Kwanini Jeshi imara kama Israel halina 4 stars General?

Vita inaonyeshwa channel gani?
 
Usidanganye aliyeshiriki Entebe hakuwa Benyamini huyu waziri mkuu,Bali alikuwa kaka yake ambaye alikufa katika operation huyo kaka alijulikana Kama Yonathan Natanyahu
 
... ha ha ha! Umenikumbusha Iddris Derby Marshal of Chad aliyeuwawa kwa mkuki na mwasi mmoja hivi haribuni siku chache kabla ya kuapishwa tena kwa awamu ya sita ya urais Chad!
 
... kaka; Rav Aluf (Lieutenant General), the highest military rank in IDF ni zaidi ma-Field Marshall unaowajua wewe! Kuwa Lieutentant General isikuchanganye ukadhani ni sawa na Lieutenant General wa shitholes! Hizo ni namba nyingine!
 
Hebe weka mtiririko wa vyeo vya jeshi hapa na sifa zao toka chini hadi rank ya juu kabisa!!!
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Sasa mwanajeshi anakula rushwa gani
 
Mkuu iko hivii?
Vyeo vya jeshi havivaliwi mabegani bila ya kufuata muundo.

Kila ngazi fulani ya muundo inaongozwa na kamanda mwenye cheo flani.

Mfano kama jeshi litakuwa na muundo wa kikundi cha watu9, basi kamanda wao atakuwa ni koporal, sajenti hahitajiki hapo.

Pia jeshi kama ni kikundi cha watu30, basi kamanda wake atakuwa ni luteni na meja hahitajiki hapo.

Kwa muktadha huo, mataifa hayalingani miundo ya najeshi yake kutokana mahitaji ya mataifa husika yaani kijiogafia na kiuchumi pia.

Kuna nchi zingine kutokana na jiografia yake, yaweza kuwa na jeshi lenye ukubwa wa brigedi moja, hivyo kamanda wake yaani mkuu wa majeshi atakuwa ni brigedia jenerali au unavyowaita wewe one star general na meja jenerali ama heo kingine cha juu hakitahitajika hapo.

Hata kama viichi vidogo sana vitahitaji kuwa na askari kombania moja basi mkuu wake wa majeshi atakuwa ni meja kutokana na muundo huo.

Sisi Tz cheo cha juu kabisa kilichostahili kimuundo ni luteni jenerali(3 star general) kutokana na muundo uliopo wa 'formation' ambao haujafikia 'Army'.

Utaratibu wa kuwatunukia maafisa wa jeshi cheo cha jenerali(4 star general) nchini Tz uliasisiwa na hayati mwalimu Nyerere baada ya 'vita vya Idd Amin' kutokana na lufufu ya majeshi iliyokuwepo wakati huo.

Waliomfuatia wakakaririshwa(nadhani jwa jili ya maslahi binafsi) kuwa mkuu wa majeshi anastahili na lazima awe jenerali, ambapo siyo sahihi.

Tunavyoona sasa, kumpachika mkuu wa majeshi cheo cha jenerali(4 star general) nje ya muundo uliopo sasa(active service) ni siasa.
 


Moshe Dayan Mzee wa kijicho kimoja, alikua hatari sana huyu mwamba..!!!
 
Katika sheria za israel kwenye mission yoyote ya hatari kama ile ni marufuku ndugu wa tumbo moja kushirikia kama wewe na kaka yako ni makomandoo basi anachukuliwa mmoja tu.benjamin netanyahu hakuwemo kwenye ile operation kwa kuwa alikuwemo ndugu yake huyo.
Kwa hiyo mleta mada katupiga kudai waziri mkuu wa Sasa wa Israel alikuwepo Entebe siku hiyo.
 
Kaka yake na siye yeye. ndiye mwanajeshi pekee wa Israel aliyeuawa kwenye operesheni hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…