Kwanini hukumu ya kesi ya Mwana FA dhidi ya TIGO imeripotiwa kwa makosa?

Tanzania tuna kwama katika kuwa na waandishi bobezi katika sekta mbalimbali

Kuna uandishi wa eneo la madai, haki jinai ili kuweza kufuata mienendo ya kesi na hukumu bila ubabaifu, uandishi eneo la michezo, uandishi eneo siasa, eneo la uchumi n.k

Sana waandishi wa Tanzania wa vyombo mbalimbali, mitandao n.k wanataka kuandika (cover) stori zote kuanzia udaku hadi mambo mazito wakati elimu na uzoefu wa maeneo mengine hawana. Hapo ndipo sisi walaji (customers) tunalishwa umbea badala ya habari kamili.
Sitanii kwani Balile yeye ni mwandishi wa nini?
 
Ukisema ni ushindi kwa tigo unakosea pia. Kwasasa mwanaFA na AY bado ni washindi wa hii kesi. Rufaa ya tigo ni kutaka vipengele vipya kumi walivyosema wao vijadiliwe na pia lalamiko la tigo kuwa hukumu kutoka mahakama ya wilaya ilikuwa ni batili kwakuwa kiwango cha fine au reward ya Billion 4 (wamelipwa 2+ bilion after all) waliyopewa hawa wasanii ni Kubwa sana kujadiliwa na mahakama ya wilaya.

So mziki ni kama wakipeleka huu mjadala mahakama kuu kukaonekana kuna vipengele vimekiukwa. Tigo hii kesi wakati ipo ngazi ya mahakama ya wilaya wao walichukulia poa wakajua vijana hawatatoboa wakapeleka wakili asiyejiweza. Matokeo ni wakazidiwa kete na msando.
 
Hiyo ishu nilivyoielewa mimi akina fa walipeleka malalamiko mahakma kuu,
Mahakama kuu ikasema yenyewe haushughuliki na madai ya haki miliki hivyo ikabidi akina fa waenda mahakama ya wilaya ya kinondoni ambapo shauli lilisikilizwa halafu akina fa wakashindwa tito wakaambiwa wawalipe.
Sasa tigoo baada ya hukumu ya mahakama ya wilaya wakaenda kukata rufaa mahakama ya rufaa kupinga hukumu hiyo, sasa mahakama ya rufaa ikakubaliana na rufaa ya tito na kuamuru shauri hilo likasikilizwe na mahakama kuu .
Kwa uelewa wangu shauri hilo linaenda kuanza kusikilizwa upya mahakama kuu
Soma vizuri tena mtiririko haukuwa hivyo. Akina mwana FA walishitaki tigo mahakama ya wilaya na kudai fidia ya kaisi cha billion 4, mahakama ya wilaya baada ya kuprocess malalamiko,wakashusha adhabu hadi kiasi cha shilingi bilioni 2 na chenji zake.

Baada ya hapo tigo wakajua kuwa ngoma kumbe ipo serious na wao walichukulia poa, so wakapeleka malalamiko yao mahakama kuu kwa kudai kuna vipengele kadhaa vimekiukwa ikiwamo swala la fidia ya shilingi bilioni 4 kuwa ni kiasi kikubwa sana kujadiliwa na mahakama ngazi ya wilaya.

Na hapo ndipo upande wa malalamiko yaani AY na FA wakaomba kukaziwa hukumu haraka sana, ndipo tigo wakafungiwa account zao ili waweze kuwalipa walalamikaji.

Malipo yametoka ila kesi ikapelekwa mahakama kuu na kusikilizwa huko ndipo uchambuzi yakinifu ulifanyika na kukawa na mjadala wavile vipengele vipya walivyoraise tigo mojawapo ni kulalamika kuwa wao tigo kama tigo hawakuhusishwa moja kwa moja na matumizi ya nyimbo za hawa wasanii bali waliletewa na wakala wao anaewaleteaga contents aitwae "Cellulant Tanzania LTD" na hao Cellulant ndio wanatakiwa wawalipe hawa wasanii fidia ila si wao tigo.

So kilichotokea ni mahakama kuu kuridhia hayo maamuzi ndio rufaa kikakatwa na mahakama ya rufaa ikaamuru kuwa kuna haja ya kuangalia upya kwanza utaratibu uliotumika katika kesi na kujiridhisha kama mahakama ya wilaya imesikiliza kesi ambayo ipo nje ya uwezo wake.

