Uchaguzi 2020 Kwanini huu ndio Uchaguzi Mgumu zaidi kwa CCM?

Amani iwe nanyi wadau

Kama mada inavyojieleza hapo juu, hizi ndo sababu za Kwa nini Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu ndo uchaguzi Mgumu zaidi kwa CCM?

1. Mwaka 2015 Chadema walikuwa na mgombea aliyependwa na watu Lowassa Ila hakuwa mgombea makini
CCM waliweza kumchafua sana Lowassa kutokana na kashfa zakena madhaifu yake. Mwaka huu Chadema hawajarudia makosa 2020. Wana mgombea makini sana Tundu Antiphas Lissu mwenye akili sana na uwezo mkubwa sana kama mwanasiasa. Wengikwa uwezo wake wa akili na kujenga hoja wanamfananisha na Mwl Nyerere pamoja na Oscar Kambona ambao ndo wanachukuliwa kama wanasiasa bora zaidi kuwai kutokea Tanzania.

2. Mgombea wa CCM kuyaumiza makundi mengi isivyo kawaida katika kipindi chake cha miaka 5
Ni ukweli ulio dhahili kuwa kila kundi katika nchi hii limeguswa vibaya sana kwenye awamu ya tano, hali ya uchumi na kodi mbaya za TRA zimeathili sana wafanyabiashara, wafanyakazi kutopandishwa mishahara kwa miaka 5, Wakulima wa mazao kama korosho, mbaazi, tumbaku, kahawa na mahindi kuharibiwa masoko yao kwa amri za serikali pamoja na kundi kubwa la vijana kukosa ajira kutokana na uchumi kutokuwa vizuri. Kufunguliwa makesi kwa wanaharakati na watu wanaompinga magufuli pia

3. Awamu ya Tano kutokuwa na mahusiano mazuri na wadau wa maendeleo wa Tanzania wa miaka yote
Hili hata mtu asiye na akili ameliona. Katika awamu ya tano ndo Tanzania imesemwa vibaya zaidi kimataifa na hata kutolewa matamko mbalimbali yasio mazuri na ya tahadhari na balozi za hapa nchini. Hiki ni kiashiria kuwa hata wadau wa kimataifa wamemchoka Magufuli

4. Lissu kuwa Mhanga wa Jaribio la Mauaji
Hii kete ingawa CCM wanaidharau ila hili ni moja ya jambo linalombeba sana Lissu. Watu wengi wanamuona Lissu kama muujiza unaotembea. Shambulio dhidi yake tena kwenye awamu ya Tano linamfanya awe rahisi kueleweka kwa watu na hata watu kumpenda zaidi.

5. Hali ya uchumi
Hali ya uchumi ya Tanzania imekuwa mbaya sana hasa kwa watanzania. Wengi maisha yao yamezidi kuwa magumu zaidi ukiangalia kama wakulima, wafanyakazi na vijana. Hawaoni ahueni mbele na wengi wanaona ni ngumu hali hii Kubadirika kwa aina ya utawala wa magufuli

Nimalize kwa kusema, katika survey yangu Kuna jambo kuu nimeliona. Kuna uwezekano mkubwa sana Watanzania wakaandika historia kuu mwaka huu. Tundu Antiphas Lissu anaenda kuishangaza dunia mwaka huu.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025 ni Tundu Antiphas Lissu.
wewe ulisikia wapi kama huuni uchaguzi mgumu?
 
Kama una akili timamu ukafanya survey na umekuja na hili hitimisho

Hakuna namna umefanikiwa kwa lolote katika maisha yako, you are average person na haupendi ukweli

TL ataweka platform nzuri na mwaka 2025 CCM itakuwa na wakati mgumu sana kuliko kawaida

