Kwanini historia ya Zanzibar ya kweli haisomeshwi?

Kwanini historia ya Zanzibar ya kweli haisomeshwi?

''Kwanini historia ya kweli ya Zanzibar haisomeshwi''

Hoja: Historia ya kweli inaandikwa na kuthibitishwa na nani?

Pascal Mayalla JokaKuu
Nguruvi3,
''Hoja: Historia ya kweli inaandikwa na kuthibitishwa na nani?''
Umeuliza swali.

Ukweli na uongo hauna shida kujulikana hata na akili ndogo.
Ni ipi historia ya kweli ya Zanzibar?

Historia ya Zanzibar inafahamika na maarufu ni historia ya mapinduzi na ndiyo kwa sasa imetiliwa mkazo na kwa hakika ndiyo historia rasmi.

Lakini ipo historia nyingine ambayo ni historia hiyo hiyo ya mapinduzi lakini haikuwa inafahamika.

Nimeandika mengi katika historia ya Zanzibar na nimezungumza katika radio na tv kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar.

Nimeshiriki kama Mtafiti Msaidizi katika uandishi wa kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Sababu ya mimi kuhusika na uandishi wa kitabu hiki ni kuwa nilikutana na mwandishi nyumbani kwake Muscat na katika mazungumzo akanieleza kuwa ana nia ya kuandika kitabu cha historia ya Zanzibar.

Nikamshauri aje Tanga azungumze na mzee mmoja anaitwa Mohamed Omari Mkwawa yeye ana mengi katika historia ya mapinduzi.

Hii ilikuwa mwaka wa 1999.

Baada ya kiasi cha miaka minne Dr. Ghassany akafika Tanga na nikamkutanisha na Mzee Mkwawa maarufu kwa jina la ''Tindo,'' jina ambalo alipewa na Mzee Karume wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar katika miaka ya 1950s.

Sikushiriki katika mazungumzo ya kwanza ya Dr, Ghassany na Mzee Mkwawa lakini Dr. Ghassany akaniambia maneno haya baada ya mazungumzo yao, ''Nimepita katika kila maktaba Marekani na Uingereza nikitafiti historia ya mapinduzi lakini maneno niliyosikia kutoka kwa Mzee Mkwawa sijakutananayo mahali popote.

Ufunguo wa kitabu changu anao Mzee Mkwawa.''

Kitu kipi ambacho Dr. Ghassany anasema hakupata kukisoma popote katika maktaba zilizohifadhi nyaraka za Zanzibar huko Marekani na Uingereza?

Hii ilikuwa historia ya kambi ya Kipumbwi kijiji cha uvuvi pembeni ya Bahari ya Hindi jirani ya shamba la mkonge la Sakura Tanga ambako iliwekwa kambi ya mamluki wa Kimakonde wafanyakazi wa mashamba ya mkonge ambao walipewa mafunzo na kisha kuvushwa kwenda Zanzibar kuipigia kura ASP mwaka wa 1963 na mwaka wa 1964 kushiriki katika mapinduzi.

Hawa Wamakonde waliua Waarabu wengi sana mjini na mashamba.

Viongozi wakuu wa kambi hii walikuwa Victor Mkello kiongozi wa chama cha wakata mkonge na Mohamed Omari Mkwawa.

Regional Commssioner wa Tanga alikuwa Jumanne Abdallah na District Commissioner wake alikuwa Ali Mwinyi Tambwe.

Yako mengi lakini tusimame hapa.

Hutosoma popote katika historia ya Zanzibar kuhusu jeshi hili la mamluki katika ardhi ya Tanganyika lililovamia Zanzibar kupindua serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.

Kila aliyehojiwa Zanzibar kuhusu kambi hii anasema hana taarifa nayo.
Utakachoelezwa ni kuwa mapinduzi yalifanywa na vijana wa ASP na utaelezwa na ushirikiwa Umma Party, makomredi katika mapinduzi.

Hutosikia kabisa historia ya Wamakonde kutoka Kipumbwi waliovushwa Zanzibar kuja kusaidia mapigano.

