Kwanini historia ya Zanzibar ya kweli haisomeshwi?

Kwanini historia ya Zanzibar ya kweli haisomeshwi?

Ulisahau kuandika mnunuzi wa watumwa Mreno na Mfaransa
Mkuu Gavana, japo ni kweli mnunuzi wa Watumwa alikuwa Mreno na Mfaransa, hao ni kwenye Trans Atlantic Slave Trade na sio Indian Ocean Slave Trade, katika bandiko hili

Nimezungumzia madhila waliyoyapata mababu zetu chini ya Mwarabu na Sultan wa Zanzibar.
P
 
Mkuu Gavana, japo ni kweli mnunuzi wa Watumwa alikuwa Mreno na Mfaransa, hao ni kwenye Trans Atlantic Slave Trade na sio Indian Ocean Slave Trade, katika bandiko hili

Nimezungumzia madhila waliyoyapata mababu zetu chini ya Mwarabu na Sultan wa Zanzibar.
P
Aliyeianzisha hiyo biashara ya utumwa Afrika Mashariki ni Mreno . Unataka kuniambia akimuuzia mwarabu??
 
Mkuu Gavana, japo ni kweli mnunuzi wa Watumwa alikuwa Mreno na Mfaransa, hao ni kwenye Trans Atlantic Slave Trade na sio Indian Ocean Slave Trade, katika bandiko hili

Nimezungumzia madhila waliyoyapata mababu zetu chini ya Mwarabu na Sultan wa Zanzibar.
P

 
Aliyeianzisha hiyo biashara ya utumwa Afrika Mashariki ni Mreno . Unataka kuniambia akimuuzia mwarabu??
Mateso makubwa kwa Watumwa, sio wakati wa biashara ya utumwa, bali baada ya biashara hii kupigwa marufuku.

Kwenye bandiko hili
https://www.jamiiforums.com/threads...nd the slave trade in Zanzibar, Pemba ...[/B]

Hiyo ndio ripoti ya madhila ya Watumwa chini ya utawala wa Sultani wa Zanzibar.
P
 
Mkuu Maalim Mohammed Said, bado unaweza kuandika historia ya kusahisha urongo wa historia zilizoandikwa kwa lengo la kuweka bayana mchango wa wazee wako bila kuwakweza unnecessarily na bila kuwadogosha wengine.

Mfano harakati za uhuru wa Tanganyika zimeanzia
AA, TAA na TANU, nikiamua kuzero in kwenye mashujaa viongozi waanzilishi, nitawataja mashujaa watatu tuu, Cecil Matola, Dr. Vedastus Kyaruzi na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!. Nilisema kina Sykes were nothing, I will still be right kwenye muktadha wa Wenyeviti waanzilishi ila nitakuwa nimewagogosha.

Nilisema nayasoma maandishi yako in between the lines na kuiibaini the ill motives behind baadhi ya hoja zako kutaka kumdogosha Mwalimu Nyerere na kuwakweza wazee wako!. Ukatumia urongo kuonyesha Mwalimu Nyerere hakulijua jiji hadi alipotambulishwa na wazee wako in 1950s, Mkuu Nguruvi3 akakuwekea data za ujio wa Mwalimu Nyerere kwenye mkutano Mkuu wa TAA mwaka 1948, ukakimbia.

Unaweza kuandika historia sawia bila kukweza wala kudogosha na bila kuongopa kwa kujazia vionjo vya maurongo.

Sasa kwenye hili la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, dunia nzima inaujua mchango wa John Okello, wewe kuibuka na kusema Okello sii lolote sii chochote ni kumdogosha.

Tunakueleza madhila ya babu zetu yaliyowakuta kwenye utumwa wa Waarabu na Sultan wa Zanzibar, wewe unataka tuzungumzie utumwa wa Trans Atlantic Slave Trade ili tuu kuudogosha utumwa wa Indian Ocean Slave Trade.

Historia ya kweli ya Zanzibar inaweza kuandikwa kwa ukweli huku ukiyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kutumia kibwagizo cha "Mapinduzi Daima" kwa kuyalaani mabaya na maovu ya Sultani wa Zanzibar kuhalalisha Mapinduzi at the same time na bado kuyaenzi mazuri ya Sultani.
P
Paschal,
Unaandika kwa kucharuka.

Sina tatizo ikiwa unaona akina Sykes "were nothing," lakini Kleist maisha yake yamo kwenye kitabu cha Iliffe (1973)na kitabu changu (1998)na katika Dictionary of African Biography (2011).

Huu hapo juu ni mukhtasari lakini kitabu cha maisha yake hii leo ndiyo kitabu kinachoaminika katika kujua kwa undani historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na katunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru na serikali ya Tanzania.

Mtu mwenye kadi ya TANU no. 3 na aliyempokea Nyerere na kumjulisha katika siasa za Dar es Salaam tena akiwa mfadhili kweli anaweza kuwa "nothing?"

Hakika mdomo haumkatai bwana wake.
 
Mtu mwenye kadi ya TANU no. 3 na aliyempokea Nyerere na kumjulisha katika siasa za Dar es Salaam tena akiwa mfadhili kweli anaweza kuwa "nothing?"
Everything is something and nothing due to the terms of measurements.

Nasema tena na kurudia, hata mara 100!, kama kigezo changu ni just No. 1 only, then kwa kigezo hicho, No. 1 kwa AA ni Cecil Matola, No. 1 kwa TAA ni Dr. Vedastus Kyaruzi na No. 1 kwa TANU ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, and everybody else is nothing!.

Hata nikipunguza vigezo nikaongeza idadi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi na Katibu Mkuu wa kwanza, utakuta hao wazee wako bado are no where to be seen, they are simply nothing ila kazi ni kuwakweza tuu!.

This kuwaita nothing, they are just nothing kwa vigezo hivyo, but in actual fact, they are not nothing, they might be everything kwenye mengine yote lakini kwenye Number 1 na 2, they are just nothing!.

The feeling you get when you hear someone ambaye kwako ni everything, halafu ukaambiwa, he is nothing, it's the feeling some of us get jinsi una m potray Mwalimu Nyerere, kwa kuwa elevate kina Sykes kuonyeshea they were everything na Nyarere was nothing compared hadi kutumia urongo kudanganya ndio wao walimtambulisha Mwalimu kwa Wazee wa Dar es Salaam ile 1950s wakati Mwalimu Nyerere amekaa na wazee hao tangu mwaka 1948!.

Sasa humu unasema kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, John Okello sii lolote sii chochote, wakati to some of us John Okello was everything thing kwenye Mapinduzi Matukufu yale.

Nasisitiza ule u nothing wa wazee wako ni kwa vigezo tuu, na sio kwa michango yao or the role they played, inawezekana kabisa yule wa kwanza did nothing, and the power behind ndio everything, lakini kama kigezo ni wa kwanza tuu, then wa kwanza ni wakwanza tuu na wazee wako hawajawahi kuwa kwanza, na kwasababu hii ni past events, and it's over, they will never be!.

P
 
Everything is something and nothing due to the terms of measurements.