So kama itaonekana kuwa hiyo kesi haikutakiwa kusikilizwa mahakama ya wilaya then mchezo unaanza upya na hapa tigo atashinda mchana kweupe sababu atakiri kutumia nyimbo alizoletewa na content client wake so yeye hahusiki ni hiyo kampuni ndio iwajibishwe na hapo ndio mwanaFA na AY watatakiwa kurejesha hela za tigo haraka sana halafu wakaanze tena kesi mpya ya madai mahakama ya wilaya huko chini tena, safari hii wakishitaki Cellulite Tanzania LTD sio tigo tena.
 
Nadhani umechanganya na kupotea kabisa katika maelezo yako. Kama kina MwanaFA walishindwa ilikuwaje TIGO waambiwe wawalipe.
 
Ukisema ni ushindi kwa tigo unakosea pia. Kwasasa mwanaFA na AY bado ni washindi wa hii kesi. Rufaa ya tigo ni kutaka vipengele vipya kumi walivyosema wao vijadiliwe na pia lalamiko la tigo kuwa hukumu kutoka mahakama ya wilaya ilikuwa ni batili kwakuwa kiwango cha fine au reward ya Billion 4 (wamelipwa 2+ bilion after all) waliyopewa hawa wasanii ni Kubwa sana kujadiliwa na mahakama ya wilaya.

So mziki ni kama wakipeleka huu mjadala mahakama kuu kukaonekana kuna vipengele vimekiukwa. Tigo hii kesi wakati ipo ngazi ya mahakama ya wilaya wao walichukulia poa wakajua vijana hawatatoboa wakapeleka wakili asiyejiweza. Matokeo ni wakazidiwa kete na msando.
Kitendo cha kurudisha kesi Mahakama Kuu ili vipengele vyao 10 vipate kusikilizwa ni aina ya ushindi Kwa TIGO maana bado inawapa uhai katika utetezi wao. Ambacho sijaelewa ni hizi taarifa kutolewa kuwa ni ushindi Kwa kina MwanaFA na AY, hapo ndiyo sijaelewa kabisa.
 
Soma vizuri tena mtiririko haukuwa hivyo. Akina mwana FA walishitaki tigo mahakama ya wilaya na kudai fidia ya kaisi cha billion 4, mahakama ya wilaya baada ya kuprocess malalamiko,wakashusha adhabu hadi kiasi cha shilingi bilioni 2 na chenji zake.

Baada ya hapo tigo wakajua kuwa ngoma kumbe ipo serious na wao walichukulia poa, so wakapeleka malalamiko yao mahakama kuu kwa kudai kuna vipengele kadhaa vimekiukwa ikiwamo swala la fidia ya shilingi bilioni 4 kuwa ni kiasi kikubwa sana kujadiliwa na mahakama ngazi ya wilaya.

Na hapo ndipo upande wa malalamiko yaani AY na FA wakaomba kukaziwa hukumu haraka sana, ndipo tigo wakafungiwa account zao ili waweze kuwalipa walalamikaji.

Malipo yametoka ila kesi ikapelekwa mahakama kuu na kusikilizwa huko ndipo uchambuzi yakinifu ulifanyika na kukawa na mjadala wavile vipengele vipya walivyoraise tigo mojawapo ni kulalamika kuwa wao tigo kama tigo hawakuhusishwa moja kwa moja na matumizi ya nyimbo za hawa wasanii bali waliletewa na wakala wao anaewaleteaga contents aitwae "Cellulant Tanzania LTD" na hao Cellulant ndio wanatakiwa wawalipe hawa wasanii fidia ila si wao tigo.

So kilichotokea ni mahakama kuu kuridhia hayo maamuzi ndio rufaa kikakatwa na mahakama ya rufaa ikaamuru kuwa kuna haja ya kuangalia upya kwanza utaratibu uliotumika katika kesi na kujiridhisha kama mahakama ya wilaya imesikiliza kesi ambayo ipo nje ya uwezo wake.