Swali limeulizwa.
''Historia ya kweli inaandikwa na kuthibitishwa na nani?''

Nani wa kujibu swali hili?

1575000307952.png

Mohamed Omari Mkwawa akionyesha kitabu cha Dr.. Harith Ghassany
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru''

Hii mada inajirudia kwa mtindo mwingine lakini mantiki yake ni ile ile ya Mohamed Said kutaka jambo lieleweke kwa mtazamo wake na pengine kwasababu nyingine

Utumwa ni ''human rights abuse'' kubwa katika historia ya maisha ya mwanadamu

Bila kujali imefanywa na Wazungu au Waarabu, utumwa ni utumwa na ni haramu tu

Pale Ghana kuna ''Door of no return'' kuelekea baharini kwa safari ya utumwa

Juu ya Door of no return kuna kanisa lililowaombea watumwa kwa safari yao
Yaani kanisa halikuzuia uhalifu bali lilitoa ''baraka'' kwa maombezi ya ''victims''

Ndivyo Waarabu walivyofanya pia kwa kuwa na soko la watumwa huku wakisali kabla ya kuwaingiza majahazini kwa safari. Yaani swala kwa ajili ya safari salama ya watumwa

Tofauti inakuja namna ya ku ''acknowledge'' uharamu wa biashara hiyo

Wazungu wanasema wazi walifanya na wanaonyesha. Waarabu hawasemi

Wazungu waliacha mabaki ya Watumwa ambao yapo,Waarabu hatujui watumwa waliishaje

Kwa hoja ya Zanzibar Mohamed Said anasema Mapinduzi yale yalikuwa na mkono wa Nyerere pengine katika kuundama Uislam kwa mantiki yake.

Wazanzibar wenyewe wamegawayika, wale wa mapinduzi daima, na wale wa mapinduzi dhulma

Hoja ambayo tumemuuliza Mohamed kwa muda mrefu na asiyotaka kuifafanua kama si kuitolea majibu ni je, mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa halali au yalikuwa haramu?

Labda katika mada hii atakuja na jibu, vinginevyo tutaishia na habari za Kipumbwi

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Mkuu acha kuzunguka mbuyu katika kuwatetea waarabu waliokuwa wafadhili wa utumwa.
Wafadhili wa utumwa hawatarudi tena Zanzibar wala pande hizi za Afrika.

Zanzibar baada ya 1964........Never, and never again will the arabs be left to return.
This is a wrong mentality, asili ya mtu au rangi ya mtu isitumike kamhukumu bila kosa lolote. Hao unaowaita Arabs wa Zanzibar, Arabs ni asili yao tuu lakini ni Wazanzibari.

Ni kufuatia sentiments kama hizi kwa Zanzibar iliyofanya Mapinduzi Matukufu kumfurusha Sultan ile 1964 na kauli kama "Mapinduzi Daima", kunapelekea kuna mtu mwenye asili ya Kiarabu, ni Mpemba, kila siku anashinda kwa kura kihalali katika uchaguzi lakini watangazwe!, kisa 'Mwarabu'!.
This is not fair hata kidogo.

Kuna Wamatumbi wenzetu, ni makaburu kuliko hata makaburu wenyewe na kuna Wazungu, Wahindi na Waarabu ni wazalendo kuliko wazawa wenyewe wa asili na mifano ipo, kina Amiri Jamal, Alnoor Kasum, Dr. Leader Starring, etc, makaburu naomba kuwahifadhi.

Naombeni sana tusitetee sentiments za kibaguzi, hata humu jf, kuna members wenye vinasaba vya Kiarabu wanajiona bora sana, wanayadharau yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuyaita ni mauaji ya kimbari kisa tuu ni uarabu wao, huku walinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kauli za "Mapinduzi Daima" wakijiapiza Mwarabu kamwe hatorejea Zanzibar, sii haki.
P
 
Hii mada inajirudia kwa mtindo mwingine lakini mantiki yake ni ile ile ya Mohamed Said kutaka jambo lieleweke kwa mtazamo wake na pengine kwasababu nyingine

