Mkuu Pasco ,
Gavana anajtahidi sana kupotosha umma ima kwa kujua au kutojua au kutotaka kujua.
Katika upotoshaji huo amefanikiwa kuwaburuza watu kama MS atika mkondo usio sahihi.
MS aliwahi kuhoji kwamba picha za watumwa ni za kuchora.
Hakuhoji kwavile hakuona hizo picha bali kuna hoja aliyosikia na bila utafiti au fikra au kwavile anaamini tu historia yake akaamua kutumbukiza hoja hiyo.
Yaani ana question picha za biashara ya utumwa! kama afanyavyo
Gavana
Sasa nimeelewa ni kwanini baada ya kumsoma Gavana akikazani kuhusu uvumbuzi wa camera mwaka 1888 ikilinganishwa na picha za biashara ya utumwa kabla ya hapo
Naomba niweke sawa kwanza, kwamba, watu kama MS na Gavana wanadhani kitu kama computer kimegunduliwa na Bill Gate au hakikuwepo miaka 100 iliyopita
Idea ya computation ilianza kutumika kwa slide rule na algorithm karne nyingi (kuanzia 1625?) kama sikosei.
Wakati wa industrial revolution, mashine zilikuwa zinafanya kazi kwa mfumo wa computer
Kilichofuata ni kuendeleza matumizi ya computer katika maeneo kama majeshi halafu maofisini.
Akina Bill Gates wamerahisisha kazi kwa software lakini si wagunduzi
Kuhusu Camera wazo la kwanza lilitolewa na mtu wa Iraq Haytham miaka 800 kabla ya Camera
Kilichofuata ni akina Johann Zahn Mjerumani akifuatiwa na Mfaransa Nicephore aliyepiga picha ya kwanza 1826
Katika mwendelezo wa improvement wapo akina Alexander n.k.
Kamera ya kwanza ilikuwa pinhole, zikaja za lens halafu colloidal na mwisho digital
Gavana anachanganyikiwa au anauchanganya umma kwamba Camera imevumbuliwa mwaka 1888.
Kilichotokea wakati huo ni Mmarekani Eastman kuwa na kampuni iliyoanza kutoa jina la Camera na brand zake zikawa ni Kodak.
Alichokifanya Eastman ni ku commercialize kamera.
Hivyo basi Gavana anaposema Camera imegunduliwa mwaka 1888 ni kutoelewa, kutotaka kusoma. Hayo yanafanyika kwa makusudi kabisa ili kuzima hoja zilizopo mbele kwasasa kuhusu mambo kadhaa.
1. Gavana kama Mohamed Said wanaturudisha wanakotaka. Tumewaambia dhahir shahir kuwa Biashara ya utumwa ni ukatili dhidi ya binadamu uwe umefanywa na Mzungu, Mwarabu, Askofu au Sheik. Ni ushenzi tu usioweza kutetewa na mtu anayefikri sawa sawa.
2. Kwa upande wetu biashara ya Uarabuni ili tuathiri sana kwani tulikuwa ndio Wahanga.
Unyama huo ulifanywa kupitia soko la watumwa la Mkunazini chini ya Sultan.
Hivyo sultan wa Zanzibar ni ''accomplice'' katika unyama huo iwe kabla au baada. Period
Kuna hoja zinazomhusu Mohamed Said, hizo zinafuata. Hakuna namna lazima tuwekane sawa kwa muda mrefu jukwaa hili limegeuzwa jamvi la msibani kila atakaye afanya ajuavyo.