Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #81
Nguruvi3,''Kwanini historia ya kweli ya Zanzibar haisomeshwi''
Hoja: Historia ya kweli inaandikwa na kuthibitishwa na nani?
Pascal Mayalla JokaKuu
''Hoja: Historia ya kweli inaandikwa na kuthibitishwa na nani?''
Umeuliza swali.
Ukweli na uongo hauna shida kujulikana hata na akili ndogo.
Ni ipi historia ya kweli ya Zanzibar?
Historia ya Zanzibar inafahamika na maarufu ni historia ya mapinduzi na ndiyo kwa sasa imetiliwa mkazo na kwa hakika ndiyo historia rasmi.
Lakini ipo historia nyingine ambayo ni historia hiyo hiyo ya mapinduzi lakini haikuwa inafahamika.
Nimeandika mengi katika historia ya Zanzibar na nimezungumza katika radio na tv kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar.
Nimeshiriki kama Mtafiti Msaidizi katika uandishi wa kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''
Sababu ya mimi kuhusika na uandishi wa kitabu hiki ni kuwa nilikutana na mwandishi nyumbani kwake Muscat na katika mazungumzo akanieleza kuwa ana nia ya kuandika kitabu cha historia ya Zanzibar.
Nikamshauri aje Tanga azungumze na mzee mmoja anaitwa Mohamed Omari Mkwawa yeye ana mengi katika historia ya mapinduzi.
Hii ilikuwa mwaka wa 1999.
Baada ya kiasi cha miaka minne Dr. Ghassany akafika Tanga na nikamkutanisha na Mzee Mkwawa maarufu kwa jina la ''Tindo,'' jina ambalo alipewa na Mzee Karume wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar katika miaka ya 1950s.
Sikushiriki katika mazungumzo ya kwanza ya Dr, Ghassany na Mzee Mkwawa lakini Dr. Ghassany akaniambia maneno haya baada ya mazungumzo yao, ''Nimepita katika kila maktaba Marekani na Uingereza nikitafiti historia ya mapinduzi lakini maneno niliyosikia kutoka kwa Mzee Mkwawa sijakutananayo mahali popote.
Ufunguo wa kitabu changu anao Mzee Mkwawa.''
Kitu kipi ambacho Dr. Ghassany anasema hakupata kukisoma popote katika maktaba zilizohifadhi nyaraka za Zanzibar huko Marekani na Uingereza?
Hii ilikuwa historia ya kambi ya Kipumbwi kijiji cha uvuvi pembeni ya Bahari ya Hindi jirani ya shamba la mkonge la Sakura Tanga ambako iliwekwa kambi ya mamluki wa Kimakonde wafanyakazi wa mashamba ya mkonge ambao walipewa mafunzo na kisha kuvushwa kwenda Zanzibar kuipigia kura ASP mwaka wa 1963 na mwaka wa 1964 kushiriki katika mapinduzi.
Hawa Wamakonde waliua Waarabu wengi sana mjini na mashamba.
Viongozi wakuu wa kambi hii walikuwa Victor Mkello kiongozi wa chama cha wakata mkonge na Mohamed Omari Mkwawa.
Regional Commssioner wa Tanga alikuwa Jumanne Abdallah na District Commissioner wake alikuwa Ali Mwinyi Tambwe.
Yako mengi lakini tusimame hapa.
Hutosoma popote katika historia ya Zanzibar kuhusu jeshi hili la mamluki katika ardhi ya Tanganyika lililovamia Zanzibar kupindua serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.
Kila aliyehojiwa Zanzibar kuhusu kambi hii anasema hana taarifa nayo.
Utakachoelezwa ni kuwa mapinduzi yalifanywa na vijana wa ASP na utaelezwa na ushirikiwa Umma Party, makomredi katika mapinduzi.
Hutosikia kabisa historia ya Wamakonde kutoka Kipumbwi waliovushwa Zanzibar kuja kusaidia mapigano.
Swali limeulizwa.
''Historia ya kweli inaandikwa na kuthibitishwa na nani?''
Nani wa kujibu swali hili?
Mohamed Omari Mkwawa akionyesha kitabu cha Dr.. Harith Ghassany
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru''