNimepata kuulizwa pia kwa nini Chuo Cha CCM Kivukoni ilipoamua mwaka wa 1981 kuandika historia ya TANU "notes" za Hassan Upeka za mahojiano aliyofanya na Abdul Sykes kuhusu historia ya TANU zilikataliwa kupokelewa?
Unakumbuka Africa Now? Unamkumbuka mtu anayeitwa Abdulrahman Babu?Nimepata vilevile kuulizwa kwa nini jarida la Africa Events lilipochapa makala "In Praise of Ancestors,"mwaka wa 1988 makala yakimtaja Abdul Sykes katika historia ya kuasisi TANU toleo hili liliondolewa kwenye mzunguko?
Unakumbuka muda wakati alipotunukiwa kulikuwa na hali gani ya kisiasa? Nani alikuwa madarakani?Kipi kimepelekewa Abdul na Ally Sykes kutunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru baada ya miaka 50?
Kwa nini medali hii hawakupewa wazalendo wengine pia waliokuwa bega kwa bega na hawa ndugu wawili kama Hamza Mwapachu, Steven Mhando, Dr. Vedasto Kyaruzi, Sheikh Hassan bin Ameir, Zuberi Mtemvu kuwataja wachache?
Ni kitabu chako na una uhuru wa kukieleza unavyoweza. Ni maoni yako ambayo si lazima ya sahihi au makosa, tunayaheshimuKwa nini kitabu cha Abdul Sykes kimependwa kiasi hiki na kusababisha uchukuliwe uamuzi wa kuandika historià ya Mwalimu Nyerere na kuandika upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika?
Nguruvi 3,Tangu mkutano wa Arnatouglo hadi 1961, Abdul alikuwa na ushiriki gani wa siasa za Tanzania? Kwanini alotoweka katika uongozi baada ya muda huo
Hassan Upeka kajaliwa Umri? Kwa maana nzuri tu ya kuelewaUnakumbuka Africa Now? Unamkumbuka mtu anayeitwa Abdulrahman Babu? Unakumbuka muda wakati alipotunukiwa kulikuwa na hali gani ya kisiasa? Nani alikuwa madarakani?
Ni kitabu chako na una uhuru wa kukieleza unavyoweza. Ni maoni yako ambayo si lazima ya sahihi au makosa, tunayaheshimu
Hebu tuanzie hapa maana yapo mengi mazuri ya kujadili
Na bila shaka kwa rejea ya bandiko#191 aya ya kwanza, utakuwa umeambiwa pia kuwa Abdul Sykes na Wilbard Kleruu walipata matatizo walipotaka kuandika historia ya TANU"Mohamed Said, post: 33690121, member: 12431"]Abdul hakuwa mtu wa kupanda jukwaani.Lakini Abdul nimeambiwa alikuwa katika mikutano ya TANU ile ya mwanzo kabisa pale Mnazi Mmoja akionekana nyuma kabisa akichukua hotuba Nyerere akizungumza katika hati mkato (short hand) verbatim yaani neno kwa neno.
Hukuziona nyaraka na bado unatueleza historiaKatika mambo yanayonisikitisha hadi leo ni kule kutopewa idhini ya kusoma shajara za Abdul Sykes ambazo nimeziona kwa jicho langu.
Na alitaka kuandika historia ya TANU.Abdul hakuwa na nafasi yoyote katika chama kuanzia 1954 baada ya kuundwa kwa TANU.
Na unasikitika kutoona nyaraka za Abdul! lakini umetumia nyaraka kuandika historiaNdiyo maana nyaraka za TANU za wakati ule wanazo akina Sykes na ndiyo hizi nilizotumia kuandika historia ya TANU.
Umesema hakuwa na nafasi ndani ya chama. Kutoweka si kimaumbile bali katika siasa za nchi.Abdul hakutoweka.
Well, bila nafasi ndani ya TANU, aliweza kutenda. Kwamba bila Abdul, Nyerere angekuwa na wakati mgumu saana. Kwamba Nyerere alisafiria nyota ya AbdulNi viongozi mfano wa Abdul ndiyo waliifanya TANU ipendeze na Nyerere kama rafiki wa Abdul na yeye apendwe.
Nimesoma magazeti ya Africa Events na Africa Now. Nimemleta Abdulrahman Babu kwasababu alikuwa na makala zake kuhusu maendeleo ya Africa, na picha yake katika makala ilikuwa na 'sweta'' kama nitakuwa na kumbu kumbu sawa.Abdulrahman Babu tumefahamiana London nilijulishwa kwake na Ahmed Rajab aliyekuwa mhariri wa Africa Analysis.Ahmed akiandika na Africa Now gazeti la Peter Enahoro.
Siku hizo mimi nikiandika na Africa Events mhariri wake marehemu Mohamed Mlamali Adam.
Nimekuuliza kama ana umri kwa maana ya kama bado tupo naye. Katika bandiko 191 umesema naye alizuiliwa kuandika historia.Hassan Upeka kaingia TANU 1956 baada ya kumaliza Tabora School na moja kwa moja akatiwa kwenye ukachero.