Utumwa ni ''human rights abuse'' kubwa katika historia ya maisha ya mwanadamu

Bila kujali imefanywa na Wazungu au Waarabu, utumwa ni utumwa na ni haramu tu

Pale Ghana kuna ''Door of no return'' kuelekea baharini kwa safari ya utumwa

Juu ya Door of no return kuna kanisa lililowaombea watumwa kwa safari yao
Yaani kanisa halikuzuia uhalifu bali lilitoa ''baraka'' kwa maombezi ya ''victims''

Ndivyo Waarabu walivyofanya pia kwa kuwa na soko la watumwa huku wakisali kabla ya kuwaingiza majahazini kwa safari. Yaani swala kwa ajili ya safari salama ya watumwa

Tofauti inakuja namna ya ku ''acknowledge'' uharamu wa biashara hiyo

Wazungu wanasema wazi walifanya na wanaonyesha. Waarabu hawasemi

Wazungu waliacha mabaki ya Watumwa ambao yapo,Waarabu hatujui watumwa waliishaje

Kwa hoja ya Zanzibar Mohamed Said anasema Mapinduzi yale yalikuwa na mkono wa Nyerere pengine katika kuundama Uislam kwa mantiki yake.

Wazanzibar wenyewe wamegawayika, wale wa mapinduzi daima, na wale wa mapinduzi dhulma

Hoja ambayo tumemuuliza Mohamed kwa muda mrefu na asiyotaka kuifafanua kama si kuitolea majibu ni je, mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa halali au yalikuwa haramu?

Labda katika mada hii atakuja na jibu, vinginevyo tutaishia na habari za Kipumbwi

JokaKuu Pascal Mayalla
Nguruvi 3,
Sijui kwa nini unasema kuwa nataka historia ya mapinduzi ifahamike nitakavyo mie.
Mimi nachangia fikra zangu kama wanavyochangia watu wengine.

Sikulazimishi uamini yaliyotokea Kipumbwi na kwa kunitwisha mimi mzigo wa Kipumbwi ni kunionea.

Walioweka kambi Kipumbwi sasa wanafahamika la kama unaona huu ni uzushi kwangu sawa hatuwezi kuvutana kwa hilo.

Hilo la uhalali wa mapinduzi hata wewe unaweza kujibu kwa kadri akili yako inavyokueleza.
Sijui kwa nini unashikilia mimi ndiye nijibu swali hilo.

Huu ni ukumbu huru na wazi yeyote anaweza kuchangia mawazo yake bila bugdha.
 
Mohamed Said rejea bandiko# 81.
Nilipoulizwa swali, nani anatakiwa kuandika historia ya kweli na nani anatakiwa kuthibitisha kuna mantiki ndani yake.

Kwa mtazamo wako historia uliyoandika na Gessany kwa kumtumia mzee Mkwawa ndiyo ya kweli na inapaswa kusomeshwa.

Historia ni mtiririko wa matukio kwa kufuata nyakati.

Ni nadra sana kusoma mahali penye historia iliyokamilika 100%.
Hii inatokana na ukweli kuwa vyanzo vinatofautiana na hata kuongozwa na mtazamo binafsi.

Historia ya Zanzibar haindikwi bila kujua tofauti za rangi! kidonda hicho hakijapona
Hivi wanaosema ''machotara'' waondoke, unategemea waandike historia kwa mtazamo upi

Na wale wanaosema Zanzibar ilikuwa ''pepo'' kabla ya 1964 unategemea waandike nini kuhusu historia ya Zanzibar

Huko Oxford na Cambridge uhistoria ya Uingereza inashangaza maana kila kitabu kina jambo pengine usililojua. Ipo historia ya watu, wafalme,vita, matukio n.k.

Kwa wenzetu historia haisomeshwi na kitabu kimoja, bali mkusanyiko wa references

Ukisikia mtu amesoma kitabu kimoja na kujua historia fulani,jiulize sana kuhusu mtu huyo

Hapa Zanzibar historia pia ina matatizo kama sehemu nyingine.

Ukisoma habari za Abdurahman Babu, Karume na John Okello unaweza usijue nani hasa kiongozi wa mapinduzi ya 1964

Harith anayeishi Muscat usitegemee akueleza jambo linalomhusu Okello au Babu kwa usahihi wa asilimia zote.

Wala Mzee Mkwawa hakamilishi historia nzima bila kujua sehemu nyingine

Nini hoja yangu?

Kwamba simulizi moja la Mzee Mkwawa na Harith akishirikiana na Mohamed haliwezi kuwa historia ya ukweli, na wala hawawezi kuwa ndio wanaothibitisha historia ya Zanzibar.

Simulizi lao linaweza kuwa sehemu ya historia kwakushirikiana na historia nyingine zinazoeleza matukio na muda na hata kushabihina.

Ni makosa kutumia maneno ''historia ya ukweli'' . Historia ukamilifu si kitu chepesi, unajua hilo
 
Udhalimu haukuanzwa na Waarabu Unguja wala Pemba bali ni Ukristo ndio ulioanza.Mwanzo wa uvamizi katika visiwa hivi umetokana na uvamizi wa Wakristo kutoka Ureno na kwa amri ya Papa Nicholas V kwa kumuagiza mfalme Alfonso aliekuwa akiwatumikia Wareno Barani Afrika. Maagizo ya Papa ni haya hapa. " Tuna mruhusu na tunamtuma kwa kumpa uhuru wote Mfalme Alfonso wa kuwashinda na kuwakamata na kuwapiga vita na kuwafanya watii amri zetu Waarabu Waislamu na Wapagani na maaduwi wote wa Ukristo popote pale walipo. Na kukamata nchi zao, Falme zao, Mali yao, Ardhi zao, na utajiri wao wote walionao na kuwaingiza katika Utumwa wa daima. "
 
Hilo la uhalali wa mapinduzi hata wewe unaweza kujibu kwa kadri akili yako inavyokueleza.
Sijui kwa nini unashikilia mimi ndiye nijibu swali hilo.
Kuntu! sasa kama huwezi kueleza hilo, utasomeshaje historia ya Ukweli?
Ukweli hauna ''grey area'' ni ima black or white

Ninashikilia hivyo kwasababu unaaminisha vijana wadogo waamini mapinduzi ni haramu yalifanywa na wasio wazanzibar. Hakuna shida katika mawazo huru!
Hata hivyo ni vema ukawa muwazi kuliko kubabaisha baisha na kuacha vijana njia panda

Ni ima unayaona mapinduzi ni halali, au unayaona ni haramu
Hakuna cha kitendawili, Nyerere au Kipumbwi.

Ndio msingi wa kukuuliza, kuhusu mapinduzi ya Zanzibar wewe una mtazamo gani na upo upande upi? Kama hujui unasimama wapi, unakwenda kusomesha ukweli wa historia ipi?
 
This is a wrong mentality, asili ya mtu au rangi ya mtu isitumike kamhukumu bila kosa lolote. Hao unaowaita Arabs wa Zanzibar, Arabs ni asili yao tuu lakini ni Wazanzibari.

Ni kufuatia sentiments kama hizi kwa Zanzibar iliyofanya Mapinduzi Matukufu kumfurusha Sultan ile 1964 na kauli kama "Mapinduzi Daima", kunapelekea kuna mtu mwenye asili ya Kiarabu, ni Mpemba, kila siku anashinda kwa kura kihalali katika uchaguzi lakini watangazwe!, kisa 'Mwarabu'!.
This is not fair hata kidogo.

Kuna Wamatumbi wenzetu, ni makaburu kuliko hata makaburu wenyewe na kuna Wazungu, Wahindi na Waarabu ni wazalendo kuliko wazawa wenyewe wa asili na mifano ipo, kina Amiri Jamal, Alnoor Kasum, Dr. Leader Starring, etc, makaburu naomba kuwahifadhi.S
iku
Naombeni sana tusitetee sentiments za kibaguzi, hata humu jf, kuna members wenye vinasaba vya Kiarabu wanajiona bora sana, wanayadharau yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuyaita ni mauaji ya kimbari kisa tuu ni uarabu wao, huku walinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kauli za "Mapinduzi Daima" wakijiapiza Mwarabu kamwe hatorejea Zanzibar, sii haki.
P
Paschal,
Umeniongezea kitu sikujua kuwa kuna Waarabu wanahamu kubwa ya kuishi Zanzibar.

