Kwanini historia ya Zanzibar ya kweli haisomeshwi?

Kwanini historia ya Zanzibar ya kweli haisomeshwi?

Nguruvi3, huyu mtu anayejiita Mohamed Said ni mtu wa hatari sana katika mustakhabali wa taifa hili...
Mag3,
Unaandika ukiwa umeghadhibika.
Mimi sijiiti.

''Mohamed'' ndilo jina nililopewa na wazazi wangu.
Unatafuta msaada wewe umeshindwa kupambana na mimi kwa hoja.

Ningekuwa mimi mchochezi ningekamatwa na kuhudhurishwa mahakamani miaka mingi iliyopita wasingekusubiri wewe.

Wala hakuna popote nilipohalalisha au kuharamisha.

Naandika na kutoa fikra zangu kadri ninavyoijua historia na ukweli wake na huku si kupandikiza chuki.

Unawazungumza Wamanyema na Wazulu katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Fanya utafiti wako mwenyewe katika majina haya utajua michango yao: Saadan Abdul Kandoro, Iddi Faiz Mafungo , Iddi Tosiri, Sheikh Mohamed Ramia, Mzee bin Sudi, Bilal Rehani Waikela, Salum Abdallah kwa kuwataja wachache.

(Huyo Salum Abdalla ni babu yangu na ni kizazi cha kwanza katika ukoo wetu kuzaliwa Tanganyika baba yake katokea Belgian Congo).

Walikuwapo pia Wanyasa katika uasisi wa TANU kama Denis Phombeah na Wakenya kama Dome Budohi.

Alikuwapo Sheikh Hassan bin Ameir, Mzanzibari Mmakundichi katika TANU na kapigania uhuru wa Tanganyika.

Mbona umewasahau Wanubi Ibrahim Hamisi na Rashid Kheri Baghdelleh na Mwalimu Sakina na Mwalimu Fatna mashoga wakubwa wa Mama Maria Nyerere walipohamia Dar es Salaam baada ya Mwalimu kujiuzulu kazi?

Hupendi watajwe?
Wakitajwa kwako ni uchochezi?

Hii ni historia ya pekee.

Labda wewe unakerwa na hayo majina lakini Mzee bin Sudi ni muasisi wa African Association 1929, Iddi Faiz Mafungo ndiye alikuwa Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na ndiye aliyeaminiwa kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO 1955.

Saadan Abdul Kandoro kafanya makubwa toka enzi za TAA na ni mmoja katika waasisi wa TANU.

Mzulu Kleist Sykes katiwa katika Dictionary of African Biography kwa mchango wake katika maendeleo ya Tanganyika.

Wanae wote watatu Abdul, Ally na Abbas wameshiriki katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika na kwa hakika ndiyo waliompokea Mwalimu Nyerere.

Abdul na Ally baada ya kusahaulika miaka mingi hatimae walitunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru na Rais Kikwete.

Yapo mengi.

Haijawa uandishi wa kuongeza elimu kuwa ni uchochezi kwa kuwa tu wewe historia hii huijui au huipendi.

Unazungumzia ulowezi wa Waarabu Zanzibar.

Mbona umesahau kuwa Zanzibar kuna kuchanganya damu kukubwa kunakokwenda nyuma karne nyingi?

Hili hulijui?

Kwa kukuelimisha Zanzibar imetawaliwa na Rais aliyekuwa na mchanganyiko wa damu lakini ni Mzanzibari kama alivyo Ussi na Makame na Ikulu ikakaliwa na "First Lady," ukipenda muite "Muarabu," maana hili ndilo utaelewa haraka.

Angalia hapo chini ''Bilombe ya Tanganyika.''

Iko nyimbo ya African Jazz Dr. Nico Kassanda, Dechaude kaka yake, Rochereau na wanamuziki wengine inaitwa ''Bilombe ya Africa,'' yaani ''Wanaume wa Afrika.''

Nyimbo hii baba yangu akiipenda sana kusikiliza katika Dansette Record Changer yake katika 1960s mimi mdogo nami nikawa pia naipenda.

Waangalie Wamanyema hapo na Baba wa Taifa mwaka wa 1955 wako Dodoma wanazunguka kuijenga TANU kupigania uhuru.

Hawa ni Bilombe ya Tanganyika.

1575026413793.png

Kushoto Iddi Faizi Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere Saada Abdul Kandoro na Hamisi Taratibu
''Bilombe ya Tanganyika''
"Midume ya Tanganyika"
 
Nguruvi3,
Sijawasikia hao unaowahurumia wakilalamika kuwa hawapendi kunisoma.

Mimi nakuhurumia wewe kwa kujua kuwa unazungumza kitu usichokijua.

Kila nikitia mguu Zanzibar huwa naombwa kuzungumza:

View attachment 1275758
Radio Mtoni Zanzibar
Kipindi Maalum


Unaalikwa kuzungumza kwasababu za kidini na sio historian.
 
Kuna lile jengo pale mji mkongwe lenye nguzo kubwa sana (sikumbuki jina) ilidaiwa enzi hizo kwamba watumwa walizikwa hai katika kila nguzo. Sasa hivi inakanushwa kwamba haikutokea hivyo! Inaelekea historia inapotoshwa pande zote in favour of the masters and pande mwingine unao favour the slaves.

Kwa kifupi wanzazibari mmechanganyikiwa. Uzuri wa leo wa mwarabu haubadili maovu waliyofanya then. Na haubadilishi kamwe role played na wamisionari katika kuondoa biashara ya watumwa.

Get your act together.

Anyway hata huku bara sielewi na sitaelewa kamwe kwa nini Mkwawa ni shujaa. Personally mtu anaye commit suicide namuona ni coward.


WAARABU KUTOKA TANGANYIKA WANAVYOWATESA WATUMWA ZANZIBAR

 
Wazungu na waarabu wali fanya yanayofanana. Wazungu walifanya biashara ya utumwa hasa hasa magharibi mwa Africa lakini baadae wakaacha. Mwarabu alifanya biashara ya utumwa huku kwetu, akaachishwa na mzungu.

Wote ni watu wa ovyo kwetu. Namwona wa ajabu yoyote anAye watetea hao watu.

Wote hawatupendi sisi. Inabidi tujipende wenyewe. Wote wanatudharau.. Inabidi tusijidharau wenyewe. Wanatuona kama vitu tu.

Mbona mnakomaa kuwatetea na kuwapamba hapa? Sijui mkoje nyie watu! Mnalipwa nini? Mnalipwa kujidharau na kujikana wenyewe?

Ooohi,

Hebu fungueni hapa siliconafrica.com

Kuna vi article vifupi fupi, hutokuwa bored na cha muhimu zaid mwandishi anasisitiza kuji amini


Wakristo Wanapanga Biashara Ya Utumwa

Watumwa walikuwa wanachukuliwa kutoka hata katika wakati wa Ufalme wa Kirumi, lakini “biashara halisi ya Utumwa”

ilianza mnamo karne ya 16 baada ya ujio wa mataifa ya Kikristo ya Ulaya. Edward A. Alpers wa Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam, anaandika kwamba;

“kama tunavyoleta utofautisho baina ya biashara inayoambatana katika watumwa ambayo ilichuruzika katika sahara kutoka magharibi mpaka kaskazini ya Afrika kuanzia siku za nyuma sana za wakati wa utawala wa Ufalme wa Kirumi, kwa upande mmoja, na kioja tunacho kiita The West African Slave Trade kwa upande mwingine, kwa hiyo lazima tulete tofauti hiyo hiyo kwa Afrika ya Mashariki.”1

Walter Rodney pia wa Chuo, Kikuu cha Dar es Salaam, anaanza kuandika kijitabu chake

“West Africa and the Atlantic Slave-Trade kwa maneno yafuatayo: -

Wakati wote lazima ikumbukwe kwamba biashara ya utumwa iliyo;fanyi- ka katika bahari ya Atlantiki” lilikuwa ni tukio katika histo- ria ya dunia, iliyo husisha mabara matatu – Ulaya, Afrika na Marekani.

