Kwanini homework za Wanafunzi zinafanywa na Wazazi? Punguzeni ujuaji

Kwanini homework za Wanafunzi zinafanywa na Wazazi? Punguzeni ujuaji

Wenyewe waalimu hutuambia kwamba kila jambo lifanyike kwa wakati wake na hiyo ndo nidhamu ktk.maisha. Iweje sasa wanavuruga? e.g. Tulipe ada, tuwasaidie kwa ulazima/shinikizo kufundisha halafu mwisho wa siku wanachukua Credit kama watoto wakifaulu vizuri mitihani. Watoto wakifurunda lawama zinaelekezwa kwa wazazi eti wazazi hawatoi ushirikiano. Hiyo sio sawa.
Well said mkuu
 
... Mtakesha na ataishia kulala unabaki na msala na humfanyi chochote. Bora umfanyie chap muwahi kulala hatakosa cha kuokotaokota!
Ndivyo inavyokuwa. Akili ikichoka au mtoto akiwa hana interest au mazingira ya kufundishia yakiwa sio rafiki au wezeshi matjisumbua bure. Sipati picha mtoto atasomaje ilhali anawasikia wenzake wakicheza, wakigombana au majirani wanapiga mziki au hata mazungumzo tu ya kawaida au kuna mahubiri hapo jirani. Ndo mana shule zinakuwa mbali kidogo na maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, makelele n.k.
 
Sisi tunawapa homework watoto kutokana na tulicho mfundisha. Na lengo ni kujua kama amaelewa alichofundishwa?

Lakini ajabu Wazazi badala ya kuwasimamia wafanye homework, wanawapa majibu na kuwafanyia homework.

Mwanafunzi akifika Shule tunajua ana uwezo mkubwa sababu homework kafanya vizuri hivyo hatmzingatii.

Matokeo yake mtoto anafeli kwa sababu maswali hajafanya yeye.

Sisi watoto tunaawatenga kwenye magroup kutokana na uelewa..

Mtoto anawekwa group A kumbe alitakiwa awe group C au D.

Wazazi wasimamie watoto wafanye Homework sio muwafanyie..

Mtoto akikosa swali najua hajanielewa napata wasaa wa kumfundisha. Lakini majibu anapewa na baba au Mama halafu kwenye mtihani hawapo, itakuaje?

Je akifika level ambayo hataweza kumfanyia itakuwaje?

NI MALALAMIKO NIMEPEWA NA MWALIMU.
kwanini uwanyanyapae eti group c na d la bashite
 
Ndivyo inavyokuwa. Akili ikichoka au mtoto akiwa hana interest au mazingira ya kufundishia yakiwa sio rafiki au wezeshi matjisumbua bure. Sipati picha mtoto atasomaje ilhali anawasikia wenzake wakicheza, wakigombana au majirani wanapiga mziki au hata mazungumzo tu ya kawaida au kuna mahubiri hapo jirani. Ndo mana shule zinakuwa mbali kidogo na maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, makelele n.k.
... mzazi una mishe zako unarejea home odd hours uko hoi mtoto naye mida hiyo yuko hoi huo muda wa kumsimamia afanye mwenyewe uko wapi? Na asipofanya mzazi unaitwa shule; wastage of time. At least zile za weekend you can dedicate some hours kumsimamia afanye mwenyewe!
 
Nilikuwa najipitia tu ila hili limenitafakarisha. Kwamba kazi ya usimamizi wa mtoto wako ni mzigo kwako?
Ndiyo. Namsimamia katika lipi?Ujue kumsimamia mtoto katika masomo ni lazima na wewe angalau uwe unajua abc katika hiko anachofanya. Kwa mfano halisi mjukuu wangu (Ke)yuko std 7. Majuzi hapo alipewa maswali Homework. Katika maswali yale lilikuwepo swali la kuchora via vya uzazi (Reproduction Organs) za mwanamke na kuzi-Label. Alihitaji msaada kwangu. Ukweli sikuamini kwanza hadi pale nilipomwuliza kama mlishafundishwa huko darasani? Akajibu ndiyyo. Nikamtaka aniletee daftari lake na anioneshe. Alileta daftari na kunionesha sawia. Ilibidi tu niwe mpole na kuanza kutoa majibu lakini kwa tahadhari kubwa sana kwani ilibidi nitumie Kiswahili ilhali shuleni wanatumia kingereza. Anasoma English medium Primary school. Kazi kweli-kweli. Sasa huo sio mzigo bwashee?
 