Kiasi wapapende nchi nzuri sana barabara za kisasa, majumba mazuri na maendeleo usiseme mahospitali shule za kupendeza mabiashara makubwa makampuni yote ya dunia yapo hapo.

Mashopping Mall yaliyojaza kila ukifikiriacho.

Arabuni dhiki kubwa wacha watamani kubadilisha pasipoti zao wachukue za huku kwetu waje kula raha wanazokula Wazanzibari.

Oman kumejaa vibaka ukianika shati uani hulikuti na mwizi akikamatwa ni kibiriti tu hata kama shati limepatikana.

Sikwambii washawasha na mazombie.
Ilimuradi dhiki, hofu, jasho na vumbi.
 
Kuntu! sasa kama huwezi kueleza hilo, utasomeshaje historia ya Ukweli?
Ukweli hauna ''grey area'' ni ima black or white

Ninashikilia hivyo kwasababu unaaminisha vijana wadogo waamini mapinduzi ni haramu yalifanywa na wasio wazanzibar. Hakuna shida katika mawazo huru!
Hata hivyo ni vema ukawa muwazi kuliko kubabaisha baisha na kuacha vijana njia panda

Ni ima unayaona mapinduzi ni halali, au unayaona ni haramu
Hakuna cha kitendawili, Nyerere au Kipumbwi.

Ndio msingi wa kukuuliza, kuhusu mapinduzi ya Zanzibar wewe una mtazamo gani na upo upande upi? Kama hujui unasimama wapi, unakwenda kusomesha ukweli wa historia ipi?
Nguruvi3,
Nimekujibu kuwa naeleza niyajuayo kama mtu mwingine yeyote yule wala si lazima uamini unaweza kusoma ukapita.

Hulka yangu si ya kubishana kwani katika kubishana hakuna tija.

Tija ni kueneza kile ukijuacho na msomaji ana uhuru wake wa kuamini au vinginevyo au akajazie elimu zaidi na sote tukafaidika.

Kama hivi historia ya Kipumbwi, Tindo na Victor Mkello.

Hamkuwa mnayajua haya lakini ni sehemu ya historia ya mapinduzi.

Haya huyapati katika ubishi.
 
Paschal,
Umeniongezea kitu sikujua kuwa kuna Waarabu wanahamu kubwa ya kuishi Zanzibar.

Kiasi wapapende nchi nzuri sana barabara za kisasa, majumba mazuri na maendeleo usiseme mahospitali shule za kupendeza mabiashara makubwa makampuni yote ya dunia yapo hapo.

Mashopping Mall yaliyojaza kila ukifikiriacho.

Arabuni dhiki kubwa wacha watamani kubadilisha pasipoti zao wachukue za huku kwetu waje kula raha wanazokula Wazanzibari.

Oman kumejaa vibaka ukianika shati uani hulikuti na mwizi akikamatwa ni kibiriti tu hata kama shati limepatikana.

Sikwambii washawasha na mazombie.
Ilimuradi dhiki, hofu, jasho na vumbi.
Mohamed hii inaitwa Pervert.
Hoja ya Pascal Mayalla ipo wazi

Kwamba, Waarabu waliozaliwa Zanzibar ni Wazanzibar na wana haki kama Wazanzibar
Kuwafanyia inda kwa rangi si jambo jema.
Wazanzibar kipipili ni Wazanzibar, kuwaita Warufiji si kuwatendea haki

Anachosema rangi istumike kumhukumu mtu kama nimemuelewa
 
Hii mada inajirudia kwa mtindo mwingine lakini mantiki yake ni ile ile ya Mohamed Said kutaka jambo lieleweke kwa mtazamo wake na pengine kwasababu nyingine