Watu walio toka kwa dhamira ya kutafuta watumwa walikuwa Wazungu waliotoka katika kila nchi kati ya Sweeden kwa upande wa Kaskazini na Ureno kwa upande wa magharibi.

Wareno walifika Afrika ya Magharibi muda mfupi kabla ya kuingia nusu karne ya kumi na tano. Mara moja na kwa haraka sana walianza kukamata (watumwa) Waafrika na kuwapeleka kufanya kazi Ulaya kama watumwa, hususan katika Ureno na Hispania.

Lakini maendeleo muhimu sana kwa biashara hii ya utumwa yalikuwa katika karne ya kumi na sita, ambapo mabepari wa Kizungu walitambua kwamba wangepata faida kubwa sana kwa kutumia nguvukazi ya Waafrika kuujenga na kuuendeleza utajiri wa nchi zote za Amerika.

Matokeo yake, Waafrika walipelekwa Amerika ya kaskazini, Amerika ya kati, Amerika ya kusini na Visiwa vya Caribbean kwa ajili ya kukidhi haja ya nguvukazi ya watumwa kwenye machimbo ya dhahabu na shaba, na kwenye mashamba ya kilimo cha mazao ya miwa, pamba na tumbaku. Biashara hii mbaya ya kununua na kuuza binadamu ilidumu kwa kipindi cha miaka (400) mia nne, kwani Atlantic slave-Trade (Biashara ya Utumwa wa kupitia bahari ya Atlantiki) ilikoma mwishoni mwa miaka ya 1870.

“Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu jinsi Biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilivyopangwa huko Ulaya, na kuhusu faida kubwa iliyokusanywa na nchi kama Uingereza na Ufaransa. Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu safari za kutisha kutoka Afrika hadi Marekani kuvu- ka bahari ya Atlantic. Waafrika walipangwa kama dagaa kwenye meli za kubeba watumwa, na matokeo yake walikufa wengi sana.”2

Na dagaa walioje! Kwa maelezo zaidi kuhusu upakiaji huu wa watumwa kwenye meli, soma taarifa ifuatayo: - Moja ya hati yenye kuuvunja moyo sana katika nyaraka zote zinazotisha ni “Plan of the Brookes,” mpango mbaya sana wa karne ya kumi na nane wa kupanga watumwa kwenye meli ya kubeba watumwa ‘Brookes’… Kwa mahesabu sahi- hi, teknolojia ya kushtua ilitengenezwa - futi na inchi, chumba cha kusimama na nafasi ya kupumua iliwekwa kwa matumaini ya faida kubwa.

Mtu mmoja Bwana Jones anapendekeza kwamba wanawake watano wahesabiwe kama wanaume wanne, na wavulana watatu au wasichana watatu wafanywe kuwa sawa na watu wazima wawili … kila mtumwa mwanaume aruhusiwe futi sita kwa futi moja na inchi nne (1’4”x6’) kama nafasi ya chumba chake, kila mwanamke alipewa nafasi ya upana wa futi tano na inchi kumi na futi moja na inchi nne…. (5’10”x1’4”); na inaendelea hivyo mpaka kila mtu anapata nafasi – watumwa 451.

Lakini Muswada wa Bunge unaruhusu watumwa 454. Kwa hiyo hati hiyo inahitimisha kwamba kama watumwa watatu zaidi wangeweza kuwekwa kwa kubanwa katikati ya wale waliotamkwa kwenye mpango, mpango huu ungeweza kuchukua idadi ile ile ambayo imeelekezwa kwenye muswada.3

Mara Waafrika walipofikishwa upande mwingine wa bahari ya Atlantic, kwa hakika walikuwa katika “Dunia Mpya”, iliyojaa ukandamizaji na ukatili. Taarifa ifuatayo inaweza kusaidia kuelewa hali ilivyokuwa wakati huo. Rodney anaandika:

“Kuanzia wakati walipofika (Wakristo) Wazungu hadi 1600, takriban Waafrika milioni moja (1, 000,000) walichukuliwa kwenye meli za kubeba watumwa. Wakati wa kipindi hicho, Wareno walikuwa ndio wafanya biashara wakuu wa biashara ya watumwa huko Afrika ya Magharibi.

Ama wali- wapeleka Waafrika huko Brazil, ambayo nchi hiyo ilikuwa koloni lao, au vinginevyo waliwauza kwa waloezi wa Kihispania huko Mexico, Amerika ya kati, Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean. Mnamo karne ya kumi na saba, kiasi cha Waafrika wapatao milioni saba hadi nane kutoka Afrika ya magharibi walivushwa bahari ya Atlantic.

Wadachi walijumuika na Wareno kama wafanya biashara wakuu wa biashara ya utumwa mnamo karne ya kumi na saba, na karne iliyofuata Waingereza wakawa wafanya biashara wakubwa kushinda wote wa biashara ya utumwa.

Wakati biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilipofikia kileleni mnamo karne ya kumi na nane, meli za Kiingereza zilikuwa zinachukua zaidi ya nusu ya jumla yote ya watumwa na idadi iliyobaki iligawanywa baina ya Wadachi, Wafaransa, Wareno na Wadane (Danish).

“Ilipofika karne ya kumi na tisa, palikuwepo na mabadiliko mengine ya watu ambao walishika nafasi mbele katika kuinyonya Afrika. Nchi za Ulaya zenyewe hazikushiriki kikamilifu kwenye biashara ya utumwa, lakini badala yake Wazungu ambao waliloea Brazil, Cuba, na Amerika ya Kaskazini ndio ambao walipanga sehemu kubwa ya biashara.

Waamerika (U.S.A) ndiyo katika kipindi hicho hicho tu walipata uhuru kutoka kwa Waingereza, hili lilikuwa taifa jipya (U.S.A.) ambalo lilikuwa na mgawo mkubwa kabisa kuliko wote katika biashara ya watumwa katika biashara ya Atlantiki katika kipindi cha miaka hamsi- ni ya mwisho, kwa kuchukua kiwango kikubwa zaidi cha watumwa kuliko ambavyo imewahi kufanya huko nyuma.

“Ilipoanza “biashara ya watumwa ya Atlantiki kwenye pwani ya Afrika ya Magharibi, ilichukua utaratibu wa kutu- mia nguvu moja kwa moja wa Wazungu kuwashambulia Waafrika waliokuwa wanaishi karibu na pwani. Mabaharia wa kwanza wa Kireno walipofika kwenye pwani inayoju- likana leo kama Mauritania, waliacha meli zao na kuanza kuwawinda watu waitwao, Moors watu walioishi katika jimbo hilo.

Kwa kweli, hii haikuwa biashara hata kidogo – ilikuwa uvamizi wa nguvu. Hata hivyo, baada ya mashambulizi kadhaa ya kushtukizwa, Waafrika wa pwani wakawa na kawaida ya kulinda kwa zamu na walijilinda kwa nguvu dhidi ya washambuliaji wao Wazungu.