Nyie walimu ndio mnatakiwa kuachana na huo utaratibu wa kutoa homework. Tenga hata dakika 10 za kutoa maswali ya ulichofundisha kwa siku hiyo.

Tunalipa ada ili mambo ya shule mmalizane na watoto uko uko shule. Mtoto akifika nyumbani anatakiwa kupata muda wa kupumzika, kucheza na wenzake pamoja na kujifunza stadi za nyumbani mfano kujifanyia usafi
 
... mzazi una mishe zako unarejea home odd hours uko hoi mtoto naye mida hiyo yuko hoi huo muda wa kumsimamia afanye mwenyewe uko wapi? Na asipofanya mzazi unaitwa shule; wastage of time. At least zile za weekend you can dedicate some hours kumsimamia afanye mwenyewe!
Kweli walimu hawapimi pros and cons wanapowaachia wazazi wafanye kazi ya kusimamia H/W waliyotoa wao. Indirectly wanatufanya tuingie tena darasani kusoma ili tuweze kwasaidia kwa kuwafundisha watoto wetu kwa mwamvuli eti Tuwasimamie watoto wafanye Homework. Kumbuka sio wazazi wote walisoma na kufaulu masomo yanayotolewa kama H/W. Wazazi wengine ni bodaboda au wakulima wa kawaida, Madreva (Samahani boda,wakulima na madreva sio kwamba ninawadogosha au kuwadhalilisha hapana) nimewatumia tu kama mfano kuonesha Gap lililoko baina ya Taaluma/ Fani za kazi mbali mbali.
 
... Kama hao wanaoitwa English medium likizo hadi wanakera. Lundo la h/w na mitoto mingine kimya hadi keshokutwa wanafungua ndio unaambiwa kuna h/w!

Imagine unao wawili watatu unawaza ada tena zimepanda na mahitaji mengine unachomekewa na h/w masomo 10 x maswali 50 x watoto 2 una maswali 1000 ya kumjibia! Dah! Nikishawahi kuomba off ya dharura mimi eti matatizo ya kifamilia🤣🤣🤣
 
Duh! Pole sana - ndo hali halisi walimu wanakwepa jukumu lao. Wazazi/kaka/dada zao wakitumia AI bado wanaambiwa hiyo sio. Tafadhali waalimu hebu :KEKBye: :KEKBye: :KEKBye:
 
Homework inasaidia watoto wasizurure. Pia inasaidia kuwakumbusha walichojifunza
Ni sawa lakini wasizurure lini na wapi?? Mbona katika siku za Juma i.e. J'tatu hadi Ijumaa wapo bize shuleni hadi saa 12 jioni - watazurura ucku? Kwa weekend J'mosi na J'pili ni sahihi wakitoka kusali wainamie H/W na pale nafasi kwa mzazi inaruhusu, atamsimamia au walau kumhimiza afanye H/W alizopewa. Hiyo pia ni fursa ya mzazi kujua maendeleo ya mtoto wake kielimu.
Lakini hii H/W ya kila siku inafikirisha kwa kiasi fulani na huenda ikawa ni kero kwa baadhi ya wazazi.
 