Nasema tena na kurudia, hata mara 100!, kama kigezo changu ni just No. 1 only, then kwa kigezo hicho, No. 1 kwa AA ni Cecil Matola, No. 1 kwa TAA ni Dr. Vedastus Kyaruzi na No. 1 kwa TANU ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, and everybody else is nothing!.

Hata nikipunguza vigezo nikaongeza idadi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi na Katibu Mkuu wa kwanza, utakuta hao wazee wako bado are no where to be seen, they are simply nothing ila kazi ni kuwakweza tuu!.

This kuwaita nothing, they are just nothing kwa vigezo hivyo, but in actual fact, they are not nothing, they might be everything kwenye mengine yote lakini kwenye Number 1 na 2, they are just nothing!.

The feeling you get when you hear someone ambaye kwako ni everything, halafu ukaambiwa, he is nothing, it's the feeling some of us get jinsi una m potray Mwalimu Nyerere, kwa kuwa elevate kina Sykes kuonyeshea they were everything na Nyarere was nothing compared hadi kutumia urongo kudanganya ndio wao walimtambulisha Mwalimu kwa Wazee wa Dar es Salaam ile 1950s wakati Mwalimu Nyerere amekaa na wazee hao tangu mwaka 1948!.

Sasa humu unasema kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, John Okello sii lolote sii chochote, wakati to some of us John Okello was everything thing kwenye Mapinduzi Matukufu yale.

Nasisitiza una nothing wa wazee wako ni kwa vigezo tuu, na sio kwa michango yao or the role they played, inawezekana kabisa yule wa kwanza did nothing, and the power behind ndio everything, lakini kama kigezo ni wa kwanza tuu, then wa kwanza ni wakwanza tuu na wazee wako hawajawahi kuwa kwanza, na kwasababu hii ni past events, and it's over, they will never be!.

P
P,
Hapana shida yoyote unaweza kuandika lolote upendalo na huu ndiyo uhuru tuutakao.

Ikiwa mimi nitakukatalia wewe kusema ulijualo mimi nitakuwa na haki gani ya kuandika vitabu na vitabu niandikavyo vikachapwa na kusomwa?

Kuna wakati watu wakiogopa kuandika ukweli wanaoujua na ndiyo tukaangukia kwenye historia zilizokuwa na makosa.

Nakuunga mkono endelea kuandika na eleza uyajuayo katika historia ya TANU na mapinduzi ya Zanzibar.
 
Mateso makubwa kwa Watumwa, sio wakati wa biashara ya utumwa, bali baada ya biashara hii kupigwa marufuku.

Kwenye bandiko hili
nimeweka ripoti hii.
Hiyo ndio ripoti ya madhila ya Watumwa chini ya utawala wa Sultani wa Zanzibar.
P

Umeandika :

Mateso makubwa kwa Watumwa, sio wakati wa biashara ya utumwa, bali baada ya biashara hii kupigwa marufuku.

Majibu :

Unafiki Wa Wakomeshaji Wa Biashara Ya Watumwa

Kama mtu yeyote anataka kudhani kwamba sababu ya kukomeshwa kwa utumwa ni maendeleo ya unyofu wa maadili, basi anashauriwa kuangalia msimamo wa watu waliokuwa wanashughulikia suala la kukomesha biashara ya watumwa katika mfumo wa malengo yao ya kiuchumi.

Hivyo tunaona kwamba wale wale washikiliaji wa maslahi ya West Indies ambao kabla ya tatizo lililotajwa, walikuwa ni waungaji mkono motomoto wa biashara ya watumwa sasa waligeuka kuwa “waungwana wenye huruma na shauku ya kuukomesha utumwa”.

Dk. Williams anasema, kwa kejeli kabisa, ilikuwa ni wamiliki wa watumwa wa siku za nyuma wa West Indies ambao sasa walishikilia tochi ya kuwahurumia binadamu.

Wale ambao, katika mwaka wa 1807, kwa majonzi walikuwa wanatabiri kwamba kukomesha biashara ya watumwa ya Uingereza “ingesababisha kupungua kwa biashara, kupungua kwa ushuru wa kodi, na kupungua kwa safari za baharini; na hatimaye kudhoofisha na kuondoa kabisa msingi mkuu wa ustawi wa Uingereza, walikuwa, baada ya 1807, watu wale wale waliokataa ‘mpango wa mtu’ kuwaiba watu masikini na ambao hawana jinsi ya kujitetea.”

Manufaa ya West India katika mwaka wa 1830 yaliweka azimio la “kuchukua hatua madhubuti zaidi kusitisha biashara ya watumwa ya nje; kushughulikia suala la ukan- damizaji uliokwisha fanywa ambao kwamba ustawi wa makoloni ya Uingereza ya West Indes… hatimaye yali- utegemea.

Wajumbe kutoka Jamaica, walopelekwa Uingereza mwaka 1823, walitangaza kwamba makoloni yangepatanishwa kwa urahisi kuhusu kukomeshwa kwa biashara ya kishenzi na ya kinyama, ambayo ustaarabu ulioendelea wa wakati huu hukuiruhusu tena kuwepo… Kundi kubwa la kukomesha biashara ya watumwa lilijidhihirisha nchini Jamaica katika mwaka 1849.

Auj claplo, vyama na madhehebu viliunganishwa kuhusu suala la Africa kutendewa haki. Walilaani biashara ya watumwa na utumwa kama ni “kinyume cha ubinadamu iliyozalisha maovu mabaya sana Afrika - kuwadhalilisha wote waliohusika katika biashara hiyo, na kudhuru maadili na utashi wa kiroho wa watumwa, na kusihi kwamba neno la kuchuk- iza ‘mtumwa’ liondolewe kwenye msamiati duniani pote.

UTUMWA LAZIMA UANGUKE, na utakapoanguka, JAMAICA ITASTAWI! Walitamka kwa ukali, iliingia kwenye vita nyingi bila ya sababu zilizo halali.” 1

Na palikuwepo na manufaa gani ya vifungu vya maneno vilivyo vikali na ambavyo vinaweza kuamuliwa kutokana na ukweli kwamba ubepari wa Uingereza, hata baada ya kuvuruga utumwa wa West Indian, “Uliendelea kustawi kutokana na utumwa uliokuwa unaendelea huko Brazil, Cuba na utumwa wa Amerika ya Kaskazini na Kusini.”

Kwa hiyo, kwa maneno ya Profesa Brogan, “tunapata mafumbo ya wajibu uliogeuzwa. Ilikuwa sawa kabisa kwa watetezi wa hoja ya kukomeshwa utumwa, kulaani matumizi ya sukari iliyo zalishwa na watumwa kutoka West Indes, lakini hakuna aliyependekeza kusimamisha matumizi ya pamba iliyozalishwa kutoka Marekani (U.S.A.).

Hakika, hakuna mtu aliyependekeza kwa dhati kuacha kutumia sukari iliyozalishwa na watumwa kutoka Brazil au Cuba. Fedha sio hisia, hisia za uovu za uzuri, husokota na kupotosha njama.”