Katika kipindi kifupi tu, Wareno walitambua kwamba uvamizi haikuwa mbinu inayofaa na iliyo salama katika kujaribu kuwapata watumwa. Zaidi ya hayo, pia walitaka dhahabu na bidhaa zingine za Kiafrika, ambazo wangeweza tu kuzipata kwa njia ya kununuliana na kuuziana kwa amani.

Kwa hiyo badala ya kuvamia, Wareno waliona afadhali kutumia bidhaa zilizo tengenezwa kiwandani ili kuwatia moyo Waafrika kubadilishana na bidhaa zao na hata kuweza kuwafikisha mateka wa Kiafrika kwenye meli za Wazungu kwa urahisi. Mpango huu haukufanywa na Wareno pekee, lakini hata wazungu wengine wote walitambua na kukubali kwamba huo ulikuwa mpango mzuri zaidi wa kupata bidhaa hapa Afrika; na ilikuwa kwa njia hii waliweza kupata mamilioni mengi ya Waafrika.”4

Akifafanua juu ya kipengele hiki cha biashara ya watumwa, mwandishi anasema: “Moja ya vitu muhimu sana ni kutambua jambo liumalo sana na lisilo pendeza kwamba walikuwepo Waafrika ambao waliwasaidia na kushirikiana na Wazungu katika kuwafanya Waafrika wenzao kuwa watumwa.

Maana yake ni kwamba hatuwezi kuchukua msimamo dhaifu na kusema kwamba watu weupe walikuwa wabaya sana na watu weusi walikuwa waathirika (katika kuangamia). Mfano unaofaa na sambamba ambao ungeweza kusaidia kuelewa yale yaliyotokea katika Afrika ya Magharibi wakati wa kipindi cha karne za biashara za watumwa unaweza kuonekana hapa Afrika leo, ambapo viongozi wengi wanashirikiana na mabeberu wa Ulaya na Marekani (U. S. A.) kwa lengo la kuwanyonya na kuwakan- damiza Waafrika walio wengi.

Hatimaye, Waafrika wa Afrika ya Magharibi walifikishwa kwenye hali ya “uza au uuzwe.”
Hapa suala la bunduki lilikuwa na umuhimu maalum. Kuwa na nguvu, serikali ili- hitaji bunduki, lakini ili kupata bunduki kutoka kwa wazungu, Waafrika ilibidi kuwapa Wazungu watumwa na wao kupewa bunduki.

Watawala wa Kiafrika walijikuta wenyewe wanawauza watumwa ili wapate bunduki ambazo ziliwawezesha kuwakamata raia wao na kuwauza kama watumwa ili wanunue bunduki nyingi zaidi. Hali hii inaweza kuelezewa, kama “ubaya juu ya ubaya (mzunguuko unaoashiria kukwama).” Watawala wa Kiafrika ambao waliwasaidia wazungu hawasameheki moja kwa moja, lakini inafafanua jinsi gani mwishoni hawakuwa washirika halisi wa Wazungu bali walikuwa watumishi au vibaraka wa Wazungu.” 5

Na kanisa lilikuwa linafanya nini wakati wote huo? Msikilize mwandishi huyu huyu anasema; “Kwa sababu faida kubwa sana ilikuwa inapatikana kwa kuwachukua watumwa kutoka Afrika, Wazungu walikataa kuzisikiliza dhamiri zao.

Walifahamu kuhusu mateso yaliyo wapata watu katika Afrika, ndani ya meli za kubebea watumwa na kwenye mashamba yaliyokuwa yanalimwa na watumwa ya Waamerika, na walitambua kwamba kuwauza binadamu wenzao ni jambo ambalo halingethibitishwa kimaadili. Hata hivyo kanisa la Kikristo lilijitokeza na kutoa sababu nyingi likijitetea kuingia kwake katika biashara ya watumwa.

Wachungaji wengi walifanya biashara ya watumwa, hasa katika Angola, na wengine wengi walimiliki watumwa, katika nchi za Amerika. Sababu moja tu ambayo ilitolewa na kanisa Katoliki kuhusu vitendo vyake ilikuwa kwamba lilikuwa kinajaribu kuziokoa roho za Waafrika kwa kuwabatiza watumwa. Waprotestanti walikuwa wabaya zaidi, kwani wala hawakuweka wazi kwamba walikubali kwamba Waafrika walikuwa na roho.

Badala yake, walikubaliana na fikira kwamba mtumwa wa Kiafrika alikuwa sehemu ya rasilimali kama fenicha au hayawani wa kufugwa. Hakuna sehemu ya historia ya Kanisa la Kikristo ambayo inafedhehesha zaidi kuliko kusaidia “Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki.”6

Kwa mujibu wa orodha ya Lloyd, iliamuliwa kwamba watumwa walikuwa ni bidhaa, na wenye thamani sana. Hati za bima zilizochukuliwa kutoka Lloyd waliwakatia watumwa hati za bima hadi kufika kiasi cha pauni za Kiingereza 45 kila mtumwa kiasi hicho cha fedha ni kikubwa katika kipindi hichi cha mwanzoni mwa karne ya 18 huko Uingereza.

Ili kuwazuia watumwa wasitoroke, au kuwaadhibu, nyenzo zisizo za kawaida kama zilivyoorodheshwa hapa zilitumiwa katika Afrika ya Magharibi na katika visiwa vya West Indies.7

Siku zote kulikuwepo watu wachache ambao walipinga Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki. tangu mwanzo; lakini serikali mbalimbali na wafanya biashara hawakuwajali, wakati wa karne ya kumi na tano, kumi na sita na kumi na saba. Haikuwa hivyo, hadi mwishoni mwa karne ya kumi na nane wakati majaribio ya dhati yalifanywa kwa lengo la kukomesha biashara hii.

James Boswell, akijaribu kukana hoja za watu waliotaka biashara ya watumwa ikomeshwe, anaandika katika kitabu chake kiitwacho “Life of Johnson.” Kwamba: Jaribio la kinyama na la hatari ambalo kwa muda fulani limeendelea kuwepo kwa lengo la kupata sheria ya bunge letu, ili kukomesha tawi la maana sana na muhimu la faida kibiashara, lazima lingekwisha amuliwa mara moja, kama isin- gelikuwa kundi lisilo na maana la washabiki waliokuwa msitari wa mbele kwalo bila kufaulu, ndilo ambalo linaunda kundi kubwa la Wakulima, Wafanya biashara na wengineo ambao rasilimali yao imetumbukizwa na kuhusishwa kwenye biashara hiyo, kwa sababu zao kujikinaisha, hufikiria kwamba hapangekuwepo na hatari.

Ujasiri ambao jaribio hilo limepata msisimko mshangao wangu na hasira, na ingawa watu fulani wenye uwezo mkubwa wameliunga mkono, ama kwa sababu ya kutaka umaarufu wa muda mfupi, wakati wanao utajiri, au kupenda kujumuika kwenye fitina, wakati hawana kitu, maoni yangu hayatetereki.

