Kwanini hukumu ya kesi ya Mwana FA dhidi ya TIGO imeripotiwa kwa makosa?

Kwanini hukumu ya kesi ya Mwana FA dhidi ya TIGO imeripotiwa kwa makosa?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Nimepitia vyombo karibia viwili vya habari vilivyoripoti hukumu ya Mahakama ya Rufaa katika kesi inayomuhusu Mwana FA na AY dhidi ya kampuni ya TIGO.

Kwa jinsi maamuzi hayo yalivyoripotiwa ni kuwa Mwana FA na AY wameshinda kesi hiyo. Ukisoma vizuri mtiririko wa kesi zenyewe, utagundua uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Rufaa kurudisha kesi hiyo Mahakama Kuu siyo ushindi Kwa Mwana FA na AY kama ilivyoripotiwa na vyombo hivyo, bali ni ushindi Kwa kampuni ya TIGO.

Kwa mfano, pitia ripoti hii:
MwanaFA, AY win copyright appeal in Sh2.1 Billion Tigo payout case

Embu tuliweke hili jambo sawa na kama ni mimi ambaye sijaelewa nieleweshwe.
 
Tanzania tuna kwama katika kuwa na waandishi bobezi katika sekta mbalimbali

Kuna uandishi wa eneo la madai, haki jinai ili kuweza kufuata mienendo ya kesi na hukumu bila ubabaifu, uandishi eneo la michezo, uandishi eneo siasa, eneo la uchumi n.k

Sana waandishi wa Tanzania wa vyombo mbalimbali, mitandao n.k wanataka kuandika (cover) stori zote kuanzia udaku hadi mambo mazito wakati elimu na uzoefu wa maeneo mengine hawana. Hapo ndipo sisi walaji (customers) tunalishwa umbea badala ya habari kamili.
 
Toka maktaba :

Mfano wa kesi kusikilizwa na mahakama isiyokuwa na mamlaka : Kesi ya Mchg. Mashimo


View: https://m.youtube.com/watch?v=zFdHYs9yxSI

Jaji S.M Magimbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania anasema ktk hukumu yake kuwa Mahakama ya Wilaya haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo anaamuru mfungwa Daudi Mashimo Nkuba almaarufu Mchungaji Mashimo aachiwe maramoja.

N.B
Mahakama za chini zinasikiliza Kesi za madai zisizozidi million 200 na zisizo pungua million 30 ukikosea hapa mahakama itatupilia mbali.

Yaani Madai ya kurejesha mali isiyohamishika (yenye thamani isiyozidi TZS milioni 300)...

Mfano wa 2:
Mahakama Kuu, Dar es Salaam, imetengua hukumu iliyoamuru kampuni ya simu za mkononi MIC (T) Limited, maarufu Tigo, kuwalipa wanamuziki wa kizazi kipya Hamisi Mwinyijuma (Mwana-FA) na Ambwene Yesaya (AY) Sh2.1 bilioni kwa kukiuka sheria za hatimiliki.

Jaji Joacquine De-Mello amebatilisha uamuzi huo baada ya kukubaliana na rufaa ya Tigo kuwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo...ya mabilioni
 
Ona hata hukumu ya mchungaji Mashimo inavyo tangazwa ktk vyombo vya habari.. na pia mchungaji Mashimo anavyohojiwa na mwandishi uchwara asiye na elimu ya kuripoti taarifa za kimahakama ..

13 Julai 2025

MAHAKAMA KUU YAFUTA UAMUZI WA MAHAKAMA YA WILAYA, MCHUNGAJI MASHIMO ASHINDA RUFANI YAKE

MCHUNGAJI MASHIMO AONGELEA SAKATA ZIMA LILOLOPELEKEA KUTUPWA GEREZANI...

View: https://m.youtube.com/watch?v=zFdHYs9yxSI

Mchungaji Daud Nkuba, maarufu Komando Mashimo, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia katika ...hata hivyo mchungaji Mashimo alikataa rufaa Mahakama Kuu, ambapo mahakama hiyo ya juu nchini Tanzania ilitengua hukumu hiyo ya mahakama ya wilaya ya Kinondoni ya jijini Dar es Salaam ....

SOMA HUKUMU YA MAHAKAMA KUU: Judgement



Daudi Mashimo Nkuba vs Republic (Criminal Appeal No. 7299 of 2025) [2025] TZHC 3515 (13 June 2025). Land disputes must...

..
With the demonstrated findings above, it is clear that the trial court did not have jurisdiction to entertain the charge levelled against the accused / appellant. Having so found that the trial court had no jurisdiction
and for the orders that will follow course, I see no reason to dwell on the remaining grounds of appeal. As a matter of law, a decision by a court without jurisdiction is a nullity, and so are the consequential orders
resulting therefrom. In consequential thereto, this appeal is allowed. The
proceedings of the trial court, resultant judgment and the consequential orders thereto are hereby nullified. The subsequent conviction and
sentence of the trial court are hereby set aside. The appellant is to be immediately released from prison unless he is otherwise held for other lawful reasons.