Mwaka huu hakuna miujiza ndugu

Pole
Lolote lawezekana. Wiki mbili zilozobaki zitatupa majibu. Ingawa watu washaamua kuna kujichanganya. Jana kuna mtu alijichanganya.Amini kuna watu wa kijani wamekuwa njia panda na wengine hawatapiga kura ama watapigia upande mwingine. Kuna mtu anabebwa habebeki.
Kuna mtu amekaza msuli hakuna kuibiwa... Hii imeanza kutishia waibaji.
Usiseme waibaji hawapo. Wapo na wamejibainisha wazi wakiwa na kijani chao.
Kwa hivi uchaguzi huu si raisi tusubiri wiki mbili ziishe.
Wengine tusingepiga kura lakini yanayoendelea yanatufanya tupige kura tunahamasisha wengine waliokuwa wamekata tamaa.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Amani iwe nanyi wadau

Kama mada inavyojieleza hapo juu, hizi ndo sababu za Kwa nini Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu ndo uchaguzi Mgumu zaidi kwa CCM?

1. Mwaka 2015 Chadema walikuwa na mgombea aliyependwa na watu Lowassa Ila hakuwa mgombea makini
CCM waliweza kumchafua sana Lowassa kutokana na kashfa zakena madhaifu yake. Mwaka huu Chadema hawajarudia makosa 2020. Wana mgombea makini sana Tundu Antiphas Lissu mwenye akili sana na uwezo mkubwa sana kama mwanasiasa. Wengikwa uwezo wake wa akili na kujenga hoja wanamfananisha na Mwl Nyerere pamoja na Oscar Kambona ambao ndo wanachukuliwa kama wanasiasa bora zaidi kuwai kutokea Tanzania.

2. Mgombea wa CCM kuyaumiza makundi mengi isivyo kawaida katika kipindi chake cha miaka 5
Ni ukweli ulio dhahili kuwa kila kundi katika nchi hii limeguswa vibaya sana kwenye awamu ya tano, hali ya uchumi na kodi mbaya za TRA zimeathili sana wafanyabiashara, wafanyakazi kutopandishwa mishahara kwa miaka 5, Wakulima wa mazao kama korosho, mbaazi, tumbaku, kahawa na mahindi kuharibiwa masoko yao kwa amri za serikali pamoja na kundi kubwa la vijana kukosa ajira kutokana na uchumi kutokuwa vizuri. Kufunguliwa makesi kwa wanaharakati na watu wanaompinga magufuli pia

3. Awamu ya Tano kutokuwa na mahusiano mazuri na wadau wa maendeleo wa Tanzania wa miaka yote
Hili hata mtu asiye na akili ameliona. Katika awamu ya tano ndo Tanzania imesemwa vibaya zaidi kimataifa na hata kutolewa matamko mbalimbali yasio mazuri na ya tahadhari na balozi za hapa nchini. Hiki ni kiashiria kuwa hata wadau wa kimataifa wamemchoka Magufuli

4. Lissu kuwa Mhanga wa Jaribio la Mauaji
Hii kete ingawa CCM wanaidharau ila hili ni moja ya jambo linalombeba sana Lissu. Watu wengi wanamuona Lissu kama muujiza unaotembea. Shambulio dhidi yake tena kwenye awamu ya Tano linamfanya awe rahisi kueleweka kwa watu na hata watu kumpenda zaidi.

5. Hali ya uchumi
Hali ya uchumi ya Tanzania imekuwa mbaya sana hasa kwa watanzania. Wengi maisha yao yamezidi kuwa magumu zaidi ukiangalia kama wakulima, wafanyakazi na vijana. Hawaoni ahueni mbele na wengi wanaona ni ngumu hali hii Kubadirika kwa aina ya utawala wa magufuli

Nimalize kwa kusema, katika survey yangu Kuna jambo kuu nimeliona. Kuna uwezekano mkubwa sana Watanzania wakaandika historia kuu mwaka huu. Tundu Antiphas Lissu anaenda kuishangaza dunia mwaka huu.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025 ni Tundu Antiphas Lissu.
kwa hakika nchi hii inakwenda kukombolewa dhidi ya mabeberu weusi, kama mwalimu J.K. Nyerere aliweza kumtoa mkoloni yule, si zaidi sana kwa TUNDU A. LISSU hasa kwa zama hizi za kuumizana? sidhani kama kuna mtanzania mwente akili timamu ambaye hajaguswa na udhalimu wa serikali ya magufuli.

ccm must go, JPM must go to Chattle.
 
Back
Top Bottom