Kukomesha hali ya kuwepo utumwa ambayo katika zama zote, MUNGU ameruhusu, na binadamu akaendeleza, haingekuwa unyang’anyi tu kwa tabaka la raia wetu wasio hesabika; lakini pia ingekuwa ukatili mno kwa Washenzi wa Kiafrika, ambao sehemu kutoka miongoni mwao inaokolewa kutoka kwenye mauaji ya kinyama, au kutoka kwenye utumwa isiyovumilika katika nchi yao wenyewe, na huwaingiza kwenye maisha ya hali ya furaha zaidi, hasa zaidi sasa kupita kwao kwenda katika visiwa vya West-Indies na wanavyotendewa huko katika hali ya udhibiti wa kibinadamu. Kukomesha biashara hiyo itakuwa sawa na kufunga milango ya huruma kwa binadamu.”8

Marekebisho ya takrima ya kibinadamu wanayofanyiwa na huruma, hujionyesha yenyewe kwenye maelezo ya kina na picha iliyoonyeshwa hapo juu!
  • 1. Alpers, Edward A., East Africa Slave-Trade (Dar-es-Salaam: The Historical
    Association of Tanzania, 1967)
  • 2. Rodney, Walter., West African and the Atlantic slave-trade (Dar- es-Salaam: The
    Historical Association of Tanzania, 1967)
  • 3. Newsweek (March 15, 1965) uk. 106
  • 4. Rodney, op. cit., uk.4-5
  • 5. Ibid, uk. 7f.
  • 6. Ibid uk.22.
  • 7. Lloyd’s list, 250th Anniversary (1734-1984) April 17, 1984, London, uk. 149.
  • 8. Boswell, J, Life of Johnson (N.Y. Modern Library Edition, 1965) Uk. 365
 
Huyu Mzee siku zoote yeye ni kurekebisha historia tu, kila kilichoandikwa si sahihi, sahihi ni anachojua yeye na maprofesa wake wa kiarabu.


Biashara Ya Watumwa Ya Afrika Ya Mashariki

Kama ilivyokuwa Afrika ya Magharibi, biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki ilikuwa mashuhuri na ilianzishwa kikamilifu na kutokana na maendeleo na jitihada za nchi za Kikristo za Ulaya.

Bwana E. A. Alpers anaandika kwenye “African Slave-Trade (Biashara ya Utumwa ya Afrika):

Ushahidi zaidi kwamba biashara ya watumwa kwa vyovyote vile ilikuwa mashuhuri katika Afrika ya Mashariki kabla ya karne ya kumi na nane, imeletwa na Wareno.

Hakika Wareno, wakiwa ndiyo waasisi (waanzilishi) wa Atlantic Slave-Trade, wangejaribu kuendeleza biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki kama wangeikuta tayari ipo na imekwisha shamiri. Lakini maandiko ya mwanzo ya Wareno yanataja tu biashara ya watumwa kwa kupitia tu.

Lililokuwa muhimu zaidi ni wale wafanyabiashara za dhahabu na pembe za ndovu walizipeleka Arabuni na India. Wavamizi wa Kireno walielekeza juhudi zao kwenye bidhaa hizo wakati wa karne ya kumi na sita na kumi na saba, sio tu kwenye pwani ya Kenya na Tanzania, bali pia katika Msumbiji na Zimbabwe.

Hata nta na ambari zinaonyesha zilikuwa bidhaa muhimu zaidi kuzidi watumwa wakati mrefu sana wa kipindi hiki. Kwani tofauti na wakoloni katika nchi ya Amerika, Wareno kamwe hawakuanzisha uchumi wowote wa kilimo huko India.

Biashara ya watumwa ya Wareno kutoka Msumbiji kwenda India kwa nadra sana ili- fika idadi ya watu elfu moja katika kipindi cha mwaka mmoja wowote ule, na kwa kawaida ilikuwa chini ya nusu ya idadi hiyo. Huko Brazil ilikuwa haramu kufanya biashara ya watumwa hadi mwaka 1645, na kamwe haikulitiliwa maanani hadi mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa.

Hadi mwaka wa 1753, wakati misingi ya biashara mpya ya watumwa ilikuwa inawekwa Afrika ya Mashariki, palikuwepo na jumla ya watumwa 4399 tu wa Kiafrika katika India yote ya Wareno.

“Misingi hii ni ipi? Licha ya mahusiano ya muda mrefu baina ya Waarabu na Afrika ya Mashariki, biashara ya watumwa haikutiliwa matumaini na Wafaransa.

Kwa mujibu wa tarakimu rasimi, zaidi ya watumwa 1,000 walikuwa wanasafirishwa kila mwaka. Wafaransa, wakifanya magendo kwa ajili ya kukwepa kodi ambazo zilitozwa Msumbiji, labda waliongeza idadi na kufika angalau 1,500.

Inawezekana ni idadi ile ile ilichukuliwa kutoka Ibo wakati wa muongo huu. Kwa hiyo Wareno kule Msumbiji na Ibo (na baadaye Quelimane, karibu na mdomo wa mto Zambezi unapoingilia baharini) walijishughulisha na sera ya biashara ya watumwa na hawakurudi nyuma, wakaendelea nayo hadi kukomeshwa kwake.

Biashara ya watumwa ilizidi kupamba moto mnamo miaka ya themanini, hasa zaidi baada ya kumalizika vita ya uhuru wan chi ya Amerika.

Katika miaka ya sabini, wafanya biashara ya utumwa wachache wa Kifaransa walichukua mizigo kutoka Msumbiji kwenda visiwa vya West-Indies, kwa sababu waliiona hasara ilikuwa inaongezeka katika wakati wa kutafuta bidhaa zao zinazohamashika kwenye pwani ya Guinea.

Sasa, wakati wa amani, kwa mashindano makubwa zaidi ya kutafuta watumwa katika Afrika ya Magharibi, ilifunguliwa njia kwa ajili ya upanuzi mkubwa wa biashara ya watumwa ya Waamerika kutoka Afrika ya Mashariki.

Wakati huo huo meli za Wareno pia zilianza sehemu ya kufaa (ingawa ilikuwa bado ni ya kufuata) katika biashara ya watumwa kwenda kisiwa cha Mascarene. Tarakimu rasimi kutoka Msumbiji peke yake zinaonyesha kwamba tangu 1781 hadi 1794 jumla ya watumwa 46,461 walipakiwa kwenye meli za Kireno na za kigeni, ambazo karibu zote zilikuwa za Wafaransa. Ikijumlishwa na idadi ndogo ya magendo, angalau watumwa 4,000 lazima walikuwa wanaondoka Msumbiji wakati wa kipindi hiki kila mwaka.” 1

Ilikuwa katika hali hii ambayo Waarabu walipanua msaada wao kuwasaidia hawa wafanyabiashara ya utumwa wa Kikristo. Mwandishi huyo huyo anasema:

“Baada ya Waarabu wa Oman kuitika wito wa baadhi ya watawala wa Kiswahili wa miji ya pwani na kwa msaada wao waliwatoa Wareno kutoka Mombasa mnamo 1698 na sehemu zingine muhimu za mbali, wao wenyewe walikuwa wanyonge sana kushughulika na jambo lingine zaidi ya kuwasumbua na kuwaibia watu hao hao waliowaomba msaada wao; lakini baada ya familia ya Busaid ilipowapindua Yarubi na kuanzisha utawala wao katika Oman mnamo 1744, wali- weza kuanza unyonyaji wa kiuchumi wenye faida kutoka kwa watu wa Afrika ya Mashariki.

Kama walivyofanya wafanya biashara wote wa zamani sehemu ya pwani, lengo lao kubwa na la msingi ni kupata pembe za ndovu, lakini kuanzia hapo pia tunaweza kuona ongezeko katika biashara ya watumwa.