Dk. Williams anaandika, “Baada ya India, Brazil na Cuba, bila ya dhana yoyote. Je, muungwana yeyote angeweza kuhalalisha pendekezo lolote lililopangwa kuimarisha minyororo ya utumwa ambayo bado imewafunga Watu Weusi wa Brazil na Cuba. Kwa usahihi hiyo ndio ilikuwa maana ya biashara huru ya sukari.

Kwani baada ya mwaka 1807 British West Indians walikataliwa na kunyimwa kuendesha biashara ya watumwa, na baada ya 1833 wakanyimwa nguvu kazi ya watumwa. Kama watetezi wa kukomesha utumwa walipendekeza sukari ya kutoka India, kwa makosa, kwa misingi ya ubinadamu kwamba ni sukari iliyolimwa na watumwa huru, ilikuwa ni wajibu wao kwa kanuni zao na dini yao kususia sukari iliyolimwa na watu wa Brazil na Cuba. Katika kuanguka kufanya hivi isiamuliwe kwamba hawakuwa sahihi, lakini si jambo la kukanusha kwamba kushindwa kwao kutumia njia hiyo ilivuruga hoja ya ubinadamu.

Baada ya 1833, watetezi wa kukomesha utumwa, waliendelea kumpinga mkulima wa West Indian ambaye sasa aliajiri wafanya kazi huru. Ambapo, kabla ya hapo 1833, waliwagomea wamiliki wa watumwa wa Uingereza, baada ya 1833 waliunga mkono sababu ya wamiliki wa watumwa wa Brazil.”2

Kuondolewa kwa Watu Weusi kishenzi kutoka Afrika ni shughuli iliyoendelea kwa karibu miaka 25 tangu 1833, ambao walipelekwa kwenye mashamba ya miwa ya Brazil na Cuba. Uchumi wa Brazil na Cuba ulitegemea biashara ya watumwa. Msisitizo peke yake ulidai kwamba watetezi wa kukomesha utumwa wa Uingereza walipinga biashara hii.

Lakini jambo hilo lingerudisha nyuma maendeleo ya Brazil na Cuba na matokeo yake kuzuia biashara ya Uingereza. Haja ya kupata sukari ya gharama ya chini baada ya 1833 ilishinda chuki yote ya utumwa. Tishio ambalo hapo mwan- zo lilichochewa na fikira ya mswaga watumwa wa Uingereza wa West Indies mwenye mjeledi; mswaga watumwa wa Cuba mwenye mjeledi, panga, jambia,. kisu na bastola na kufuatwa na mbwa mwitu, haikuamsha hata maoni ya watetezi wa kuzuia biashara ya watumwa.”3

Hivyo ni wazi kwamba sababu halisi yaubinadamu na uungwana wa Uingereza wala haikuwa usawa wa kiunyofu au mwamko wa kimaadili bali ilikuwa ni kwa sababu ya shinikizo la kiuchumi na kuwaumiza washindani wao wa biashara.

Kwa maneno ya Profesa Brogan, somo la Ubepari na Utumwa linavunja moyo na kufadhaisha kama si jipya.

“Pale ilipo hazina yako ndipo moyo wako unapo lala.’
  • 1. Ibid, uk 175-6.
  • 2. Ibid, uk 188.
  • 3. Ibid, uk. 192.
 
Mateso makubwa kwa Watumwa, sio wakati wa biashara ya utumwa, bali baada ya biashara hii kupigwa marufuku.

Kwenye bandiko hili
nimeweka ripoti hii.
Hiyo ndio ripoti ya madhila ya Watumwa chini ya utawala wa Sultani wa Zanzibar.
P


PASCAL WACHA KUTULETEA PROPAGANDA ZA MAKANISA NA WAZUNGU


Uliweka picha hizi eti ndio waarabu walivyowatesa watumwa wa kiafrika


img-20160417-wa0025-jpg.339723


winterton_image_large.jpg



f1cfd5c8c022ec081b501e137cd76f48.jpg


0d422469a7bfe49699e19d8d898530d7.jpg


East-African-Slave-Trade.jpg



6ea26ffb39629355ebf88004858ec924.jpg


images


images


Slavezanzibar2.JPG


Servant_or_slave_woman_in_Mogadishu.jpg


8193f522fd2fbf34063d4baf59dfcced.jpg


Hizi picha wajemeni sio picha ya kuchorwa, ni picha za kweli na halisi zilizopigwa na kamera za wadhungu na sii lazima ziwe zimepigwa Zanzibar.


Pascal Utumwa ulipigwa marufuku mwaka 1833

Britain abolished slavery throughout its empire by the Slavery Abolition Act 1833 (with the notable exception of India), the French colonies re-abolished it in 1848 and the U.S. abolished slavery in 1865 with the 13th Amendment to the U.S. Constitution.
Abolitionism - Wikipedia


CAMERA ILIVUMBULIWA MWAKA 1888

1888

The use of photographic film was pioneered by George Eastman, who started manufacturing paper film in 1885 before switching to celluloid in 1888–1889. His first camera, which he called the "Kodak", was first offered for sale in 1888.
History of the camera - Wikipedia


HIZO PICHA ULIZOLETA ZILIPIGWA NA CAMERA IPI ??


BADO TU MNAENDELEZA HIZI PROPAGANDA NA CHUKI DHIDI YA WAARABU NA WAISLAMU ?? HASA HUKU KWETU ZANZIBAR


NJIA YA MWONGO NI FUPI
 
Mateso makubwa kwa Watumwa, sio wakati wa biashara ya utumwa, bali baada ya biashara hii kupigwa marufuku.

Kwenye bandiko hili
nimeweka ripoti hii.
Hiyo ndio ripoti ya madhila ya Watumwa chini ya utawala wa Sultani wa Zanzibar.
P


Kwa Nini Utumwa Ulikomeshwa.

Mtu anaweza akasema: “Hivi haikuwa Uingereza ya Kikristo hatimaye ndio iliyo komesha utumwa? Vema, kama mtu anafanya udhalimu si yeye ndiye anayetakiwa kuendeleza udhalimu huo?

Kama ambavyo imekwisha elezewa, Uingereza ilikuwa ndio mfanya bishara ya watumwa mkub- wa zaidi ya wote, na nguvu za kiuchumi zilipoilazimisha kukomesha biashara ya watumwa, ilifanya hivyo. Je! ni Uingereza inayostahili au Ukristo ndiyo unastahili kupewa shukurani zozote kwa tukio hilo? Kwa nini tusizishukuru nguvu za uchumi ambazo ndizo zililazimisha Uingereza kutokuendelea na biashara hiyo?

Ukweli ni kwamba harakati dhidi ya utumwa hazikuongozwa na makanisa; kazi hiyo ilifanywa na watu waadilifu wachache ambao vilio vyao vilikuwa havisikilizwi hadi pale umuhimu wa kiuchumi ulipolazimisha Bunge kupitisha muswada mnamo mwaka wa 1870 dhidi ya biashara ya watumwa.