Utumwa ni ''human rights abuse'' kubwa katika historia ya maisha ya mwanadamu

Bila kujali imefanywa na Wazungu au Waarabu, utumwa ni utumwa na ni haramu tu

Wazungu waliacha mabaki ya Watumwa ambao yapo,Waarabu hatujui watumwa waliishaje
?
Labda katika mada hii atakuja na jibu, vinginevyo tutaishia na habari za Kipumbwi

JokaKuu Pascal Mayalla
Mkuu Nguruvi3, mambo ya maskani Kipumbwi ni mastori tuu ya town. Alichoandika Ghasani nyingi ni hearsay tuu, wakati wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, BBC Swahili walitoa 5 Series za Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwahoji walioshiriki Mapinduzi physically sio kwa kuhadithiwa kama mastori ya Maalim Mohammed Said na Ghasani.

Hili la watumwa wa Trans Atlantic Slave Trade walipelekwa Europe na America, hawa wali survive na walizaana na kuongezaka biashara ilipositishwa walipewa fursa ya kurejea Africa, Watumwa wa America walirejeshwa Liberia, Watumwa wa Europe walirejeshwa Sierra Leone.

Watumwa wa India Ocean Slave Trade ambao soko kuu ndio lilikuwa Zanzibar, walipelekwa Arabuni na India, walipofika tuu, kitu cha kwanza ni Watumwa wanaume wote walihasiwa!. Hivyo hakuna mazalia ya Watumwa wa soko la Zanzibar, machotara wa kule ni matokeo ya wajakazi kubakwa, waliposhika ujauzito wenye bahati walufanywa masuriya, wasio na bahati waliuliwa kwa kutobolewa matumbo.

P
 
Nguruvi3,
Nimekujibu kuwa naeleza niyajuayo kama mtu mwingine yeyote yule wala si lazima uamini unaweza kusoma ukapita.

Hulka yangu si ya kubishana kwani katika kubishana hakuna tija.

Tija ni kueneza kile ukijuacho na msomaji ana uhuru wake wa kuamini au vinginevyo au akajazie elimu zaidi na sote tukafaidika.

Haya huyapati katika ubishi.
Kuna ubishi waaina mbili, wa kijinga na wa kiweledi.
Hutaki kueleza kuhusu mapinduzi unataka watu wameze tu habari za kipumbwi
Hapana Mohamed, kuna watakao kaa jamvini wakisikiliza wakiitika hewala

Baadhi yao hawapo katika kundi hilo, wana macho mang'avu

Je, mapinduzi ya Zanzibar ni halali au ni haramu?
 
Mkuu Nguruvi3, mambo ya maskani Kipumbwi ni mastori tuu ya town. Alichoandika Ghasani nyingi ni hearsay tuu, wakati wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, BBC Swahili walitoa 5 Series za Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwahoji walioshiriki Mapinduzi physically sio kwa kuhadithiwa kama mastori ya Maalim Mohammed Said na Ghasani.
I mean ngano tuuu ! hapana inafika mahali tuwaonee huruma vijana wadogo
Mag3 mkubwa kuna jingine la kusomeshwa huku
 
Paschal,
Umeniongezea kitu sikujua kuwa kuna Waarabu wanahamu kubwa ya kuishi Zanzibar.

Kiasi wapapende nchi nzuri sana barabara za kisasa, majumba mazuri na maendeleo usiseme mahospitali shule za kupendeza mabiashara makubwa makampuni yote ya dunia yapo hapo.

Mashopping Mall yaliyojaza kila ukifikiriacho.

Arabuni dhiki kubwa wacha watamani kubadilisha pasipoti zao wachukue za huku kwetu waje kula raha wanazokula Wazanzibari.

Oman kumejaa vibaka ukianika shati uani hulikuti na mwizi akikamatwa ni kibiriti tu hata kama shati limepatikana.

