Kwanini Instagram na Facebook bado wanamlilia Magufuli?

JF unaweza ku argue na fake account 10 zote zinazoendeshwa na mtu mmoja...
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji220]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jf kufungua page facebook haiondoi ukweli kwamba watz wengi ambao wapo active fb ni wajinga.

mfano mdogo, ingia fb then fanya spellcheck kwenye account za wabongo uone vituko.
Naunga mkono hoja, aisee wengi sana hawajui kuandika.
 
Ni kweli, tabaka kubwa la wapiga kura wa nchi hii ni huko Instagram na Facebook ambako pia ndipo linapopatikana tabaka kubwa pia la wananchi wenye upeo mdogo sana wa kufikiri.
Bado tuna safari ndefu kama nchi.
Hata wewe unayehisi una upoe mkubwa kufikri Hauna huo upeo
 
Are you really informed au wewe unachojua ni kupata tetesi
 
Nchi hii kura haziheshimiwi aisee labda USA huko na nchi za dunia ya kwanza. Nchi Ina illiteracy level ya 80% utegemee wafanye maamuzi serious kwa nchi?
[emoji23][emoji23][emoji23]Hiyo 80% sijui umeitoa wapi
 
There is no way mjinga ataweza kureason mambo.

Napata shida mtu ana akili zake timamu anaponiambia meko anazushishwa.

Hivi kipindi anajitoa kwenye mikataba ya transparency alikuwa na malengo gani? Hili nalo watu hawajiulizi.
 


Sista unapofanya mijadala na watu achana na maneno kama haya 'mwanaume mzima' jifunze kutetea hoja zako bila excuse za kijinga kama hizo!!
 
Ni kweli tena MTU na akili zako kweli unashinda Facebook kutafuta nini labda, insta kumejaa umbea tu hakuna cha maana huko
Huwezi kuwa great thinker ukawa na mawazo kama haya. Mtu aache kuendesha biashara zake katika platform yenye population kubwa eti kwa kufofia kuonekana ni kilaza?

Hata humu JF vilaza ni wengi mno.
 
Sasa hawa ndiyo wanajiona GT na kuwadharau users wa FB. Huo uzi ndiyo ulionyesha kiwango cha uelewa mdogo wa members wengi hasa Pro-Chadema,comments nyingine nilikiwa nasoma naishia kucheka hadi naangalia Profile ya aliyeandika.
Kwani JF zama hizi bado watu wanaitana GTs? sidhani. Ningeliijua JF ikiwa hivi ingenifikirisha sana kujifanya mmoja wake.

Nilitamani kumuhoji Mzee Mwanakijiji kwenye bandiko lake lakini nikaona wote ataona ni wakosoaji hewa. Siku izi unakuta mada nzuri lakini ukiangalia mjadala unasema nisipoteze muda wangu.

Lakini ni matokeo yakutoa mwanya mchache wa watu kuwasilisha kero zao. Ukisoma dhana ya representative democracy unagundua kuwa ni haki yao watu kutumia mitandao kusema ukweli wawakilishi wayajue. Hawakuwa karibu nao kwa miaka na mikaka leo wapo wote kwenye jukwaa moja la melo.
 
Comments za fb nimekuja kugundua huwa zinasukumwa na upepo, inaweza kuanzishwa mada ukakuta kundi la wapinzani ndio wana comment tu kuelekea upande wao, lakini pia inaweza kuanzishwa mada nyingine ukakuta kundi la CCM tu ndio lina comment kuelekea upande wao, all in all napo kuna mgawanyo wa wapiga kura.

Lakini huku jf ni kikundi kidogo sana cha wapiga kura kisicho na impact yoyote, ID nyingi ni zile zile miaka nenda rudi, tofauti na fb huko kila siku zinazuka ID mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…