Baada ya miaka 26, muswada mwingine ulipitishwa kukomesha utumwa katika makoloni ya Uingereza mnamo mwaka 1833. Kama Profesa D.W. Brogan alivyoandika kwenye utangulizi wa kitabu cha Dk. Eric Williams ambacho ni kizuri, kiitwacho “Capitalism and Slavery”,

“Kukomeshwa kwa biashara ya utumwa halafu kusitishwa kwa utumwa, hayakuwa tu matokeo ya kuboreka kwa kiwango cha mfumo wa maadili ya kisiasa humo Uingereza (ingawaje Dk. Williams hadharau kazi ya watu kama Clarkson kuwa ina umuhimu) lakini ilikuwa namna ya kupunguza hasara.

Ukiritimba wa kilimo cha miwa cha visiwa vya West Indies haukuvumilika kulinganishwa na jamii ya viwanda iliyokuwa inastawi haraka, yenye kujiamini kwa usahihi katika nafasi yake ya ushindani isio tetereka mnamo siku za mwanzo za mageuzi ya viwanda. “Kufupisha, kwa maneno ya Profesa Brogan, mpango wa utumwa ulikuwa “unavumiliwa, unatetewa, unasifiwa almuradi ulikuwa na faida.”

“Mpango wa mtumwa ulikuwa na faida sana na kwa kipindi kirefu. Mafanikio ya Bristol na Liverpool na kwa kiwan- go fulani, ya Glasgow yalitegemea faida ya mashamba ya miwa ya visiwa vya West Indies. Mkulima wa West Indies alikuwa mshindani wa ufahari wa tajiri mpenda anasa wa East Indies.

Ilikuwa kama kupoteza muda kwa waadilifu kuonyesha kwamba kila tofali lililojenga maghala makubwa ya Bristol na Liverpool lilitokana na damu ya Mtu Mweusi.

Lakini sauti ya waadilifu ilisikika mara chache sana miongoni mwa mlio wa sarafu ya Uingereza Guine (jina hilo hilo linakumbusha biashara ya pembetatu baina ya Uingereza, Afrika na makoloni ya transatlantic).”

“Biashara ya pembe tatu” maana yake ni nini? Kutoka Uingereza, bidhaa mchanganyiko “mfano halisi wa mzigo wa mfanya biashara ya watumwa” ulipelekwa Africa.

Mavazi mazuri na umalidadi kwa Waafrika, vyombo vya nyumbani, nguo za kila aina, chuma na metali, pamoja na bunduki, pingu na minyororo.” Kutoka Afrika mzigo wa binadamu ulichukuliwa kupelekwa visiwa vya West Indies na nchi za Amerika.

Kutoka West Indes na makoloni mengine; sukari, tumbaku na rangi ya buluu, pamba, kahawa na malighafi zingine zilipelekwa nchi mama (yaani Uingereza) ambako yalitengenezwa kwenye viwanda na halafu yakaingizwa tena kwenye makoloni.1

Mashamba yalianzishwa kwa sababu ya kuwepo nguvu kazi ya utumwa na yakalindwa na ukiritimba. Halafu ukaja mtengano wa makoloni 13 ya Marekani ambayo yalifunga soko kubwa dhidi ya nchi iliyohuru makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West Indies.

Athari yake nyingine ilikuwa kwamba nchi iliyo huru sasa, ya Marekani (U.S.A.) iligeuka kwenye makoloni ya Ufaransa yaani Visiwa vya Saint Domingue (Haiti), Cuba na Brazil. Dk. Williams anaandika, “Ubora wa makoloni ya sukari ya Ufaransa ulikuwa kwa ajili ya wakulima wa Kiingereza, kubwa miongoni mwa maovu mengi ambayo yalijitokeza nje kutoka kwenye Pandora’s box**. (sanduku la Pandora) ilikuwa ni mapinduzi ya Marekani.

Kati ya mwaka 1783 na 1789 maendeleo ya sukari ya visiwa hususan vya Ufaransa, vya Saint Domingo (Haiti), hususan lilikuwa jambo la kushangaza katika maendeleo ya kikoloni. Rutuba ya udongo wa makoloni ya Ufaransa ilikuwa ni ya wazi mno, sukari ya Ufaransa iligharimu moja ya tano (1/5) chini zaidi ya ile ya Uingereza, mavuno ya wastani huko Saint Domingo na Jamaica yalikuwa tano kwa moja.”2

Athari iliyosababisha maafa kwenye makoloni ya Uingereza ya West Indies inaweza kuamuliwa na ukweli kwamba “mwaka 1775 Jamaica ilikuwa na mashamba 775; hadi kufika 1791, katika kila mashamba mia moja, mashamba ishirini na tatu yaliuzwa kwa ajili ya kulipa, kumi na mbili yalikuwa kwenye miliki ya wafilisi, wakati saba yaliachwa; na wakulima wa West Indies, wakiwa na deni la kiasi cha pauni milioni ishirini.”

Polepole, wakulima wa Kiingereza walipoteza moja kwa moja mamlaka yao ambayo waliyafurahia kwa kipindi kirefu katika soko la Ulaya. “Uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Ufaransa, uliingiza pauni za Kiingereza zaidi ya milioni nane, na Uingizaji bidhaa ndani ya nchi, zaidi ya pauni milioni nne, tani zilizo shughulikiwa 164,000 na wafanya kazi wa meli 33,600; uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Uingereza uliingiza pauni za Kiingereza milioni tano, na uingizaji bidhaa ndani ya nchi chini ya milioni mbili, tani zilizo shughulikiwa, 148,000 na wafanya kazi wa meli 14,000.

Katika hali zote makoloni ya sukari yalikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa Ufaransa kuliko yalivyokuwa kwa Uingereza.”3

Hivyo, gharama ya sukari (na hivyo hivyo kwa bidhaa zingine zote.) ilianza kwenda juu sana.

Dk. Williams anaeleza, “Ukiritimba wa mkulima wa West Indies haukuwa tu jambo lisilofaa kinadharia, haukuwa na faida katika hali halisi. Mnamo mwaka 1828 ilikisiwa kwamba iliwagharimu raia wa Uingereza zaidi ya pauni milioni moja na nusu kwa mwaka.

Mnamo mwaka 1844, ulikuwa unagharimu nchi pauni 70,000 kwa juma moja na jiji la London peke yake pauni 6,000. Uingereza ilikuwa inalipa zaidi ya pauni milioni tano kwa ajili ya sukari yake kwa mwaka kuliko Bara lota la Ulaya… Mbili ya tano (2/5) ya bei ya ratili moja ya sukari iliyotumiwa Uingereza iliwaisha gharama ya uzalishaji, Mbili ya tano (2/5) ilichukuliwa kama ushuru wa serikali, moja ya tano (1/5) shukurani kwa mkulia wa West-Indies…4

Pole pole, Saint Domingue (Haiti) koloni la Ufaransa, lili- ibuka kama mzalishaji muhimu sana wa sukari. Kwa mtazamo wa Waziri Mkuu wa Uingereza, William Pitt, hili lilikuwa jambo lenye uamuzi. Umri wa visiwa vya Uingereza vya sukari ulifika mwisho. Mpango wa West- Indian haukuwa na faida, na biashara ya watumwa ambayo ndio ilikuwa tegemeo lake, badala ya kuwa na manufaa kwa Great Britain… ni ya uharibifu mno ikilinganishwa na dhana ya maslahi.5

Kwa hiyo, Pitt aligeukia India kulima na kuzalisha sukari. Mpango wa Pitt ulikuwa na sehemu mbili: kurejesha soko la Ulaya kwa msaada wa sukari kutoka India, na kupata fursa ya kukomesha biasharra ya watumwa kimataifa tukio ambalo lingeiangamiza Saint Domingue. Kama haingekuwa ukomeshaji wa Uingereza.