Kudogosha ndiko huku.Ati TANU iliasisiwa nyumbani kwa Mzee Mwinjuma Mwinyikambi Mwananyamala ilhali Nyerere kapokelewa na Abdul Sykes na mipango ya kuunda TANU mara ya kwanza masikioni kwake kaisikia nyumbani kwa Abdul Kariakoo.
Nimepotea njiaMzee Mwinjuma akishakausha nazi zake anazipeleka Kariakoo sokoni na pale Market Master ni Abdul Sykes na Collector wa soko Sharif Abdallah Attas na ni kupitia kwa Abdul ndiyo Nyerere akamjua Mzee Mwinjuma na wazee wengine wa Dar es Salaam.
Shariff Attas akimjua vyema Mwalimu Nyerere na ni burdani ya pekee kumsikiliza akikumbuka siku zile wakiunda TANU.
Nyerere hakumjua Mzee Mwinjuma kwa kuwa aliundanae TANU.
Nguruvi3,Na bila shaka kwa rejea ya bandiko#191 aya ya kwanza, utakuwa umeambiwa pia kuwa Abdul Sykes na Wilbard Kleruu walipata matatizo walipotaka kuandika historia ya TANUHukuziona nyaraka na bado unatueleza historia
Na alitaka kuandika historia ya TANU.Na unasikitika kutoona nyaraka za Abdul! lakini umetumia nyaraka kuandika historia
Umesema hakuwa na nafasi ndani ya chama. Kutoweka si kimaumbile bali katika siasa za nchi. Well, bila nafasi ndani ya TANU, aliweza kutenda. Kwamba bila Abdul, Nyerere angekuwa na wakati mgumu saana. Kwamba Nyerere alisafiria nyota ya Abdul Nimesoma magazeti ya Africa Events na Africa Now. Nimemleta Abdulrahman Babu kwasababu alikuwa na makala zake kuhusu maendeleo ya Africa, na picha yake katika makala ilikuwa na 'sweta'' kama nitakuwa na kumbu kumbu sawa.
Magazeti hayo mwanzo nilidhani ni ya Nigeria kwasababu yalikuwa na habari nyingi za akina Murtala Mohamed, Obasanjo, Alhaji Othmani Shehu Shagari n.k.
Ni sehemu nzuri sana ya kupata ''coup de tat' zilizokuwa zinafanyika Nigeria
Hata hivyo, magazeti hayo yalikuwa yanasema sana Ujamaa wa Nyerere.
Moja ya habari nilizosoma zilihusu ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Termina 2
Kwamba, walisema Mwl hakuwa a haja ya kujenga uwanja mkubwa akiwa hana ndege
Pesa hizo zingetumika kuendeleza mabonde ya mpunga ingalikuwa bora zaidi
Makala hizo ziliendelea kuudhi viongozi wakati huo wa chama kushika hatamu.
ndipo yalipopigwa marufuku, wengine tuliyasoma kwa kupitia ''wazee' waliokuwa na access na sehemu nyingine kama Nairobi
Hoja yangu hapa ni rahisi, magazeti hayakupigwa marufuku kwasababu ya makala zako
Kama ilitokea basi ilikuwa ni katika ujumla ule ule wa kupiga marufuku
Hivyo basi unaposema makala zako ndizo chanzo, si kweli, ni kupotosha na kutafuta ''credit''
Nimekuuliza kama ana umri kwa maana ya kama bado tupo naye. Katika bandiko 191 umesema naye alizuiliwa kuandika historia.
Hakuna mahali umeweka ushahidi wa maneno yake au nyaraka za kuthibitisha hilo.
Tunaweza kukubaliana nawe kwani huenda umeambiwa Kudogosha ndiko huku.
Mwalimu alikuja Dar kikazi. Kabla ya hapo (1948) alikuja kisiasa. Hapa ni katika jitihada za kuonyesha mwenye TANU ni Abdul. Sina kumbu kumbu nzuri, hivi mkutano wa Anatoglo ulifanyika lini? Nimepotea njia
Nguruvi3,
Mimi sina tatizo na vipi unaichukulia historia ya TANU.
Kila siku nakuambia unaweza ukaikataa na wala si tabu kwangu.
Chuo Cha CCM Kivukoni wameandika historia hii na wala Abdul hakutajwa popote ila kwenye orodha ya watu 17 walioasisi TANU.
Hakuna aliyepelekwa polisi.
Maisha yameendelea kama kawaida.
Wakisema wao haya ,ni sawia,hawatii chuki nchini,lakini wakisemwa wao wayatendayo hivi kila uchao ni kosa la jinai na unaweza kuozea jela.Wanasiasa wameitumia historia ya Visiwa hivi kwa manufaa yao na kuzidisha chuki, na kutoelewana miongoni mwa raia wa kisiwa hichi. Uwafrika, Uwarabu, Utumwa ndio nyenzo na Turufu za watanganyika na zaidi wakristo kwa maslahi ya siasa. Pamoja na kuchakaa kwa nyenzo hizo bado viongozi wa naendelea nazo.
Wao ukiyaanika matendo walioututendea kuanzia 1964 hadi sasa huwa wanashindwa kuvumilia. Gazeti la DIRA la Marehemu Nabwa walilipiga marufuku kwa sababu eti lilikua likitia chuki nchini.