“Hata hivyo, hakuna takwimu sahihi zozote zile zenye kuonyesha kuhusu ukubwa wa biashara ya utumwa iliyofanywa na Waarabu katika karne ya kumi na nane. Dalili ya kwanza iliopo inatoka kwa mfanya biashara ya watumwa wa Kifaransa aitwaye Jean Vincent Morice, ambaye alifanya biashara Zanzibar na Kilwa, ambayo ilikuwa bandari muhimu ya watumwa katika pwani, mnamo miaka ya 1770. Mnamo tarehe 14, September, 1776, Morice alifanya mkataba na Sultani wa Kilwa kwa ununuzi wa angalau watumwa

1,000 kwa mwaka. Katika misafara mitatu kabla ya kuutia sahihi mkataba huu, Morice alikwisha nunua watumwa 2325 kwa ajili ya kuwasafirisha nje. Morice hatuambii Waarabu walikuwa wakiwachukua watumwa wangapi kutoka pwani kila mwaka, lakini kwa wazi aliona kuwa ilikuwa biashara kubwa kwa viwango vya Kifaransa.

Inaonekana ni sawa kusema kwamba angalau watumwa 2000 walikuwa wanachukuliwa kwa mwaka katika kipindi hicho. Kwa hiyo, licha ya kwamba Wafaransa hawakutawala biashara ya watumwa hapa kama walivyofanya Msumbiji, walikuwa kichocheo kwa mahitaji ya soko la watumwa katika kipindi ambacho biashara ya Waarabu ilikuwa bado ndiyo inakua katika uchanga wake. Juhudi za Ufaransa ziliendelea hadi miaka ya 1780, lakini mnamo mwishoni mwa karne hiyo, juhudi hizi zilionyesha zilikwisha pungua sana umuhimu wake kuliko biashara ya Waarabu.

Mambo kadhaa mapya yalisababisha kuongezeka mahitaji ya watumwa kutoka Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya kumi na tisa. Katika eneo la mamlaka la pwani ya Ureno, palikuwepo na ongezeko la juu sana katika biashara ya utumwa kwenda Brazil. Hii ilisababishwa na kuondolewa kwa familia ya kifalme ya Kireno kutoka Lisbon kupelekwa Brazil wakati wa Vita za Napoleon. Ruhusa maalum zilitolewa kwa Wabrazil na mara biashara inayoshamiri katika watumwa ikawa inaendeshwa kupitia Rasi ya Tumaini Jema huko Afrika ya kusini.2

“Sasa ni ukweli unaokubalika miongoni mwa wataalam wa historia makini wa Afrika ya Mashariki kwamba njia ndefu za biashara kati ya bara na pwani zilianzishwa hasa zaidi kwa kutumia ujasiri na moyo wa kujituma wa Waafrika. Kwa maneno mengine njia za biashara zilibuniwa na Waafrika kutoka bara kwenda pwani, wala si Waarabu, au Waswahili, ambao walisafiri kutoka pwani kwenda bara kupitia sehemu zisizojulikana.

Wafanya biashara wa Kiswahili walianza tu kutelekeza usalama wa pwani mnamo nusu ya pili ya karne ya kumi na nane, na walisafiri kufuata njia safi ambazo ziliendelezwa kwa miongo mingi kabla yake. Ni baada tu kuanza karne ya kumi na tisa ndipo wafanya biashara wa Kiarabu walijasiri kufuata njia hiyo.” 3

Wayao ambao walikuja kuwa wafanya biashara makini sana wa Kiafrika wa biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki, hivyo walikuwa na desturi ya muda mrefu ya kubeba pembe za ndovu na bidhaa zingine halali kwenda pwani miongo mingi kabla ya mahitaji ya pamoja ya Wafaransa na Waarabu kutaka watumwa yalipoeleweka.”4

“Katika Afrika Magharibi njia hizi ziliendeshwa kwenda bara kutoka pwani na Waafrika ambao kazi yao hasa ilikuwa kutafuta watumwa. Watumwa walitawala biashara ya Afrika ya Magharibi tangu mwanzo. Katika Afrika ya Mashariki wala hapakuwepo na hali zilizolingana na hiyo. Biashara ya watumwa lazima ionekane kuwepo katika mazingira ya mapema zaidi, iliyokwishajengeka kwa umakini, na biashara yenye faida ya masafa marefu ambayo chimbuko lake ilikuwa ubebaji wa pembe za ndovu. Hii ni muhimu kukumbuka hasa kwa mikoa ya kusini ambalo kila mara ilikuwa hazina kuu ya “Biashara ya Utumwa katika Afrikamashariki.”5

Bwana Alpers anahitimisha, “lazima iwe wazi sasa kwamba fikira ya zamani inayotamkwa kiholela kwamba wengi wa watumwa walikamatwa na wafanya biashara wanyang’anyi wa Kiarabu na Kiswahili ni moja wapo ya mambo ya kubuniwa na ngano tu ambazo zimekuzwa kuhusu biashara ya watumwa ya Afrika mashariki. Lakini lazima tuwe waangalifu tusifanye kosa la kutoa tathmini potofu kuhusu mchango waliotoa watu hawa kwenye biashara hii.” 6

Kwa mara nyingine, lazima nisisitize kwamba lengo langu si kudhihaki juhudi za kundi dogo la waadilifu ambao walikuwa wanashughulika na propaganda dhidi ya utumwa. Ninachotaka kuonyesha ni kwamba juhudi zao hazikufaulu (na hazingefaulu) hadi pale shinikizo la kiuchumi lilipoilaz- imisha kwanza Uingereza ilipolazimika kufuatana na matatizo ya kiuchumi kuanza kuzuia utumwa, biashara ya utumwa na halafu kukomesha utumwa.

Kwa kweli, Uingereza ilipojitokeza kwa ajili ya kutaka kukomesha utumwa haikusimama kwenye mapaa ya nyumba na kutangaza kwamba ilikuwa inakomesha utumwa kushindana dhidi ya wenye viwanda wa Kifaransa. Uingereza ililigeuza jambo hili kuwa suala la kimaadili na kiunyofu kabla haijatumainia kushinikiza serikali zingine kufuata mpango wake. Na ilifanya hivyo. Tunatambua jinsi Uingereza ilivyoanzisha vita si kwa lengo la kulinda maslahi ya himaya yake kiuchumi na kisiasa, lakini ilifanya hivyo ili “kulinda Uhuru wa Watu.”

Ndivyo ilivyokuwa kuhusu vita yake dhidi ya utumwa. Murua na maadili mema lilikuwa suala la waadilifu wachache tu ambao hawakuwa na uwezo. Suala halisi, kama serikali mbali mbali na walowezi na wakoloni walivyohusika, lilikuwa kuhusu uchumi.
  • 1. Alpers, op. cit., uk. 5-6
  • 2. Ibid uk. 7-8.
  • 3. Ibid, uk. 13.
  • 4. Bid, uk. 14.
  • 5. Ibid uk. 15.
  • 6. Ibid uk. 24.
 
Unaalikwa kuzungumza kwasababu za kidini na sio historian.
Remote,
Tujaalie nimealikwa na Waislam wanamualika Muislam mwenzao.

Lakini nimealikwa Zentrum Moderner Orient Berlin.

Nimealikwa University of Iowa na nimealikwa Northwestern University Evanston Chicago.

Nimealikwa Kenyatta University na kwengine kwingi.

Nimeshirikishwa katika miradi ya kuandika historia ya Afrika Harvard na Oxford University Press New York wamechapa kazi zangu.

Hawa si Waislam.
 
