Kwanini homework za Wanafunzi zinafanywa na Wazazi? Punguzeni ujuaji

Mtoto lazima apate muda wa kucheza, kupumzika na kusoma.
Sasa hawa walimu wa sasa wanafanya watoto hawapati muda wa kupumzika wala kucheza,
Hii ni hatari kwa afya ya akili...
Na watoto wengine wanaanza kuichukia shule.
 
Mtoto anaamka asb. lakini haendi shule ukiuliza anakwambia kichwa kinauma sana.Ukimpeleka zahanati, mkiwa njiani anakwambia nimepona kichwa hakiumi tena.
Mtoto anaamka akijiandaa kwenda shule akiwa bado ana usingizi,,
Analala njia nzima hadi anafika shule yupo hoi..
 
Complications...tulikuwa tunafanza zoezi wenyewe hakuna mjomba...baba wala mama...jichanganye usimalize hayo mazoezi ya shule😛😛
 
Nilivyomwelewa mtoa mada ni kuwa wewe kazi yako ni kuhakikisha unamsimamia mtoto na kuhakikisha amefanya kazi zake. Sio umfundishe au umpatie majibu. Ni sawa na unapomsimamia na kuhakikisha anafanya mambo yake mengine.

Lakini hivi kumfundisha mtoto wako (kama unaweza) kuna tatizo lolote?
Nadhani pia mtoa mada alikuwa na maana hiyo, msimamie mtoto afanye homework yake, siyo umpe majibu
 
Mtihani ukija wanapata matokeo ya kutengeneza..
Ili ada zitoke kwa wakati
Yep! Waalimu wanajua kuchezesha karata zao vizuri sana ili mkono uende kinywani. Utasikia mara kuna tuisheni, ziara mbuga za wanyama au kutembelea mapango ya amboni n.k. Mzazi anatakiwa atoe mchango ili mtoto wake aweze kushiriki kwani ni hiyo ni ziara muhimu kwake kimasomo. Na Ole wako usipotekeleza; hapo nyumbani nakwambia hapatakaliki, dogo ni kilio mtindo mmoja.
 
Halafu sio pesa ndogo,,kianzio 80k au 100k kila wanafunzi..
 
Mtoto lazima apate muda wa kucheza, kupumzika na kusoma.
Sasa hawa walimu wa sasa wanafanya watoto hawapati muda wa kupumzika wala kucheza,
Hii ni hatari kwa afya ya akili...
Hatari sana. Wazazi wanakwepa sana na hawapendi kuhusu mtoto kucheza wakidhani mtoto anapoteza muda kujifunza taaluma.
 
Your too primitive teacher, in modern teaching methods such as Flipped class emphasise the learner to do his/her homework after class using ICT materials(smartphones, tablets etc). Usikaririshe wanafunzi wafundishe kuelewa. To score your marks is not the big deal
 
Hatari sana. Wazazi wanakwepa sana na hawapendi kuhusu mtoto kucheza wakidhani mtoto anapoteza muda kujifunza taaluma.
Wazazi tunakosea pakubwa sana,
Mtoto lazima umpe nafasi ya kurelax akili,, kucheza na kujifunza mambo mengine ya ulimwengu..
Umpe nafasi kucheza ili ujuwe kipaji cha mtoto nje ya elimu..nk..

Kumnyima mtoto nafasi ya kucheza au kupumzika ni kudumaza akili yake..
 
Nilivyomwelewa mtoa mada ni kuwa wewe kazi yako ni kuhakikisha unamsimamia mtoto na kuhakikisha amefanya kazi zake. Sio umfundishe au umpatie majibu. Ni sawa na unapomsimamia na kuhakikisha anafanya mambo yake mengine.

Lakini hivi kumfundisha mtoto wako (kama unaweza) kuna tatizo lolote?
Mimi sio mwalimu ila najaribu kuwasoma wote wawili, mtoa mada yupo sahihi. Kumsimamia mtoto afanye home work au akirudi akioga, mwambie ashike daftari afanye home work, hakuna Home Work inayozidi lisaa limoja. Sasa nashindwa kuelewa hao wajinga wanaosema eti wanalipa ada kubwa, naamini kabisa hakuna anayelipa ada kubwa hapo.
 
Tumekuwa wazembe kiasi kwamba hata majukumu yetu ya malezi tunatamani tutoe pesa wengine watufanyie.
Wanajitetea sijui kuwasimamia watoto kujifunza kazi za nyumbani kama kutunza bustani nk, utafikiri kweli wanafanya hivyo. Kama unaweza hayo mengine, hata hilo la HW ambalo hata halichukui muda pia hushindwi.
 
Back
Top Bottom