Kwanini Instagram na Facebook bado wanamlilia Magufuli?

Kwanini Instagram na Facebook bado wanamlilia Magufuli?

Baada ya ishu ya CAG nikasema niingie mitandaoni nione reaction ya wananchi juu ya serikali ya JPM.

Twitter na JF kama kawaida ni matusi tu na kejeli kwa mwendazake, ila awa ni wachache na tumeshawazoea hawanaga madhala.

Nikasema niingie kwa majority ya wananchi huko Facebook na Instagram penye watumiaji 90% wa social media wa Tanzania.

Nikakuta vilio na kukata tamaa kwa wananchi baada ya kuona kipenzi chao JPM anazushiwa uongo na mema yake yanapondwa.

Wananchi imani yao kwa Magufuli ni kubwa sana, waite wajinga awajaelimika ila kuna namna JPM aligusa maisha yao na akatengeneza connection nao. Hakuna kitu mtafanya sasa hivi kufuta hii love ya raia kwa JPM.

Nawashauri CCM na wapinzani mnaoendeleza vita na JPM wasibeze hivi vilio maana awa wananchi watawaadhibu siku moja. Kumpuuza Magufuli ni kuwapuuza majority ya watanzania 93%.

Msije sema hamkuambiwa.
View attachment 1748149View attachment 1748150View attachment 1748151View attachment 1748152View attachment 1748153View attachment 1748154
Research yako ipo biased sana! Hufai kukusanya data
 
Mleta uzi amechagua comments zinazoendana na hisia zake ndo kazileta hapa. Hata huko facebook na intagram wakeleketwa wapo kibao .

Endelea kujifariji.

Ripoti imetolewa wakati sahihi. Uandaaji wa ripoti umefanyika kipindi cha uhai wa mwendazake. Sioni sababu ya kusema anachafuliwa, kwahiyo mlitaka ripoti isifie kila kitu. Mbona chama tawala kimepewa hati safi mbona hilo hamlizungumzii yaani mlitaka yote yawe mazuri tu wakati watendaji walivurunda.
 
Sawa endeleeni na matusi yenu nyinyi si mnajua kuongea sana. Ila mjue wananchi sio wajinga wanamjua mbaya kwao na mzuri kwao. Magufuli kawafanyia mengi mazuri haya matusi ya kumuita fisadi yatawahukumu siku moja.
Ebu toa mfano wa hayo mazuri ili watu wakuelewe!!!
 
Kichwa maji wewe... Emmh angalia huyo mkuda amefolliw watu wangapi kama si wawili 2. Which means hakuna mtu potential huko insta ambao wanaweza mu inspire zaidi ya hao wawili tu kati ya hao milioni 19.

JF is there to stay na bado itakua dira kwa serikali

Unajifanya kuijua sana JF kuliko wengine,hizi ndizo akili za kujiita GT,style yenyewe ya uchangiaji wako ni ya kihuni huni tu,actually u’re wasting my time,ingia kwa Ignore list,Imbecile.
 
Ni kweli, tabaka kubwa la wapiga kura wa nchi hii ni huko Instagram na Facebook ambako pia ndipo linapopatikana tabaka kubwa pia la wananchi wenye upeo mdogo sana wa kufikiri.
Bado tuna safari ndefu kama nchi.
Em kuweni serious basi.. Wapiga kura wengi ni wanavijiji, wakulima wa kawaida hata smartphone hawazijui, afu unawahusisha na wale wauza sura wa insta na Fb ?!!!
 
Ni kundi dogo Sana la wananchi,
Wanaothubutu kuwaita wenzao walio wengi kwamba Ni vilaza.
Wakati huo huo wakipiga kelele kuhusu demokrasia ambayo haitambui tofauti ya vilaza na viamza..
Hamnaga uchaguzi huwa tunakamilisha ratiba
long live JPM
Na hivi ndo ilivyokuwa reaction ya wananchi wengi WANYONGE wa huko vijijini, wasio na smartphone, baada ya matokeo ya ule uchaguzi HARAMU...


Magari, nyumba vyachomwa moto​

By
Mtanzania Digital
-
November 3, 2020
0
323

https://www.facebook.com/sharer.php?u=https://mtanzania.co.tz/magari-nyumba-vyachomwa-moto/
https://twitter.com/intent/tweet?text=Magari,+nyumba+vyachomwa+moto&url=https://mtanzania.co.tz/magari-nyumba-vyachomwa-moto/&via=Mtanzania
Logga in – Google Konton
Magari, nyumba vyachomwa moto | Mtanzania

Hadija Omary -Lindi

MAGARI saba,nyumba tatu, zahanati moja na ofisi ya kata, vimechomwa moto maeneo tofauti mkoani Lindi.