"Mag3, post: 33615720, member: 10873"]Sina shaka kwamba mapinduzi yaliyomfungasha virago Sultani kwake yeye yalikuwa haramu. Huyu ni mtu wa kuogopwa kama ukoma.
Atakwambia watu waliletwa kutoka Kipumbwi kufanya mapinduzi.

Hasemi kama tukio hilo limeharamisha mapinduzi, lakini between the lines Mohamed anaamini Zanzibar ilikuwa bora wakati wa Sultan.

Mapinduzi anayaona kama shambulizi dhidi ya Uislam. Hasemi wazi maandiko yake yanasema

Kwa msingi huo mwenzetu yupo njia panda kati ya mambo mawili yanayotofautiana

Hawezi kusema mapinduzi ni haramu, atawaudhi Wamatumbi Waislam
Hawezi kusema mapinduzi ni halali, atawaudhi waathirika ambao ni Waislam

Kwahiyo njia nyepesi ni kutafuta ''grey area'' akijivika wajihi wa Popo
 
Nguruvi 3,
Umeandika mengi na umenisukumia mengi.
Zanzibar haikuja kujua jela za mateso na mauaji ila baada ya mapinduzi.

Ikiwa huu ndiyo ukweli bila shaka Zanzibar ilikuwa njema kabla ya mapinduzi kwani hapakuwa na umwagaji wa damu chini ya Sultani wala Sultani hakuwa na jela ya mateso na mauaji.

Tafadhali usichukue hili kuwa nimehalalisha utawala wa Sultani.
Hapo nimeeleza Zanzibar kama ilivyokuwa wakati wa Sultani.

Hakuna Sultani aliyeingia kaburini na damu katika vidole vyake.
Umezungumza kuhusu mapinduzi kuwa shambulizi dhidi ya Uislam.

Hili ni suala ambalo itakuwa vyema kwa Wazanzibari wenyewe kulizungumza kwani moja kwa moja linaungana na nia ya mapinduzi yenyewe.

Mimi siwezi kukupa rejea ya Lukuvi na Sitta waliposema Zanzibar haiwezi kuachiwa kwani ikiachiwa itaweka serikali ya Kiislam na serikali imekaa kimya kwa kauli hizi.

Kauli hizi maana yake ni moja tu.

Kati yangu mimi na wewe nani aliye njia panda?
Zanzibar imefanya chaguzi tano kuanzia mwaka wa 1995.

Sihitaji mimi kukueleza wewe Wazanzibari wamepiga kura namna gani na damu iliyomwagika kwa ajili ya uchaguzi.

Huu ndiyo ukweli wa historia ya Zanzibar.
 
"Mohamed Said, post: 33625549, member: 12431"]
Zanzibar haikuja kujua jela za mateso na mauaji ila baada ya mapinduzi.
Biashara ya utumwa ilikuwa starehe! Wamatumbi kuwa ''mabawabu'' ilikuwa amani na burudani

Kutupiwa biriani madirishani ilikuwa utu!
Ikiwa huu ndiyo ukweli bila shaka Zanzibar ilikuwa njema kabla ya mapinduzi kwani hapakuwa na umwagaji wa damu chini ya Sultani wala Sultani hakuwa na jela ya mateso na mauaji.
Umeeleza wazi, kwa mujibu wako mapinduzi yameleta adha na mateso na kuifanya zanzibar jela ya mateso.
Hili limekwisha, msimamo wako upo wazi
Tafadhali usichukue hili kuwa nimehalalisha utawala wa Sultani.
Unaruka kimanga! hii si ndio njia panda yenyewe, hakuna shaka yoyote iwe halali au haramu si hoja, msimamo wako ni Zanzibar njema chini ya Sultani. Mapinduzi ni mateso na jela ya adha. Huhitaji kutumia neno haramu au halali, inatosha
Hakuna Sultani aliyeingia kaburini na damu katika vidole vyake.
Yeah kwasababu biashara ya utumwa ilikuwa halali.

Halafu watumwa wenyewe walipewa biriani damu itoke wapi?
Wamatumbi walisimama milangoni na kustareheshwa kwa makalimati!
Wale watumwa waliohasiwa ilikuwa kuzuia tu uzao, hakuna damu iliyomwagika!
Umezungumza kuhusu mapinduzi kuwa shambulizi dhidi ya Uislam.
Hili ni suala ambalo itakuwa vyema kwa Wazanzibari wenyewe kulizungumza kwani moja kwa moja linaungana na nia ya mapinduzi yenyewe.
Kwa mujibu wako, Ghassan na Mzee mkwawa nia ilikuwa kupeleka ''watu wa kipumwbi kupinga Uislam'' .

Hao Wazanzibar wapo wa mapinduzi Daima, halafu wa ''Zanzibar njema kama ya Sultani''

Hivi nini kilimnyima Salim Ahmed Urais?

Hivi katiba mpya ilikwamishwa na akina nani? Huoni tatizo hapo?

Ungefuatilia kwa umakini wala usingezungumzia hayo! upo bize na Kipumbwi mengine tuachie
Mimi siwezi kukupa rejea ya Lukuvi na Sitta waliposema Zanzibar haiwezi kuachiwa kwani ikiachiwa itaweka serikali ya Kiislam na serikali imekaa kimya kwa kauli hizi.
Haifanyi mapinduzi kuwa halali au haramu.

Umeshasema Sultani alikuwa bora, huna haja ya rejea.
Utumwa kwako ni bora ilimradi tu bwana wa mtumwa ni Mwarabu!
Kati yangu na wewe nani aliye njia panda?
Wewe unayehangaika kuweka wazi wapi unasimamia, mapinduzi haramu au Halali?

Mimi sina njia panda, msimamo wangu ni mmoja, utumwa ni ushenzi tu uwe umefanywa na askofu au Sheikh, Mzungu au Mwarabu. Ni ushenzi tu uliokubuhu! period

Hakuna mtu mwenye kufanya utumwa anayeweza kutetewa hata kwa neno moja
Kutetea utumwa ni kudhalilisha utu wako. Unaweza kuwa na utu na Uislam bila dhalili

Nimesema ,Mapinduzi ya Zanzibar ni halali kuondoa adha dhidi ya Wamatumbi

Iwe imefanywa na yoyote, hilo haliondoi ukweli kuwa Sultan alikuwa bwana wa utumwa

Kitendo cha kuwabagua Wamatumbi na kuwa mabawaba, wakitupiwa biriani ni kukosa utu

Tatizo lako huna mpaka kati ya dini na watu. Waarabu ni binadamu ambao dini imeshuka kwao

Hilo haliwafanyi wawe Waislam zaidi.

Uislam na Waislam vina tofauti za kimantiki, sijui kama utanielewa katika hili na naomba radhi kama hutanielewa maana ni dhana kubwa kidogo inayohitaji fikra pana

Uislam ni dini na Waislam ni wafuasi wa dini lakini si kila Mwislam ana sifa za Uislam
Waarabu wameupokea Uislam lakini si kila mwarabu ni Mwislam
 
Biashara ya utumwa ilikuwa starehe! Wamatumbi kuwa ''mabawabu'' ilikuwa amani na burudani

Kutupiwa biriani madirishani ilikuwa utu!Umeeleza wazi, kwa mujibu wako mapinduzi yameleta adha na mateso na kuifanya zanzibar jela ya mateso.
Hili limekwisha, msimamo wako upo wazi Unaruka kimanga! hii si ndio njia panda yenyewe, hakuna shaka yoyote iwe halali au haramu si hoja, msimamo wako ni Zanzibar njema chini ya Sultani. Mapinduzi ni mateso na jela ya adha. Huhitaji kutumia neno haramu au halali, inatoshaYeah kwasababu biashara ya utumwa ilikuwa halali.