Wafaransa waliwategemea sana wafanyabiashara ya watumwa wa kimataifa, basi ingekuwa ukomeshaji wa Uingereza hivyo kwamba hata kama Uingereza peke yake ingepiga marukufu biashara ya watumwa, uchumi wa makoloni ya Ufaransa ungetetereka.

“Mpango wa Pitt ulishindwa kwa sababu mbili. Umuhimi wa sukari ya kutoka India ya Mashariki, kwa kiwango kilichopangwa, haingewezekana kwa sabahu ya kodi ya ushuru kuwa juu iliyowekwa kwa sukari yote isipokuwa ile iliyozalishwa kwenye makoloni ya Uingereza ya West-Indies… Pili, Wafaransa, Wadachi na Wahispania walikataa kukomesha biashara ya utumwa.

Ilikuwa rahisi kuona malengo halisi ya kisiasa yaliyoko nyuma ya pazia la ubinadamu la Pitt. Gaston-Martin, Mfaransa maarufu mwenye taaluma ya historia ya biashara ya watumwa na makoloni ya Caribbean, anamlaumu Pitt kwa kutaka kuwapa uhuru watumwa kwa kutumia propaganda, hapan shaka kwa kutumia jina la ubinadamu. lakini pia kuharibu biashara ya Ufaransa. Na anahitimisha kwamba kwenye propaganda hii ya kiihsani na kiubinadamu palikuwepo na malengo ya kiuchumi.

Halafu pakatokea tukio moja kubwa. Wakulima wa Kifaransa huko Saint Domingo, mwaka 1791, wakihofia matokeo ya Mapinduzi ya Ufaransa, waliwapa Uingereza visiwa hivyo; muda si mrefu Windward Island ilifuata mtindo huo; Pitt alikubali kuvichukua visiwa hivyo mwaka wa 1793. Vikosi vya jeshi la Ufaransa vilipelekwa kimoja baada ya kingine mara kadhaa lakini havikufanikiwa kuvirejesha visiwa hivyo kwenye miliki ya Ufaransa.

Dk. William anafafanua: “Hii ni zaidi ya manufaa ya kiso- mi. Pitt hangeweza kumiliki Saint Domingo na kukomesha biashara ya watumwa wakati huo huo. Bila ya kawaida yake ya kuingiza watumwa 40.000 kwa mwaka, Saint Domingo ingekwisha filisika. Kitendo cha Pitt kukubalia kuchukua kisiwa hicho kimantiki kilikuwa na maana kwamba hangeendelea na mpango wake wa kukomesha biashara ya watumwa. Kwa wazi hakusema hivyo. Pitt alikwisha fika mbali sana katika kuwaahidi raia wa Uingereza.

Aliendelea kuzungumza kuhusu kukomesha biashara ya watumwa hata hapo alipokuwa anaitumainisha biashara ya watumwa katika hali halisi… Sababu za Pitt zilikuwa za kisiasa na kwa kiwango kidogo kibinafsi. Pitt alipendelea biashara ya sukari: Ama ilikuwa lazima aivuruge Saint Domingo kwa kuingiza sukari nyingi sana Ulaya na ya bei rahisi kutoka India au kwa kukomesha biashara ya watumwa; au aichukue Saint Domingo iwe yake binafsi.”6

Hali hii ingeipatia Uingereza ukiritimba wa sukari, rangi ya buluu, pamba na kahawa… Lakini kama Pitt angeikamata Saint Domingo, biashara ya watumwa lazima ingeendelea. Wakati Saint Domingo ilipochukuliwa na Ufaransa, biashara ya watumwa ilichukua sura mpya ya kuwa kama vile suala la ubinadamu tu…

Lakini kuharibika kwa Saint Domingo haikuwa na maana ya ukombozi kwa makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West- Indies. Walijitokeza maadui wawili wapya kwenye uwanja. Cuba ilisonga mbele na kuziba pengo lililoachwa kwenye soko la dunia baada ya kutoweka Saint Domingo.”7

Wakati ule ule, chini ya mamlaka ya Marekani, sukari ya Cuba na wazalishaji wengine waliokuwa na msimamo wa kati, bado ilipata soko Ulaya, na sukari ya ziada kutoka British West Indian ililundikana Uingereza. Kufilisika kwa wakulima ilikuwa hali ya kawaida. Kati ya 1799 hadi 1807, mashamba 65 ya Jamaica yaliachwa, 32 yaliuzwa kufuta madeni, na malalamiko 1807 ya madai yalikuwa yana ngoja uamuzi dhidi ya 115. Mada zilizokuwa zinazungumziwa hapo kisiwani ni madeni, maradhi na vifo.

Kamati ya bunge iliyoundwa mwaka 1807 iligundua kwamba mkulima wa British Indian alikuwa anazalisha kwa hasara. Mwaka wa1800 faida ya mkulima ilikuwa asilimia 2.5 (2 ½ %), mwaka wa 1807 hakuna faida. Mwaka wa 1787 mkulima alipata 19/6d. Faida kwa kila ratili mia na kumi na mbili; mwaka 1799, 10/9d; mwaka wa 1803, 18/6d; 1805, 12/-; katika kwaka 1809, hasara.

Kamati ilidhani sababu kubwa ilikuwa hali mbaya ya soko la nje. Mwaka 1809 sukari ya ziada ya Uingereza ilikuwa tani 6,000. Uzalishaji ukasitishwa. Kuwekea mipaka uzalishaji, biashara ya watumwa lazima ikomeshwe.” 8
Kwa hiyo, kwa maneno ya Dk. Williams, “Kukomeshwa kwa biashara ya watumwa moja kwa moja ilisababishwa na kuvurugika kwa uchumi huo.”9

  • 1. Williams, Dr. Eric. Capitalism and Slavery uk. 65.
    ** Pandora box ni maneno ya methali, maana yake ni mpango ambao ukihamasishwa
    huzalisha matatizo mengi yasiyodhibitika.
  • 2. Ibid, uk. 122.
  • 3. Ibid, uk. 123
  • 4. Ibid, uk. 138-9.
  • 5. Ibid, uk. 146.
  • 6. Ibid uk. 146 -7, Ibid uk. 1487- 8.
  • 7. Ibid, uk. 148-9.
  • 8. Ibid, uk 149.
  • 9. Ibid, uk 150.
 