So kama itaonekana kuwa hiyo kesi haikutakiwa kusikilizwa mahakama ya wilaya then mchezo unaanza upya na hapa tigo atashinda mchana kweupe sababu atakiri kutumia nyimbo alizoletewa na content client wake so yeye hahusiki ni hiyo kampuni ndio iwajibishwe na hapo ndio mwanaFA na AY watatakiwa kurejesha hela za tigo haraka sana halafu wakaanze tena kesi mpya ya madai mahakama ya wilaya huko chini tena, safari hii wakishitaki Cellulite Tanzania LTD sio tigo tena.
Nadhani Kwa kiasi kikubwa maelezo yako yako sahihi. Sioni inakuwaje haya maamuzi ya Mahakama ya Rufaa ni ushindi kwa kina MwanaFA na AY
 
Tanzania nasi tunatakiwa kuwa na waandishi wanaoweza kuelezea matukio hadi tamati ya hukumu kwa ufasaha:

Kesi ya mwili wa Edgar Lungu, mwandishi akifafanua hukumu ya kule South Africa

PART 1:
Pretoria, South Africa
06 August 2025

Edgar Lungu’s Court Case Explained - Who Is Likely to Win and Why
Will Edgar Lungu family win the court case in South Africa? On 4 August 2025,

View: https://m.youtube.com/watch?v=JJb86H9SRP0

inside the Pretoria High Court, Edgar Lungu’s legal team was cornered as judges pointed out contradictions in their own affidavits. The court heard emotional arguments from the widow’s side, but the Zambian state’s lawyers responded with documents and timelines that dismantled the case point by point.

PART 2 :
On 8 August,2025 the High Court ruled that former president Edgar Lungu’s body must be handed over to the Zambian government for a state funeral at Embassy Park. The judgment dismissed all of the family’s legal challenges, giving President Hakainde Hichilema’s administration full control over the burial. Here’s the full breakdown of what happened and what it means next.

View: https://m.youtube.com/watch?v=fV3-hngvXNU
 
Cheki jinsi jaji akisoma hukumu yake alivyotulia na kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu hukumu yake.

Tanzania tuna kila sababu waandishi na mahakama kuhakikisha viwago vya mfumo haki jinai, haki madai upo wazi bila kutoa nafasi ya usabaaji taarifa zisizo sahihi

8 August 2025
The Pretoria High Court has ordered that the remains of former Zambian President Edgar Lungu be repatriated to Zambia for a state funeral. Gauteng Deputy Judge President Aubrey Ledwaba delivered the ruling in favor of the government. Lungu passed away in Johannesburg in June while undergoing medical treatment...

View: https://m.youtube.com/watch?v=X2LvVUyEnVo
 
Mods hii mada ni muhimu sana. Sidhani kama mlitakiwa muitupe huku kwenye Celebrities Forum Active Cookie

Dola haitaki raia kufahamu mifumo ya kisheria, mahakama na katiba inafanya kazi vipi.

Uzi huu ni elimu kubwa ya haki kwa raia na siyo kwa ma celebrities.

Naunga mkono uzi huu urudi jukwaa la Hoja Mchanganyiko au hata jukwaa la siasa.

Mahakama au korti kubebe mamlaka isiyokuwa nayo kisheria ni masuala makubwa kwa umma mzima hivyo Mods Robot wa JamiiForums wasikilize hoja yako muhimu ambayo pia naamini wasomaji wengi wanaona.
 
Kitendo cha kurudisha kesi Mahakama Kuu ili vipengele vyao 10 vipate kusikilizwa ni aina ya ushindi Kwa TIGO maana bado inawapa uhai katika utetezi wao. Ambacho sijaelewa ni hizi taarifa kutolewa kuwa ni ushindi Kwa kina MwanaFA na AY, hapo ndiyo sijaelewa kabisa.
Ushindi ambao nahisi unasemwa na waandishi ni kuwa kesi zinazohusu hakimiliki na hakishiriki Zina mamlaka ya kusikilizwa mahakama ya wilaya hivyo imetengua uamuzi wa mahakama kuu kuwa mahakama ya wilaya haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi. Kutokana na kipengele Cha sheria mahususi ya hakimiliki na hakishiriki inasema kabisa kesi zake zisikilizwe mahakama ya wilaya. Sheria inayosema kuhusu kesi za madai ambazo ni za hela nyingi kusikilizwa mahakama kuu sheria ya jumla. Kwahyo mahakama ya Rufaa imerudisha kusikiliza vipengele vingine vya Rufaa kasoro hicho.
 
Soma vizuri tena mtiririko haukuwa hivyo. Akina mwana FA walishitaki tigo mahakama ya wilaya na kudai fidia ya kaisi cha billion 4, mahakama ya wilaya baada ya kuprocess malalamiko,wakashusha adhabu hadi kiasi cha shilingi bilioni 2 na chenji zake.