Halafu watumwa wenyewe walipewa biriani damu itoke wapi?
Wamatumbi walisimama milangoni na kustareheshwa kwa makalimati!
Wale watumwa waliohasiwa ilikuwa kuzuia tu uzao, hakuna damu iliyomwagika!
Kwa mujibu wako, Ghassan na Mzee mkwawa nia ilikuwa kupeleka ''watu wa kipumwbi kupinga Uislam'' .

Hao Wazanzibar wapo wa mapinduzi Daima, halafu wa ''Zanzibar njema kama ya Sultani''

Hivi nini kilimnyima Salim Ahmed Urais?

Hivi katiba mpya ilikwamishwa na akina nani? Huoni tatizo hapo?

Ungefuatilia kwa umakini wala usingezungumzia hayo! upo bize na Kipumbwi mengine tuachie
Haifanyi mapinduzi kuwa halali au haramu.

Umeshasema Sultani alikuwa bora, huna haja ya rejea.
Utumwa kwako ni bora ilimradi tu bwana wa mtumwa ni Mwarabu! Wewe unayehangaika kuweka wazi wapi unasimamia, mapinduzi haramu au Halali?

Mimi sina njia panda, msimamo wangu ni mmoja, utumwa ni ushenzi tu uwe umefanywa na askofu au Sheikh, Mzungu au Mwarabu. Ni ushenzi tu uliokubuhu! period

Hakuna mtu mwenye kufanya utumwa anayeweza kutetewa hata kwa neno moja
Kutetea utumwa ni kudhalilisha utu wako. Unaweza kuwa na utu na Uislam bila dhalili

Nimesema ,Mapinduzi ya Zanzibar ni halali kuondoa adha dhidi ya Wamatumbi

Iwe imefanywa na yoyote, hilo haliondoi ukweli kuwa Sultan alikuwa bwana wa utumwa

Kitendo cha kuwabagua Wamatumbi na kuwa mabawaba, wakitupiwa biriani ni kukosa utu

Tatizo lako huna mpaka kati ya dini na watu. Waarabu ni binadamu ambao dini imeshuka kwao

Hilo haliwafanyi wawe Waislam zaidi.

Uislam na Waislam vina tofauti za kimantiki, sijui kama utanielewa katika hili na naomba radhi kama hutanielewa maana ni dhana kubwa kidogo inayohitaji fikra pana

Uislam ni dini na Waislam ni wafuasi wa dini lakini si kila Mwislam ana sifa za Uislam
Waarabu wameupokea Uislam lakini si kila mwarabu ni Mwislam
Nguruvi3,
Unaamini watumwa walikuwa wanatupiwa biriani, wanahasiwa, watu wamezikwa kwenye kila nguzo ya Beit el Ajaib nk.

Unaamini minyororo ya kufungia watumwa Mkunazini na propaganda nyingi za kitabu cha Mbotela, "Uhuru wa Watumwa."

Uzuri ni kuwa wanaoeneza propaganda hizi wanafahamika lakini hawa hawa kama utawaita hapa kujadili TransAtlantic Slave Trade hawatakuja.

Yote kwa yote ukweli ni kuwa Wazanzibari wameamka na hawanasi tena katika propaganda hizi na ndiyo maana katika chaguzi tano Zanzibar wananchi wamezungumza.

Hivi sasa hili ni suala la muda tu.
 
"Mohamed Said, post: 33626084, member: 12431"]
Unaamini watumwa walikuwa wanatupiwa biriani, wanahasiwa, watu wamezikwa kwenye kila nguzo ya Beit el Ajaib nk.
Well, Pascal Mayalla, Mag3 na wengine wamekuuliza kitu muhimu sana. Tunaona mabaki ya TransAtlantic Slave trade!
Tuonyeshe wapi uzao wa watu weusi waliopelekwa Uarabuni?
Pili, watumwa walikamatwa iwe walitupiwa mkate au Birian hilo halihalalishi utumwa wao

Mohamed, Waarabu ni wakatili na wabuguzi sana kwa Waafrika.
Hili` nimelishuhudia na ku experience mwenyewe . Fikiria karne moja nyuma

Ni ubaguzi na roho za kikatili ndizo zinawafanya wasithamini wenzao kama Yemeni
Hivyo kutupiwa biria au kufungwa mnyororo miaka 100 iliyopita kwao si issue
Unaamini minyororo ya kufungia watumwa Mkunazini na propaganda nyingi za kitabu cha Mbotela, "Uhuru wa Watumwa."
Uzuri ni kuwa wanaoeneza propaganda hizi wanafahamika lakini hawa hawa kama utawaita hapa kujadili TransAtlantic Slave Trade hawatakuja.
Utumwa ni Utumwa tu haijalishia umefanywa na Askofu au Sheikh. Hakuna ushenzi mzuri

Mohamed anachotaka ni kulinganisha utumwa, upi ulikuwa bora.

Unahitaji sana kusoma mambo nje ya kile unachojua. Unahitaji kuijua dunia nje ya Kipumbwi

Huwezi kuweka utumwa katika mizani kwamba wa waarabu ni bora kuliko wazungu
Umefika hapo, sijui ukiwa uarabuni inakuwaje!

Yote kwa yote ukweli ni kuwa Wazanzibari wameamka na hawanasi tena katika propaganda hizi na ndiyo maana katika chaguzi tano Zanzibar wananchi wamezungumza.
Hivi sasa hili ni suala la muda tu.
Ndio maana nakuambia wewe hujui mambo mengine ya dunia hii kaa kimya, unajianika

Chaguzi tano wananchi wamezungumza, usichojua ni kwamba matokeo ya chauguzi hizo ni kutokana na mgawanyiko. Nilikuuliza nani alimnyima Mzee Ahemd Salim fursa ya Urais?
Salimu alikubalika na Watanganyika 100 bila kujali rangi au eneo analotaka.

Waliomkataa ni Wazanzibar wakimwita Hizbu.

Ndani ya kamati kuu na Halmashauri kuu, wazanzibar waliopo kule ni mapinduzi daima.

Wengi wao wana machungu ya Uharamia wa Mwarabu ndiyo maana wakahamishia hasira zao kwa kila ''chotara'' arudi kwao. Haya hujui, upo Kipumbwi ukila embe ng'ongo

Wanayo pindua pindua ni akina Jecha! Sababu kubwa ni kwamba nchi''imepatikana kwa damu haiwezi kuchukuliwa kwa kipande cha karatasi''

Wanaosema hatyo ni Wazanzibar! Huyajui haya kwasababu fikra zako zimekwama Kipumbwi

Waliokwamisha katiba mpya ni Wazanzibar waliokataa mfumo wa serikali 3.

Mohamed, uliona maandamano ya ''Machotara'' warudi kwao?

Upande mwingine ukiwa na kipili pili si mzanzibar halisi, unatoka Mkuranga au Morogoro

Hayo unayosema wewe ni kuonyesha kuwa Wanzibar wameamua ili kuficha ukweli wa wewe kusema Mapinduzi ni haramu, Zanzibar ilikuwa nzuri wakati wa Sultani

Kwamba Utumwa ni bora tena ule wa Waarabu.