Sikwambii washawasha na mazombie.
Ilimuradi dhiki, hofu, jasho na vumbi.
Aliyetoka Omani akaihamishia sultanate yake kutoka Oman kuja Zanzibar, ni nani?. Ni Mmatumbi yule?. Kisa cha kuhamia Oman kuhamia Zanzibar ni nini?. Zanzibar ni kwao?. Alipokuja hakuwakuta wenyeji Wamatumbi wenye visiwa vyao?. Jee unajua aliwafanya nini kina Mwinyi Mkuu waliomkaribisha Sultan Zanzibar?.

Mambo mengine tuyaache tuu tusitonyeshe vidonda.

Mambo ya Zanzibar tuwaachie wenyewe, sisi huku tuendelee kuhifadhi historia ya babu zetu iliyosahaulika.
P
 
Kuna ubishi waaina mbili, wa kijinga na wa kiweledi.
Hutaki kueleza kuhusu mapinduzi unataka watu wameze tu habari za kipumbwi
Hapana Mohamed, kuna watakao kaa jamvini wakisikiliza wakiitika hewala

Baadhi hawao katika kundi hilo

Je, mapinduzi ya Zanzibar ni halali au ni haramu?
Nguruvi3,
Hapana usiamini chochote kuhusu Kipumbwi narudia kukueleza.

Hii Kipumbwi haipo popote katika historia ya mapinduzi.

Hili si tatizo kwangu.

Nafurahi kuwa nilishiriki katika kuieleza historia hii.

Kuhusu mapinduzi nina mengi sana:

Hii ni baadhi ya mchango wangu katika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Nina pia personal recollections za udogoni za marafiki wawili wa baba yangu Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala waliouliwa baada ya mapinduzi.
 
Aliyetoka Omani akaihamishia sultanate yake kutoka Oman kuja Zanzibar, ni nani?. Ni Mmatumbi yule?. Kisa cha kuhamia Oman kuhamia Zanzibar ni nini?. Zanzibar ni kwao?. Alipokuja hakuwakuta wenyeji Wamatumbi wenye visiwa vyao?. Jee unajua aliwafanya nini kina Mwinyi Mkuu waliomkaribisha Sultan Zanzibar?.

Mambo mengine tuyaache tuu tusitonyeshe vidonda.

Mambo ya Zanzibar tuwaachie wenyewe, sisi huku tuendelee kuhifadhi historia ya babu zetu iliyosahaulika.
P
P,
Historia inasema Oman ilikuja kuwatoa Wareno Zanzibar.

Naamini unawajua vyema Wareno.
 
I mean ngano tuuu ! hapana inafika mahali tuwaonee huruma vijana wadogo
Mag3 mkubwa kuna jingine la kusomeshwa huku
Nguruvi3,
Sijawasikia hao unaowahurumia wakilalamika kuwa hawapendi kunisoma.

Mimi nakuhurumia wewe kwa kujua kuwa unazungumza kitu usichokijua.

Kila nikitia mguu Zanzibar huwa naombwa kuzungumza:

1575006460688.png

Radio Mtoni Zanzibar
Kipindi Maalum

P,
Historia inasema Oman ilikuja kuwatoa Wareno Zanzibar.
Naamini unawajua vyema Wareno.
Ni kweli Mwarabu aliombwa na wenyeji chini ya Mwinyi Mkuu, kuja kuwasaidia Wamatumbi dhidi ya uvamizi wa Wareno, na kweli Mwarabu akaitika wito akaleta usaidizi na Mreno akaondoshwa.

Jee baada ya hapo unakijua alichokifanya Mwarabu kwa Mwinyi Mkuu?. Ile ya 1964 ndio malipo yake, kazi ile tukufu imefanywa na Wamatumbi. Visiwa vya Zanzibar mwanzo vilikuwa vya Wamatumbi, kutokana na mwingiliano na Waarabu na Wahindi sasa Zanzibar ni cosmopolitan, Wamatumbi, Waarabu, Wahindi na Machotara idadi kubwa ikiwa ni Washirazi na Wapemba.

