ha ha ha....
Mentor that is a compliment i bliv... Thankyou..
I hope you heart is now beating calm calm calm...
Moyo umetulia...zaidi ya mtungi maji,
Nafsi yafurahia...cha zaidi sihitaji;
Kamwe usijerudia...muhimbili ntalazwa,
Taarifa japo toa...kazi nisijefukuzwa!!!
ila waonyesha una tofauti!!!Mentor next time will do the above...
alafu hayo maneno mazuri kweli... nataka
nikujulishe mapemaaa mimi ni full dada wa Mjini....lol
Me chanzo cha kutaka kujua kuhusu Jf ni mh. Kibonde kuna siku kwenye kipindi chake cha jahaz alikuwa anailalamikia na kuiponda kwa kumsema vibaya wakati huo alikuwa na Gadner so ndo nikaamua kuifatilia kuna nini hasa ndani yake na hatimaye nikajiunga.Thanks Kibonde kwa kunionyesha njia
I am so sorry kua am not.... Dah! pole kuku dissapoint...
usijali lakini... kwani urafiki plutonic rafiki hafai??? lol
Ninajitahidi kufikiri kwanini watu wanajiunga JF.
Mimi nilijiunga kwa nia ya dhati ya kutaka kujua zaidi watu wanavyoinyonya nchi yetu hasa kupitia Siasa. Wakati ninajiunga sikujua kama kuna majukwaa mengine kama Chit Chat, IT, Elimu, Jukwaa la wakubwa n.k kwa kuwa haikuwa nia yangu kutafuta vitu hivyo.
Bahati mbaya mtu hazuiliwi kukaa jukwaa moja, na si ajabu ukaona mtu anakurupuka toka jukwaa la wakubwa akiwa uchi na kwenda kuchangia mada nzito zilizopo kwenye majukwaa makini kama siasa. Wengine wakawa wanalalama kwamba wanaume wa JF hawawatokei, wao wanang'ang'ania siasa tu. Wapo wanaolia kwa kulizwa ndani ya JF.
JF inakua sana. Wengine siku zote walikuwa wanapiga chabo tu, hasa pale matukio makubwa yanapotokea ila wakaishia kuingia ndani. Na wapo ambao wao huja kuandika tu na kukimbia ati sisi ndio tusome. Wengine wametumwa (na vyama vyao au sirikali) kuja kuharibu tu au kukusanya taarifa.
Hii ndio JF yetu, Sijui wewe ulikujaje hapa?
Mimi nilivutiwa na "breaking news" , wakati niko nje, kufuatilia sakata la kujiuzulu edward lowassa.
Nikawa msomaji weee! Baadae nikajiunga.
Mimi nilikuwa naifuatilia hii JF toka 2008 kwa kusoma tu na kama reference yangu kwenye study kipindi hicho, baada ya kupewa taarifa na mshkaji wangu wa pale MNF....
Baadae nikapata kijiwe permanent, hivy ikawa daily kwaanzia asubuhi mpaka jioni, pitia majukwaa yote...
Basi baada ya mda kidogo nikawa nikijaribu ku-access naambiwa siwezi tena kufungua JF mpaka nijisajiri..
Nikaona isiwe taabu nikajiunga fasta tu hapo majuzi