Kwanini huu mkataba umesainiwa baada ya yeye kuondoka?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
Nilishaacha kujishughulisha sana na mambo ya Tanzania kwa ujumla wake maana ni kazi bure tu.

Ni kujisumbua tu. Ni kupigania maslahi ya majitu mengi yasiyo na akili.

Ila hili jambo la ‘Covfefe’ ya bandari zetu, muda wake ambao mkataba umesainiwa, kelele za wananchi dhidi yake, harakati za wanaharakati, ukwepaji wa serikali katika kutoa ufafanuzi wa kueleweka, kujishuku kwa wahusika, na kadhalika, kumenifanya niwaze kidogo kwa sauti 🤔. Nawaza maswali ya kijinga kijinga yanayoendana na elimu yangu ya kidato cha nne 🤣.

Ni hivi; hivi kweli huu mkataba angekuwepo yule Ngosha, pamoja na mapungufu yake mengi aliyokuwa nayo, angemwaga kweli wino wa kalamu yake na kuridhia nchi kuingia kwenye mkataba wa namna hiyo?

Na hao jamaa wa Dubai walianza lini kuzinyemelea bandari zetu?

Kwa nini huo mkataba umesainiwa baada Ngosha kurudisha namba?

Ah, maswali ni mengi lakini majibu ya kuridhisha na kueleweka, mpaka hivi sasa hayapo!

Anyway, ni hivyo tu. Nilikuwa nawaza tu kwa sauti. Sijali….wafanye tu wanavyotaka.
 
Duh

Kama Paul kahusika basi hata Shujaa angesaini

Paul na Yoweri ni Watoto wa DSM wanaelewa vilivyo Udhaifu Wetu katika kufikiri na kuamua

Nitajie Mwanasiasa mmoja wa Tanzania ambaye mwanae yuko Jeshini kizalendo zaidi kama ilivyokuwa Enzi za akina Makongoro na mdogo wake?

Hawa wanawaza ufisadi tu ndio unauona akina General Muhoza wanavyomdharau Ruto
 
Mbona ikulu imekamilishwa,bwawa la Nyerere je? Vitu walivyovipanga pamoja ilikuwa Lazima wavitimize la sivyo wananchi tungekasirika
Hiyo kwako ndio justification bandari yetu kutolewa sadaka kwa wajomba?

Au kutoa sadaka bandari yetu kwa wajomba zake walipanga huyo mzanzibari msaliti na nani?
 
Mbona wamesema ni suala la kitambo...hatukushirikishwa tu.Serikali ya TZ haijawahi mwona mtanzania kama ni Binadamu wa kushirikishwa jambo
Kitambo kipi wakati bandari imetolewa kwa wajomba, zile safari za arabuni baada ya msaliti kuingia madarakani hukuwahi kuziona?

Hukuwahi kuona mpaka picha yake ilipowekwa kwenye lile jengo refu huko Dubai? ndio alikuwa anatongozwa sasa.
 
Mbona wamesema ni suala la kitambo...hatukushirikishwa tu.Serikali ya TZ haijawahi mwona mtanzania kama ni Binadamu wa kushirikishwa jambo
Anhaaa….kama ni suala la kitambo basi inawezekana kabisa Ngosha alilikataa na baada ya yeye kufariki, hao waliobaki wakaona ndo muda muafaka wa kulirejea tena!

Maswali yanazidi kuongezeka tu!
 
Yeah,Kuna uwezekano pia
 
Nilishaacha kujishughulisha sana na mambo ya Tanzania kwa ujumla wake maana ni kazi bure tu.

Ni kujisumbua tu. Ni kupigania maslahi ya majitu mengi yasiyo na akili.

Ila hili jambo la ‘Covfefe’ ya bandari zetu, muda wake ambao mkataba umesainiwa, kelele za wananchi dhidi yake, harakati za wanaharakati, ukwepaji wa serikali katika kutoa ufafanuzi wa kueleweka, kujishuku kwa wahusika, na kadhalika, kumenifanya niwaze kidogo kwa sauti 🤔. Nawaza maswali ya kijinga kijinga yanayoendana na elimu yangu ya kidato cha nne 🤣.