Zile hostilities za Walichowafanya Waarabu, zimelipizwa ile 1964. Kwavile aliyepinduliwa ile 1964 ni Mzanzibari na aliyepindua pia ni Mzanzibari, sasa mpindua na mpinduliwa they should be one, wote ni Wazanzibari, akitokea Mwarabu au Mpemba kashinda, apewe tuu ushindi wake awe, na sio kumpoka kwasababu ya Uarabu wake au Upemba wake, lakini ili apewe ni lazima itakubali kuyaheshimu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuimba kibwaguzo cha "Mapinduzi Daima", chini ya hapo Wamatumbi walioikomboa nchi yao dhidi ya ukoloni wa Waarabu walowezi, hawatakubali Mwarabu arudi, na ndio maana mara tuu baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, waliikabidhi Zanzibar chini ya ulinzi wa Wamatumbi wenzao wa Bara na kuungana, sasa tumekuwa kitu kimoja, Mwarabu kamwe hawezi kurudi tena, ila Mzanzibari mwenye asili ya Kiarabu, rukhsa.
P
 
I mean ngano tuuu ! hapana inafika mahali tuwaonee huruma vijana wadogo
Mag3 mkubwa kuna jingine la kusomeshwa huku
Nguruvi3, huyu mtu anayejiita Mohamed Said ni mtu wa hatari sana katika mustakhabali wa taifa hili. Alianza kwa kupotosha historia ya Tanganyika akidai walowezi Wakizulu na Manyema ndio walipigania uhuru wa Tanganyika. Huo upotoshaji akawa na jeuri ya kuuita eti historia ya kweli!

Naona baada ya kuwateka baadhi ya vijana waliomeza hizo ngano zake, sasa kahamia Unguja. Huko nako anataka kuwainua walowezi wa Kiarabu waonekane kama ndio wazalendo kuliko wazawa waliopitia mateso makubwa mikononi mwa hao Waarabu!

Mpaka sasa swali la kujiuliza ni nini lengo la huyu mchochezi kwa kujaribu kupandikiza chuki kwa anachodai historia ya kweli? Sina shaka kwamba mapinduzi yaliyomfungasha virago Sultani kwake yeye yalikuwa haramu. Huyu ni mtu wa kuogopwa kama ukoma.
 
Ni kweli Mwarabu aliombwa na wenyeji chini ya Mwinyi Mkuu, kuja kuwasaidia Wamatumbi dhidi ya uvamizi wa Wareno, na kweli Mwarabu akaitika wito akaleta usaidizi na Mreno akaondoshwa.

Jee baada ya hapo unakijua alichokifanya Mwarabu kwa Mwinyi Mkuu?. Ile ya 1964 ndio malipo yake, kazi ile tukufu imefanywa na Wamatumbi. Visiwa vya Zanzibar mwanzo vilikuwa vya Wamatumbi, kutokana na mwingiliano na Waarabu na Wahindi sasa Zanzibar ni cosmopolitan, Wamatumbi, Waarabu, Wahindi na Machotara idadi kubwa ikiwa ni Washirazi na Wapemba.

Zile hostilities za Walichowafanya Waarabu, zimelipizwa ile 1964. Kwavile aliyepinduliwa ile 1964 ni Mzanzibari na aliyepindua pia ni Mzanzibari, sasa mpindua na mpinduliwa they should be one, wote ni Wazanzibari, akitokea Mwarabu au Mpemba kashinda, apewe tuu ushindi wake awe, na sio kumpoka kwasababu ya Uarabu wake au Upemba wake, lakini ili apewe ni lazima itakubali kuyaheshimu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuimba kibwaguzo cha "Mapinduzi Daima", chini ya hapo Wamatumbi walio nchi yao dhidi ya ukoloni wa Waarabu walowezi, hawatakubali Mwarabu arudi, na ndio maana mara tuu baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, waliikabidhi Zanzibar chini ya ulinzi wa Wamatumbi wenzao wa Bara na kuungana, sasa tumekuwa kitu kimoja, Mwarabu kamwe hawezi kurudi tena, ila Mzanzibari mwenye asili ya Kiarabu, rukhsa.
P
Paschal,
Sina tatizo na historia hiyo.
Ipo na hakuna wa kuifuta.

Lakini ipo na historia nyingine pia.
 
Back
Top Bottom