Mohamed mada kama hizi kaa kimya maana utaondoa mashaka kwa wenye shaka
 
Well, Pascal Mayalla, Mag3 na wengine wamekuuliza kitu muhimu sana. Tunaona mabaki ya TransAtlantic Slave trade!
Tuonyeshe wapi uzao wa watu weusi waliopelekwa Uarabuni?
Pili, watumwa walikamatwa iwe walitupiwa mkate au Birian hilo halihalalishi utumwa wao

Mohamed, Waarabu ni wakatili na wabuguzi sana kwa Waafrika.
Hili` nimelishuhudia na ku experience mwenyewe . Fikiria karne moja nyuma

Ni ubaguzi na roho za kikatili ndizo zinawafanya wasithamini wenzao kama Yemeni
Hivyo kutupiwa biria au kufungwa mnyororo miaka 100 iliyopita kwao si issue
Utumwa ni Utumwa tu haijalishia umefanywa na Askofu au Sheikh. Hakuna ushenzi mzuri

Mohamed anachotaka ni kulinganisha utumwa, upi ulikuwa bora.

Unahitaji sana kusoma mambo nje ya kile unachojua. Unahitaji kuijua dunia nje ya Kipumbwi

Huwezi kuweka utumwa katika mizani kwamba wa waarabu ni bora kuliko wazungu
Umefika hapo, sijui ukiwa uarabuni inakuwaje!

Ndio maana nakuambia wewe hujui mambo mengine ya dunia hii kaa kimya, unajianika

Chaguzi tano wananchi wamezungumza, usichojua ni kwamba matokeo ya chauguzi hizo ni kutokana na mgawanyiko. Nilikuuliza nani alimnyima Mzee Ahemd Salim fursa ya Urais?
Salimu alikubalika na Watanganyika 100 bila kujali rangi au eneo analotaka.

Waliomkataa ni Wazanzibar wakimwita Hizbu.

Ndani ya kamati kuu na Halmashauri kuu, wazanzibar waliopo kule ni mapinduzi daima.

Wengi wao wana machungu ya Uharamia wa Mwarabu ndiyo maana wakahamishia hasira zao kwa kila ''chotara'' arudi kwao. Haya hujui, upo Kipumbwi ukila embe ng'ongo

Wanayo pindua pindua ni akina Jecha! Sababu kubwa ni kwamba nchi''imepatikana kwa damu haiwezi kuchukuliwa kwa kipande cha karatasi''

Wanaosema hatyo ni Wazanzibar! Huyajui haya kwasababu fikra zako zimekwama Kipumbwi

Waliokwamisha katiba mpya ni Wazanzibar waliokataa mfumo wa serikali 3.

Mohamed, uliona maandamano ya ''Machotara'' warudi kwao?

Upande mwingine ukiwa na kipili pili si mzanzibar halisi, unatoka Mkuranga au Morogoro

Hayo unayosema wewe ni kuonyesha kuwa Wanzibar wameamua ili kuficha ukweli wa wewe kusema Mapinduzi ni haramu, Zanzibar ilikuwa nzuri wakati wa Sultani

Kwamba Utumwa ni bora tena ule wa Waarabu.

Mohamed mada kama hizi kaa kimya maana utaondoa mashaka kwa wenye shaka
Nguruvi3,
Unazungumza umehamaki.

Ingekuwa hayo usemayo kweli CCM Zanzibar wangekuwa wanashinda uchaguzi.

Isingehitaji kuchukua serikali kwa kufuta uchaguzi.

Haiwezekani Wazanzibari wachague utumwa katika kila uchaguzi.

Wanajua fika kuwa hawana uwezo wa kushinda.

Suala la Salim si jepesi kama unavyodhani.

Amani Karume kachanganya damu na katawala Zanzibar na unajua kilichotokea.

Ati nikae kimya.

Miaka minane nasoma nyaraka za Zanzibar nikiwa msaidizi wa Dr. Ghassany.

Mengine hatukuweka kwa huruma.
 
Nguruvi3,
Unazungumza umehamaki.

Ingekuwa hayo usemayo kweli CCM Zanzibar wangekuwa wanashinda uchaguzi.

Isingehitaji kuchukua serikali kwa kufuta uchaguzi.

Haiwezekani Wazanzibari wachague utumwa katika kila uchaguzi.

Wanajua fika kuwa hawana uwezo wa kushinda.

Suala la Salim si jepesi kama unavyodhani.
Kuna vitu viwili unachanganya. Utumwa na uchaguzi

Utumwa ni uharamaia uliofanywa na Wazungu na Waarabu dhidi ya Waafrika

Huo hauna utetezi wa aina yoyote kwa wanaofikiria vema. Hakuna ushenzi mzuri

Tatizo lako Mohamed, unadhani kulaani Waarabu ni kulaani Uislam.

Hujui tofauti ya vitu hivyo. Uarabu ni asili au unasaba au kabila

Uislam ni imani ya dini ambayo imekuja kupitia kwa Waarabu.

Waliotenda udhalim wa utumwa ni Waarabu ambao wali practice Uislam.

Siyo Uislam uliosababisha biashara ya utumwa. Tofautisha hapo

Hivyo Sultani alitenda kama Mwarabu na kama alitumia Uislam basi ni kwa manufaa yake lakini hilo halikuwa takwa la Uislam kama dini.

Kuhusu chaguzi, matokeo ya chaguzi yanakwazwa na Wazanzibar wenyewe.

Laiti wangekuwa na msimamo mmoja kama Umma, hakuna kitu kingewakwamisha

Nimekuuliza, unajua maana ya ''machotara'' warudi kwao?
Unajua kipili pili cha kichwani na Mkuranga na Morogoro?

Kisa cha Salim Ahmed, kaa kimya Mohamed huko usiende kabisa, wewe elekea Kipumbwi

Hizi siasa za Kitaifa na Kimataifa tafadhali jieupushe nazo, endelea na Kipumbwi

Ni hivi Mpinduzi Daima na Zanzibar ya Sultani yamebaki kuwa makovu makubwa ya siasa za Zanzibar na wala hayapona katika miaka ya karibuni.

Mateso ya kusimama katika milango kusbiri leftover za Biriani walioshuhudia hayo wapo hai
 
Nguruvi3, huyu mtu anayejiita Mohamed Said ni mtu wa hatari sana katika mustakhabali wa taifa hili. Alianza kwa kupotosha historia ya Tanganyika akidai walowezi Wakizulu na Manyema ndio walipigania uhuru wa Tanganyika. Huo upotoshaji akawa na jeuri ya kuuita eti historia ya kweli!

Naona baada ya kuwateka baadhi ya vijana waliomeza hizo ngano zake, sasa kahamia Unguja. Huko nako anataka kuwainua walowezi wa Kiarabu waonekane kama ndio wazalendo kuliko wazawa waliopitia mateso makubwa mikononi mwa hao Waarabu!

Mpaka sasa swali la kujiuliza ni nini lengo la huyu mchochezi kwa kujaribu kupandikiza chuki kwa anachodai historia ya kweli? Sina shaka kwamba mapinduzi yaliyomfungasha virago Sultani kwake yeye yalikuwa haramu. Huyu ni mtu wa kuogopwa kama ukoma.
Naunga mkono hoja, tena ni afadhali humu jf anafanya kuandika tuu, hivyo there is a room ya kumkosoa anapoleta maurongo humu, lakini anapokaribishwa kwenye redio zao, urongo wake huenea bila room ya critics, wasikilizaji wake wanameza mazima maxima, hivyo nimeishawahi kutoa angalizo hili kumhusu mtu huyu


P
 
Back
Top Bottom