Kutokana na hali hiyo, jeshi la polisi linawashikilia watu kadhaa kwa kuhusika na tukio hilo

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema uhalifu huo umefanyika wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Alisema katika Wilaya ya Liwale, uhalibifu huo umefanywa kwa mbunge mteule wa jimbo, Zuberi Kuchauka ambapo nyumba zake mbili na magari matatu yamechomwa na moto.

Alisema mgombea udiwani Kata ya Liwale Mjini ambaye alishinda nyumba yake imechomwa moto na zahanati yake, imevunjwa vioo vyote na kuharibiwa baadhi ya vifaa vya maabara.

Alisema pamoja na mali nyingine ambazo wanaendelea kuzitathmini magari hayo saba yaliyochomwa moto, yalikuwamo ya Serikali yakiwamo yaliyopelekwa kwa ajili ya uchaguzi.

Alisema watu hao ambao baadhi yao wamekamatwa pia walikusudia kuchoma moto nyumba ya askari mmoja ambaye alikuwa akishiriki zoezo la kusimamia upigaji kura,lakini walishindwa, badala yake wakaishia kuvunja vioo vyote vya nyumba hiyo.

Alisema hali aliyoikuta baada ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa, inaacha maswali mengi kama vurugu zote hizo ni kwa sababu ya uchaguzi tu au kuna jamnbo jingine nyuma yake?
“Kwa sababu vurugu zile zilianza kufanyika mapema kabla ya matokeo kutolewa, zilianza kufanywa saa mbili usiku hadi saa nne,wakati huo matokeo yalikjuwa bado…”alisema.

Alisema katika mji wa Nachingwea kumefanyika mambo aloyoyaita yasiyo ya kiungwana wala kibinadamu.

Alisema gari la Serikali liilichomwa moto pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ahmad Makoroganya na nyumba yake kuvunjwa vioo vyote. Makoroganya alikuwa mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alishinda uchaguzi huo.

Alisema pia ofisi ya Serikali ya Kata ya Mpiruka pia ilichomwa moto.
Akizungumza watu waliokamatwa kutokana na vitendo hivyo wilayani Nachingwea, Zambi alisema kundi la watu lilikuwa limejificha nyumbani kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa wa Chadema likiwa na lita zaidi ya 40 za petroli, vinyago vya kuziba uso(mask), fomu namba 3 za polisi, pamoja na vitambulisho vya kupigia kura zaidi ya 60.
Kuhusu Jimbo la Mtama, Zambi alisema ofisi maendeleo ya jamii ilichomwa moto imeanguka haifai tena kwa matumizi, huku akisema jaribio kama hilo lilifanyika Kijiji cha Nyangamara.
Kuhusu Kilwa Kusini,alisema kulikuwa na jaribio la kuchoma ofisin ya kata ambapo petroli ilikwishamwagwa eneo hilo, lakini hivyo wasamaria wema waliwahi na kuidhibiti.
Alisema hadi sasa haijajulikana dhamkira ya watu wanaofanya huhalifu huo ni kina hadi, huku wakijiapiza kuwa wataua.
Aliyataja maeneo ambayo kauli hizo zimekuwa zikisemwa, kuwa ni Nachingwea, Liwale, baadhi ya maeneo ya Mtama na Kivinje.

Cc:
happyxxx
Nyamizi
 
Sio kwamba wote walio na account Facebook wana uelewa mdogo ila asilimia kubwa wana Wanauelewa mdogo
 
Mitandao ya wenye akili ndogo hyo huwezi kuta great thinker anaitumia hyo
Kwa haya mabadiko mengi yenye maneno ya kashfa nadhani hao great thinker hawavuki asilimia kumi ya members
 
Ujue watu wengi huko FB hawajui hata CAG na majukumu yake ni yapi, na wamesahau kuwa CAG tangu enzi za kikwete walikuwa wanatoa hizi report na Assad alivoendeleza hvo akafanyiwa zengwe la kuitwa Hadi bungeni, ingawa alikuja kusoma report kwa wananchi ikawa mwisho wake, jiwe mwenyewe alimchagua kichere ili amuendeshe and I do believe alikuwa anapelekewa report then inafanyiwa editing ije kwenye umma ili kumuonyesha yeye msafi. Na kamwe report ya CAG sio ya kisiasa useme inataka kufuta legacy ya mtu maana office u report Hali halisi.
Mie nikisema huko FB wanaojua hata CAG ni Nini watu wananishambulia tu bila sababu
Baki na CAG yako..
 
Unaweza ukawa unaishi pangoni au popote na ukawa great thinker vile vile loh
Yeeees !!!!!
Great thinker huyo,.....
Acheni kujikweza,
Kazi tu kuwadharau wenzenu kwamba hawana akili.
Tatizo Ni hivyo vielimu vyenu vidogo vidogo.
Wenye mashule yao makubwa Wala hawanaga mambo hayo..
 
Facebook ambao hawakupendezwa na mekoView attachment 1748891View attachment 1748894View attachment 1748893
Screenshot_20210411-015523.jpg
View attachment 1748892
 
Back
Top Bottom