PASCAL WACHA KUTULETEA PROPAGANDA ZA MAKANISA NA WAZUNGU
Uliweka picha hizi eti ndio waarabu walivyowatesa watumwa

Hizi picha wajemeni sio picha ya kuchorwa, ni picha za kweli na halisi zilizopigwa na kamera za wadhungu na sii lazima ziwe zimepigwa Zanzibar.
Pascal Utumwa ulipigwa marufuku mwaka 1833

Britain abolished slavery throughout its empire by the Slavery Abolition Act 1833 (with the notable exception of India), the French colonies re-abolished it in 1848 and the U.S. abolished slavery in 1865 with the 13th Amendment to the U.S. Constitution.
Abolitionism - Wikipedia


CAMERA ILIVUMBULIWA MWAKA 1888

1888

The use of photographic film was pioneered by George Eastman, who started manufacturing paper film in 1885 before switching to celluloid in 1888–1889. His first camera, which he called the "Kodak", was first offered for sale in 1888.
History of the camera - Wikipedia

HIZO PICHA ULIZOLETA ZILIPIGWA NA CAMERA IPI ??

BADO TU MNAENDELEZA HIZI PROPAGANDA NA CHUKI DHIDI YA WAARABU NA WAISLAMU ?? HASA HUKU KWETU ZANZIBAR

NJIA YA MWONGO NI FUPI
Mkuu Gavana, kwanza usilete maurongo humu, picha za kamera zimeanza kupigwa 1826, na sio 1888, usichangaye mambo ya kuanzishwa kwa kampuni ya Kodak Eastman na kuanza kwa kamera.

Kuona ni kuamini, seeing is believing. Hizo ni picha kweli za kupigwa na camera ya mzungu na sio za kuchorwa!, na zimepigwa baada ya biashara ya utumwa kupigwa marufuku. Badala ya wewe kuingia huruma kwa mateso ya babu zetu Watumwa dhidi ya Waarabu madhalimu, wewe unazungumzia picha?!.

Nimekuekeza mateso makubwa waliyapata baada ya biashara ya utumwa kupigwa marufuku.

Kwanini tuandikie mate na hali wino upo?.
Fungua document hii uisome kwa kituo

Hii ni Ripoti ya aliyetumwa na utawala wa Waingereza kufuatilia kilichokuwa kinafanywa na serikali dhalimu ya Sultan, baada ya kupigwa marufuku biashara ya utumwa.

Pitia hapa: A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba ...

Na kwa vile wengi wetu ni wavivu, hatupendi kusoma kujiongezea maarifa bali tunapenda kupikiwa, kupakuliwa, kulishwa, kutafuniwa, sisi kazi yetu ibaki ni kumeza tuu, hivyo na mimi nitawatafunia sehemu chache chache za ripoti hii na kuzitafasiri kwa ajili ya wale wenzangu na mimi.

"They complained that the Arabs treated them harshly", yaani Waarabu wanawatesa.

In Zanzibar a good many people had been telling me how slaves were suffering in the hands of Arabs!. At Chaki Chaki I walked into a tumble-down I found a number of slaves male and female, heavily chained and fettered". Nilikuta makundi ya watumwa wake kwa waume wamefungwa minyororo!"

Lengo sio ubaguzi, au kuwakumbusha machungu ya Waarabu, bali ni kujikumbusha tuu historia na kuwaelimisha baadhi ya wenzetu, wasiowajua hawa Waarabu wa Unguja na Pemba waliwafanya nini mababu zetu!.

Ila pia naomba kutoa Maangalizo muhimu yafuatayo:

1. Tuwe makini sana na watu waliofilisika kiakili ambao watachanganya Uarabu na dini ya Kiislam simply because, Dini ya Kiislamu inatumia lugha ya Kiarabu!. Masikini muflisi hawa, hawajui kuwa hata Ukiristo umeanzia Arabuni. Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail, aliyezaa na mjakazi wa ki Misri, na Wakristo ni uzao wa Isaka aliyezaa na mkewe Sara. Hata Yesu Kristo, licha ya kuzaliwa Israel, alikulia Misri na alizungumza lugha ya Kiarabu!. Hapa mimi nazungumzia udhalimu wa Waarabu kama jamii na sio dini ya Kiislamu.

Udhalimu ni udhalimu tuu hauna dini, wala kabila, wala jamii, kwa sababu kwenye udhalimu sio Waarabu tuu peke yao ndio madhalimu, watu wa mataifa mbalimbali wamefanya udhalimu kwa watu wa mataifa mengine, na mfano mzuri ni udhalimu wa Wajerumani kwa Mayahudi chini ya Hitler ulioitwa Halocust ambapo Hitler aliwaua Wayahudi zaidi ya milioni 6 kwa ukatili wa ajabu!, ila kwenye biashara ya Utumwa Unguja, Pemba, na Arabuni, watumwa hawa walihasiwa hivyo kufanyiwa genoside na wahusika sii wengine bali ndugu hawa hawa ndugu zetu Waarabu ambao leo tunakula nao, tunakunywa nao na kufurahi nao kwa vile tumeisha samehe na tumeishasahau, yaliyopita sii ndwele.

2. Kwenye biashara ya utumwa, waliokuwa wakikamata watumwa, sio Waarabu, Waarabu wao walikuwa ni wafanyabiashara ya watumwa kwenye soko kuu la watumwa la Zanzibar, wakitokea Bagamoyo, na wanunuzi wakuu wa watumwa toka soko la Zanzibar kwa ajili ya kuwasafirisha kuwauza Uarabuni na India, ambako kote huko baada ya kufika, watumwa wanaume walihasiwa!. Waarabu pia ndio walikuwa wamiliki wa watumwa katika mashamba ya Zanzibar na`Pemba, ambapo nako watumwa wanaume walihasiwa, wanawake walifanywa vijakazi na ndio wazazi wa machotara wa Zanzibar na Pemba, wengi ni baba Mwarabu, mama uzao wa watumwa wanawake wenye bahati, ambao hawakutumbuliwa mimba za Waarabu!

Upatikanaji wa watumwa kutoka bara pia ulihusisha baadhi ya watawala wetu wa asili wakiwemo machifu ambapo baadhi ya wahalifu waliostahili adhabu za vifo katika jamii zao, badala ya kuuliwa na kuwa hasara jumla, waliuzwa, utumwani, lakini watumwa wengi ni watu tuu wa kawaida wasio na hatia yoyote ambao waliwamiwa na kukamatwa kwa nguvu, wakiwemo wanawake na watoto!. Zoezi la ukamataji watumwa pia lilihusisha vitendo vya ukatili, ambapo wengi watumwa hawa, waliuawawa katika purukushani, na wengine wengi walifia njiani na miili yao kuachwa ikioza, miili yenye bahati ilifanywa vitoweo vya wanyama wa porini.

Kwenye misafara hiyo, ndugu zetu waliteswa sana mateso ambayo hayazungumziki walioishiwa nguvu, walipigwa hadi kifo ila hakukuwepo na kamera ya mzungu wa kutupigia picha kuja kutuleta humu!.