Baada ya hapo tigo wakajua kuwa ngoma kumbe ipo serious na wao walichukulia poa, so wakapeleka malalamiko yao mahakama kuu kwa kudai kuna vipengele kadhaa vimekiukwa ikiwamo swala la fidia ya shilingi bilioni 4 kuwa ni kiasi kikubwa sana kujadiliwa na mahakama ngazi ya wilaya.

Na hapo ndipo upande wa malalamiko yaani AY na FA wakaomba kukaziwa hukumu haraka sana, ndipo tigo wakafungiwa account zao ili waweze kuwalipa walalamikaji.

Malipo yametoka ila kesi ikapelekwa mahakama kuu na kusikilizwa huko ndipo uchambuzi yakinifu ulifanyika na kukawa na mjadala wavile vipengele vipya walivyoraise tigo mojawapo ni kulalamika kuwa wao tigo kama tigo hawakuhusishwa moja kwa moja na matumizi ya nyimbo za hawa wasanii bali waliletewa na wakala wao anaewaleteaga contents aitwae "Cellulant Tanzania LTD" na hao Cellulant ndio wanatakiwa wawalipe hawa wasanii fidia ila si wao tigo.

So kilichotokea ni mahakama kuu kuridhia hayo maamuzi ndio rufaa kikakatwa na mahakama ya rufaa ikaamuru kuwa kuna haja ya kuangalia upya kwanza utaratibu uliotumika katika kesi na kujiridhisha kama mahakama ya wilaya imesikiliza kesi ambayo ipo nje ya uwezo wake.

So kama itaonekana kuwa hiyo kesi haikutakiwa kusikilizwa mahakama ya wilaya then mchezo unaanza upya na hapa tigo atashinda mchana kweupe sababu atakiri kutumia nyimbo alizoletewa na content client wake so yeye hahusiki ni hiyo kampuni ndio iwajibishwe na hapo ndio mwanaFA na AY watatakiwa kurejesha hela za tigo haraka sana halafu wakaanze tena kesi mpya ya madai mahakama ya wilaya huko chini tena, safari hii wakishitaki Cellulite Tanzania LTD sio tigo tena.
Tigo Inabidi Wapambane Na Huyo Wakala Wao....Kama Wakina Ay Walivyombana Na Tigo...
 
Ushindi ambao nahisi unasemwa na waandishi ni kuwa kesi zinazohusu hakimiliki na hakishiriki Zina mamlaka ya kusikilizwa mahakama ya wilaya hivyo imetengua uamuzi wa mahakama kuu kuwa mahakama ya wilaya haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi. Kutokana na kipengele Cha sheria mahususi ya hakimiliki na hakishiriki inasema kabisa kesi zake zisikilizwe mahakama ya wilaya. Sheria inayosema kuhusu kesi za madai ambazo ni za hela nyingi kusikilizwa mahakama kuu sheria ya jumla. Kwahyo mahakama ya Rufaa imerudisha kusikiliza vipengele vingine vya Rufaa kasoro hicho.
Nadhani wewe naye unazidi kutuvuruga. Kati ya hizo pande mbili, nani alifungua kesi Mahakama ya Rufaa?
 
Tigo Inabidi Wapambane Na Huyo Wakala Wao....Kama Wakina Ay Walivyombana Na Tigo...
Kama wakala alikuwepo katika issue hii nzima, basi TIGO wanaweza kumtumia kama shahidi. Kawaida katika situation kama hiyo, kampuni ya mwisho inajivua jukumu lote la hatimiliki na linabebwa na hiyo anayewapelekea kazi.
 
Unachanganywa na neno KUSHINDA

Wakina Fa&Ay WALISHINDA kesi na kutakiwa kulipwa kwenye mahakama ya Wilaya

Tigo wakaata rufaa Mahakama kuu Hoja zao zikashindwa kwamba mahakama haina jurisdiction hiyo

Tigo Wakakata rufaa mahakama ya rufaa ili Hoja zao ambazo wanadai hazikuzingatiwa zisikilizwe WAKASHINDA kwamba kesi sasa ihamie Mahakama ya rufaa ili isikilizwe

Kwahiyo ikiripotiwa kwamba Tigo wameshinda kesi yao mahakama ya Rufaa ili hoja zao zisikilizwa mahaka kuu inakua sahihi kabisa
 
Kwa hiyo unakubaliana na mimi kuwa haileti mantiki kwa hatua hii kesi ilipokuwa imefikia na maamuzi ya mahakama kusema kina MwanaFA na AY "wameshinda".
 
Back
Top Bottom