Kusimamia i.e. kuhakikisha jambo linakwenda kama linavyotakiwa kunahitaji utulivu na pia Uelewa kwa kiasi fulani. Mtoto katika kufanya H/W anaweza akakuomba msaada wa ufafanuzi. Utafafanuaje kama hujui mwl. alifundishaje huko shuleni? Aidha waalimu wanawaweka wazazi ktk wakati mgumu sana pale inapotokea mzazi amesahau kile mtoto anaomba msaada au pengine hakumbuki kabisa au hajui kabisa. You cant be a jack of all trades. Hapo utona ni kwa nini baadhi ya wazazi wanatumia AI. Hakuna mzazi anayependa kufedheheka mbele ya mtoto wake.
Kama hauna mbinu za kukwepa kujibu usichojua bila kusema hujui basi tatizo laweza kuwa kubwa zaidi maana watoto wana maswali mengi nje ya hizi H/W wanazopewa. Unadeal nayo vipi? Tumia mbinu hiyo hiyo kumwezesha kuhangaika mwenyewe kutafuta majibu (inapobidi).
Wazazi wetu shule hawakwenda ila walihakikisha tunafanya kazi za nyumbani na shuleni. Tusipende kukwepa wajibu wetu kwa lame excuses.
Hakuna Tatizo lolote na inashauriwa iwe hivyo kwani katika somo unaloweza/unalomudu ukimfundisha mwanao unamjazia uelewa zaidi. Mwl. hawezi kumaliza kila kitu huko darasani. Na ndo mana kuna vitabu vya shule vya kiada na vya ziada.
Good.
 
Ndiyo. Namsimamia katika lipi?Ujue kumsimamia mtoto katika masomo ni lazima na wewe angalau uwe unajua abc katika hiko anachofanya. Kwa mfano halisi mjukuu wangu (Ke)yuko std 7. Majuzi hapo alipewa maswali Homework. Katika maswali yale lilikuwepo swali la kuchora via vya uzazi (Reproduction Organs) za mwanamke na kuzi-Label. Alihitaji msaada kwangu. Ukweli sikuamini kwanza hadi pale nilipomwuliza kama mlishafundishwa huko darasani? Akajibu ndiyyo. Nikamtaka aniletee daftari lake na anioneshe. Alileta daftari na kunionesha sawia. Ilibidi tu niwe mpole na kuanza kutoa majibu lakini kwa tahadhari kubwa sana kwani ilibidi nitumie Kiswahili ilhali shuleni wanatumia kingereza. Anasoma English medium Primary school. Kazi kweli-kweli. Sasa huo sio mzigo bwashee?
Sio lazima. Mimi wakiniuliza maswali huwa nawauliza kama ni HW au wanajisomea tu wakakutana na swali. Wakijibu ni HM nawaambia wapambane mpaka wajibu kama mwl wao alivyowafundisha.

Kama atakosea basi ndio kazi ya mwl wake kumwelekeza hadi aweze. Kazi yangu ni kuhakikisha wamefanya kazi zao za shule🤣
 
Hiyo imekaa vizuri. Hongera mkuu.
 
Daa , inachekesha sana, lakini vijana wetu wanazidi kuwa mazombie
 
Mtoto anarudi shule saa 12 hiyo home work atafanya saa ngp?
Saa kumi alfajiri anatakiwa ajiandae kwenda shule,,analala saa ngp na anapumzika saa ngp?
Mambo ya shule malizeni shule,tunalipa ada kubwa na bado tuwasaidie kufundisha watoto wetu..
Sijui huwa wanalenga nn kuwashindisha kutwa nzima shule, saa 12 hadi 12 jioni. Miaka ya 1990 tumesoma Kwa raha na nafasi, ukiingia asubuhi, mchana unarudi nyumbani. Ukiingia mchana, jioni unarudi nyumbani.
 
Mtoto lazima apate muda wa kucheza, kupumzika na kusoma.
Sasa hawa walimu wa sasa wanafanya watoto hawapati muda wa kupumzika wala kucheza,
Hii ni hatari kwa afya ya akili...
 
Sijui huwa wanalenga nn kuwashindisha kutwa nzima shule, saa 12 hadi 12 jioni. Miaka ya 1990 tumesoma Kwa raha na nafasi, ukiingia asubuhi, mchana unarudi nyumbani. Ukiingia mchana, jioni unarudi nyumbani.
Huu "ukisasa" una mambo mengi sana. Utadhani e.g. 2x2 imebadilika nakuwa sio 4 tena kumbe ni 4 ile-ile tuliyoisoma enzi hizo hadi leo. Ninamaanisha masomo ya zamani sio tofauti na ya sasa.
 
Back
Top Bottom