Ni hivi; hivi kweli huu mkataba angekuwepo yule Ngosha, pamoja na mapungufu yake mengi aliyokuwa nayo, angemwaga kweli wino wa kalamu yake na kuridhia nchi kuingia kwenye mkataba wa namna hiyo?

Na hao jamaa wa Dubai walianza lini kuzinyemelea bandari zetu?

Kwa nini huo mkataba umesainiwa baada Ngosha kurudisha namba?

Ah, maswali ni mengi lakini majibu ya kuridhisha na kueleweka, mpaka hivi sasa hayapo!

Anyway, ni hivyo tu. Nilikuwa nawaza tu kwa sauti. Sijali….wafanye tu wanavyotaka.
Ngosha na wewe ni wale wale Wajamaa ambao ni wajinga na watu wa.hovyo and so Wala asingesaini..

Mtu ambae anasema anataka matajiri waishi kama mashetani au watu waendee kuwa maskini ndio awatawale anaweza saizi mkataba wa kuleta Neema Kwa Nchi?

Hizi hapa ni faida za mkataba,haya na nyie Wajamaa tuelezeeni hasara zake Kwa hoja sio Kwa hisia na propaganda..
 
Toka hapa na hizo faida zako za kutungwa.

Hakuna lolote.
 
Mkataba wa kijinga tumejifunga kwa mwarabu halafu unatuonesha faida zake? hauna akili.

Hakuna faida yoyote tutakayopata itakayozidi ile atakayopata mwarabu, kwasababu msaliti ameitoa bandari yetu kwao milele.
 
Jibu hoja wewe mjinga,hizo ni faidia za kwenye mkataba Sasa tuonyeshe na wewe na hasara la sivyo unaingia kwenye kapu lile lile nalosema siku zote kwamba Wajamaa ni watu wa hovyo sana nyie..

Kwa mfano mismanagement ya hiyo Bandari kwangu inanisaidia nini? Na mnaopinga hili bila shaka mligeuza Chaka lenu la upigaji kama wale wajinga wa awamu wa 5 waliokuwa wanaomba Uzalendo huku wanapiga pesa ,pumbavu zenu.
 
Ngosha na wewe ni wale wale Wajamaa ambao ni wajinga na watu wa.hovyo and so Wala asingesaini..

Mtu ambae anasema anataka matajiri waishi kama mashetani au watu waendee kuwa maskini ndio awatawale anaweza saizi mkataba wa kuleta Neema Kwa Nchi?

Hizi hapa ni faida za mkataba,haya na nyie Wajamaa tuelezeeni hasara zake Kwa hoja sio Kwa hisia na propaganda..

Wasafwa mliiuza Mbeya kwa Wanyakyusa 😂😂
 
Mkataba wa kijinga tumejifunga kwa mwarabu halafu unatuonesha faida zake? hauna akili.

Hakuna faida yoyote tutakayopata itakayozidi ile atakayopata mwarabu, kwasababu msaliti ameitoa bandari yetu kwao milele.
Chuga man vp upo mzee?
 
Mkataba wa kijinga tumejifunga kwa mwarabu halafu unatuonesha faida zake? hauna akili.

Hakuna faida yoyote tutakayopata itakayozidi ile atakayopata mwarabu, kwasababu msaliti ameitoa bandari yetu kwao milele.
Pumbavu sana ,faida hizi zitakazopatikana hapa ni mara 100 zaidi ya upuuzi mnafanya hapo bandarini..

Mwarabu anafanya biashara ni investor unadhani amekuja kuuza sura? Iko hivyo Hadi kwenye Madini,viwanda nk anae commit ujuzi na mtaji atapata zaidi..

Nitajie hasara Nchi itapata maana baseline tunayo kwamba Port Ina underperform since independence
 
Back
Top Bottom