JUDGE
S.M Maghimbi.
Signed
13 June 2025
 
Soma vizuri
Tigo alienda mahakama kuu
Kwa nilivyosoma mlolongo wa kesi hii, ndiyo TIGO alienda Mahakama Kuu ila alishindwa na kesi ilishatosha Mahakama Kuu ikaenda Mahakama ya Rufaa ambao ndiyo wametoa uamuzi huu wa sasa wa kesi kurudishwa Mahakama Kuu ili wasikilize vipengele 10 ambaye hawakuvisikiliza wana kuzizingatia.
 
Hiyo ishu nilivyoielewa mimi akina fa walipeleka malalamiko mahakma kuu,
Mahakama kuu ikasema yenyewe haushughuliki na madai ya haki miliki hivyo ikabidi akina fa waenda mahakama ya wilaya ya kinondoni ambapo shauli lilisikilizwa halafu akina fa wakashindwa tito wakaambiwa wawalipe.
Sasa tigoo baada ya hukumu ya mahakama ya wilaya wakaenda kukata rufaa mahakama ya rufaa kupinga hukumu hiyo, sasa mahakama ya rufaa ikakubaliana na rufaa ya tito na kuamuru shauri hilo likasikilizwe na mahakama kuu .
Kwa uelewa wangu shauri hilo linaenda kuanza kusikilizwa upya mahakama kuu
 
Tanzania tuna kwama katika kuwa na waandishi bobezi katika sekta mbalimbali

Kuna uandishi wa eneo la madai, haki jinai ili kuweza kufuata mienendo ya kesi na hukumu bila ubabaifu, uandishi eneo la michezo, uandishi eneo siasa, eneo la uchumi n.k

Sana waandishi wa Tanzania wa vyombo mbalimbali, mitandao n.k wanataka kuandika (cover) stori zote kuanzia udaku hadi mambo mazito wakati elimu na uzoefu wa maeneo mengine hawana. Hapo ndipo sisi walaji (customers) tunalishwa umbea badala ya habari kamili.

Ona hata hukumu ya mchungaji Mashimo inavyo tangazwa ktk vyombo vya habari.. na pia mchungaji Mashimo anavyohojiwa na mwandishi uchwara asiye na elimu ya kuripoti taarifa za kimahakama ..

13 Julai 2025

MAHAKAMA KUU YAFUTA UAMUZI WA MAHAKAMA YA WILAYA, MCHUNGAJI MASHIMO ASHINDA RUFANI YAKE

MCHUNGAJI MASHIMO AONGELEA SAKATA ZIMA LILOLOPELEKEA KUTUPWA GEREZANI...

View: https://m.youtube.com/watch?v=zFdHYs9yxSI

Mchungaji Daud Nkuba, maarufu Komando Mashimo, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia katika ...hata hivyo mchungaji Mashimo alikataa rufaa Mahakama Kuu, ambapo mahakama hiyo ya juu nchini Tanzania ilitengua hukumu hiyo ya mahakama ya wilaya ya Kinondoni ya jijini Dar es Salaam ....

SOMA HUKUMU YA MAHAKAMA KUU: Judgement



Daudi Mashimo Nkuba vs Republic (Criminal Appeal No. 7299 of 2025) [2025] TZHC 3515 (13 June 2025). Land disputes must...

..
With the demonstrated findings above, it is clear that the trial court did not have jurisdiction to entertain the charge levelled against the accused / appellant. Having so found that the trial court had no jurisdiction
and for the orders that will follow course, I see no reason to dwell on the remaining grounds of appeal. As a matter of law, a decision by a court without jurisdiction is a nullity, and so are the consequential orders
resulting therefrom. In consequential thereto, this appeal is allowed. The
proceedings of the trial court, resultant judgment and the consequential orders thereto are hereby nullified. The subsequent conviction and
sentence of the trial court are hereby set aside. The appellant is to be immediately released from prison unless he is otherwise held for other lawful reasons.

JUDGE
S.M Maghimbi.
Signed
13 June 2025

Ni kweli waandishi hawapendi kuspecialize na vyombo vyenyewe vya habari havitaki kuwekeza vya kutosha kuwa na specialized reporters.

Embu tusaidie kuliweka sawa. Inakuwaje huu ni ushindi kwa MwanaFA na AY wakati rufaa ya TIGO imesikilizwa na uamuzi wa kurudisha kesi Mahakama Kuu unayapa nafasi madai yao 10 ambayo hayakusikilizwa?
 
Back
Top Bottom