3. Waarabu ninaowazungumza hapa, ni wale Waarabu madhalimu na makatili wa enzi zile za utumwa ambao wengi wao, mwaka 1964, walifurushwa kutoka Unguja kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964!, ila waliofurushwa ni wale tuu waliokuwa Zanzibar tu, lakini waliokuwa Pemba hawakuguswa.

Hawa Waarabu wa leo, ni vizalia vya Waarabu wale wale, ila hawa wa sasa, ni Waarabu wema, wastaarabu kama Waarabu wa sasa, wenye roho nzuri, sio wakatili, sio wadhalimu na wanawapenda watu weusi na kuwaoa kwa mapenzi, huku wanawake wao, wakiwapenda weusi na wakiolewa nao japo mwanzo ilikuwa ni kwa kulazimishwa na Karume, hivyo nashauri, kwa siku zijazo, hata Waarabu hawa, ama machotaa wao, wakishiriki tena uchaguzi, wakashinda kwenye uchaguzi huru na wa haki, wapewe tuu nchi watawale kwa sababu Waarabu hawa sii wale, wasinyimwe kutawala eti kwa sababu tuu ni Waarabu.

Waarabu wa enzi za utumwa, walikuwa madhalimu, hivyo kuendelea kudhani hata hawa wazaliwa wao pia ni lazima watakuwa ni madhalimu!, kwa kanuni ya mwana wa nyoka ni nyoka!, hivyo wanashinda uchaguzi lakini hawapewi, sio kuwatendea haki.

Japo mwana wa nyoka nyoka lakini si lazima kila mwana wa nyoka awe ni nyoka mwenye sumu kali, nyoka wengine ni kama joka la mdimu, halina madhara, hivyo Waarabu hawa wa leo wamebadilika, kwa sababu hata shetani mwanzo alikuwa malaika, hivyo Waarabu hawa wa sasa ni Waarabu wema, ni wenzetu na ni sehemu yetu, ukifanyika uchaguzi tena, wakishinda, wapewe tu nchi.

P
 
Mkuu Gavana, kuona ni kwanini, seeing is believing. Hizo ni picha kweli za kupigwa na camera ya mzungu na sio za kuchorwa. Badala ya kuingia huruma kwa mateso ya babu zetu Watumwa dhidi ya Waarabu madhalimu, wewe unazungumzia picha?!.

Nimekuekeza mateso makubwa waliyapata baada ya biashara ya utumwa kupigwa marufuku.

Kwanini tuandikie mate na hali wino upo?.
Fungua document hii uisome kwa kituo

Hii ni Ripoti ya aliyetumwa na utawala wa Waingereza kufuatilia kilichokuwa kinafanywa na serikali dhalimu ya Sultan, baada ya kupigwa marufuku biashara ya utumwa.

Pitia hapa: A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba ...

Na kwa vile wengi wetu ni wavivu, hatupendi kusoma kujiongezea maarifa bali tunapenda kupikiwa, kupakuliwa, kulishwa, kutafuniwa, sisi kazi yetu ibaki ni kumeza tuu, hivyo na mimi nitawatafunia sehemu chache chache za ripoti hii na kuzitafasiri kwa ajili ya wale wenzangu na mimi.

"They complained that the Arabs treated them harshly", yaani Waarabu wanawatesa.

In Zanzibar a good many people had been telling me how slaves were suffering in the hands of Arabs!. At Chaki Chaki I walked into a tumble-down I found a number of slaves male and female, heavily chained and fettered". Nilikuta makundi ya watumwa wake kwa waume wamefungwa minyororo!"

P

Utaniambia kitu gani na muingereza huyo ndiye aliyepigana vita na waislamu Zanzibar kumkamata mfalme na kumpeleka uhamishoni na kumweka mfalme amtakaye? na kuipeleka Zanzibar Tanganyika?

Umeona propaganda zenu na hujaniambia camera gani ilipiga picha ulizotuma wakati utumwa ulikwisha pigwa marufuku 1833. Camera ikavumbuliwa 1888??
 
Utaniambia kitu gani na muingereza huyo ndiye aliyepigana vita na waislamu Zanzibar kumkamata mfalme na kumpeleka uhamishoni na kumweka mfalme amtakaye? na kuipeleka Zanzibar Tanganyika?

Umeona propaganda zenu na hujaniambia camera gani ilipiga picha ulizotuma wakati utumwa ulikwisha pigwa marufuku 1833. Camera ikavumbuliwa 1888??
Tatizo lako Mkuu Gavana, ni uvivu wa kusoma!, au lugha?.

Pitia hapa: A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba ...

Nimekueleza na nina kueleza tena, madhila haya ni baada ya kukomeshwa kwa biashara ya utumwa, Zanzibar iliendelea kwa siri kwa miaka mingi baadaye hadi Missionary walipowagomboa Watumwa kwa kuwalipa waliowanunua, na ndipo lile soko kuu la Watumwa Mkunazini lilipofungwa na kujengwa kanisa.

P.
 
Unajipotezea heshima mkuu kwa ukereketwa.

Ulipata wapi hiyo imani ya kuwa alikua ni everything? au kanisani?
Tafuta andiko lolote kuhusu Zanzibar Revolution ambapo Okello hajatajwa kama kiongozi wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar.
John Okello was everything kwenye Mapinduzi Matukufu yale who was reduced to nothing.
P
 
Naunga mkono hoja, tena ni afadhali humu jf anafanya kuandika tuu, hivyo there is a room ya kumkosoa anapoleta maurongo humu, lakini anapokaribishwa kwenye redio zao, urongo wake huenea bila room ya critics, wasikilizaji wake wanameza mazima maxima, hivyo nimeishawahi kutoa angalizo hili kumhusu mtu huyu


P
Sure mkuu pasco nilipata kuona CD take moja watu alivyowapa sumu hadi wamebadilika. Huyu mzee namfananisha na yule shehe aliyekuwa akisapoti mauaji mwanza somebody ilunga
 
Tatizo lako Mkuu Gavana, ni uvivu wa kusoma!, au lugha?.
Mkuu Pasco , Gavana anajtahidi sana kupotosha umma ima kwa kujua au kutojua au kutotaka kujua.

Katika upotoshaji huo amefanikiwa kuwaburuza watu kama MS atika mkondo usio sahihi.

MS aliwahi kuhoji kwamba picha za watumwa ni za kuchora.

Hakuhoji kwavile hakuona hizo picha bali kuna hoja aliyosikia na bila utafiti au fikra au kwavile anaamini tu historia yake akaamua kutumbukiza hoja hiyo.

Yaani ana question picha za biashara ya utumwa! kama afanyavyo Gavana

Sasa nimeelewa ni kwanini baada ya kumsoma Gavana akikazani kuhusu uvumbuzi wa camera mwaka 1888 ikilinganishwa na picha za biashara ya utumwa kabla ya hapo

Naomba niweke sawa kwanza, kwamba, watu kama MS na Gavana wanadhani kitu kama computer kimegunduliwa na Bill Gate au hakikuwepo miaka 100 iliyopita

Idea ya computation ilianza kutumika kwa slide rule na algorithm karne nyingi (kuanzia 1625?) kama sikosei.

Wakati wa industrial revolution, mashine zilikuwa zinafanya kazi kwa mfumo wa computer

Kilichofuata ni kuendeleza matumizi ya computer katika maeneo kama majeshi halafu maofisini.

Akina Bill Gates wamerahisisha kazi kwa software lakini si wagunduzi

Kuhusu Camera wazo la kwanza lilitolewa na mtu wa Iraq Haytham miaka 800 kabla ya Camera

Kilichofuata ni akina Johann Zahn Mjerumani akifuatiwa na Mfaransa Nicephore aliyepiga picha ya kwanza 1826

Katika mwendelezo wa improvement wapo akina Alexander n.k.
Kamera ya kwanza ilikuwa pinhole, zikaja za lens halafu colloidal na mwisho digital

Gavana anachanganyikiwa au anauchanganya umma kwamba Camera imevumbuliwa mwaka 1888.

Kilichotokea wakati huo ni Mmarekani Eastman kuwa na kampuni iliyoanza kutoa jina la Camera na brand zake zikawa ni Kodak.
Alichokifanya Eastman ni ku commercialize kamera.

Hivyo basi Gavana anaposema Camera imegunduliwa mwaka 1888 ni kutoelewa, kutotaka kusoma. Hayo yanafanyika kwa makusudi kabisa ili kuzima hoja zilizopo mbele kwasasa kuhusu mambo kadhaa.

1. Gavana kama Mohamed Said wanaturudisha wanakotaka. Tumewaambia dhahir shahir kuwa Biashara ya utumwa ni ukatili dhidi ya binadamu uwe umefanywa na Mzungu, Mwarabu, Askofu au Sheik. Ni ushenzi tu usioweza kutetewa na mtu anayefikri sawa sawa.

2. Kwa upande wetu biashara ya Uarabuni ili tuathiri sana kwani tulikuwa ndio Wahanga.
Unyama huo ulifanywa kupitia soko la watumwa la Mkunazini chini ya Sultan.
Hivyo sultan wa Zanzibar ni ''accomplice'' katika unyama huo iwe kabla au baada. Period

Kuna hoja zinazomhusu Mohamed Said, hizo zinafuata. Hakuna namna lazima tuwekane sawa kwa muda mrefu jukwaa hili limegeuzwa jamvi la msibani kila atakaye afanya ajuavyo.
 
Mohamed Said tafadhali rejea bandiko#132 kipengele cha Hanga ulicholalamikia
Nilifanya editing nahisi ulinukuu baada tu ya bandiko

Pamoja na hayo umetueleza baba yako aliondoa picha, hivyo kulikuwa na mahusiano makubwa

Ukasema Hanga alikuwa akicheza bao na wazee wako wa Dar.

Hayo tuyaache yasituondoe katika mstari na wala kuingiza mengine kama bandiko# 136 ambalo sijui hata linahusiana vipi na hoja zilizoainishwa hapo awali zinasoburi hoja zako pia

Hoja hizo ni kama ifuatavyo;
1. Picha ya Okello ilipigwa lini, wapi ,na hao aliokaa nao ni akina nani kwa majina

2. Mzanzibar ''khalisi'' ana haiba, wasifu au sifa gani tofauti na mzanzibar mwingine

4. Abdallah Kassim Hanga ndiye alipanga mapinduzi kwa mujibu wako.
Je, ni Hanga ndiye aliyehusika na kupeleka mamluki wa Kimakonde kutoka Kipumbwi

5.Ikiwa Hanga aliandaa mapinduzi, je,wanaosema mapinduzi daima wapo sahihi au wanakosea

6. Ikiwa Hanga ndiye aliye andaa mapinduzi wazee wako wa Dar ambao ni maswahiba wa Hanga katika kucheza bao na maongezi walijua mpango huo?

7. Ikiwa Okello alikuwa si lolote si chochote, dhima ya kutangaza mapinduzi alipewa kwa minajili gani na kwanini akina Hanga hawakwenda kutangaza wao

8. Nani mwenyekiti wa kwanza wa baraza la mapinduzi na wajumbe walikuwa akina nani


Hizi ndizo hoja zilizopo mbele yetu, tukimaliza tutaweza kupata picha halisi ya mapinduzi

Pascal Mayalla Mag3 JokaKuu
Mohamed Said, hoja hizo zinakusubiri

Kuna sababu nzuri tu kwanini unahitajika. Umeleta picha ya Okello ukatoa challenge kwamba mtu aeleze miongoni mwa washirika aliokaa nao ni yupi '' Mzanzibar Khalisi''

Tueleze picha ilipigwa lini na wapi. Mzanzibar halisi ana wajihi au wasifu gani tofauti na Mzanzibar mwingine.

Halafu malizia na hoja nyingine 6
 
Mohamed Said, hoja hizo zinakusubiri

Kuna sababu nzuri tu kwanini unahitajika. Umeleta picha ya Okello ukatoa challenge kwamba mtu aeleze miongoni mwa washirika aliokaa nao ni yupi '' Mzanzibar Khalisi''

Tueleze picha ilipigwa lini na wapi. Mzanzibar halisi ana wajihi au wasifu gani tofauti na Mzanzibar mwingine.

Halafu malizia na hoja nyingine 6
Nguruvi 3,
Mimi huwa sishinikizwi.
Hupenda kufanya mjadala wa kistaarabu.

Wala sioni shida kujibu swali lolote kwani kama sijui nitakwambia.
 
Mkuu Pasco , Gavana anajtahidi sana kupotosha umma ima kwa kujua au kutojua au kutotaka kujua.

1. Gavana kama Mohamed Said wanaturudisha wanakotaka. Tumewaambia dhahir shahir kuwa Biashara ya utumwa ni ukatili dhidi ya binadamu uwe umefanywa na Mzungu, Mwarabu, Askofu au Sheik. Ni ushenzi tu usioweza kutetewa na mtu anayefikri sawa sawa.

2. Kwa upande wetu biashara ya Uarabuni ili tuathiri sana kwani tulikuwa ndio Wahanga.
Unyama huo ulifanywa kupitia soko la watumwa la Mkunazini chini ya Sultan.
Hivyo sultan wa Zanzibar ni ''accomplice'' katika unyama huo iwe kabla au baada. Period
Mkuu Nguruvi3, Mkuu Gavana ni free writer tuu akiwatetea Waarabu na udhalimu wao kwenye biashara ya utumwa kwa kuhusianisha na dini ya Kiislamu, kwa vile dini ya Kiislamu inatumia lugha ya Kiarabu, kwake Waarabu ni watu wa Allah na ndani ya Quran utumwa umeruhusiwa, hivyo kwake atatetea lolote litakalofanywa na Mwarabu in the name of Islam, hata Osama alitetewa sana humu.

Lakini Maalim Mohammed Said, is a writer with a mission and a motive behind.

P
 
Back
Top Bottom