Ninajitahidi kufikiri kwanini watu wanajiunga JF.
Mimi nilijiunga kwa nia ya dhati ya kutaka kujua zaidi watu wanavyoinyonya nchi yetu hasa kupitia Siasa. Wakati ninajiunga sikujua kama kuna majukwaa mengine kama Chit Chat, IT, Elimu, Jukwaa la wakubwa n.k kwa kuwa haikuwa nia yangu kutafuta vitu hivyo.
Bahati mbaya mtu hazuiliwi kukaa jukwaa moja, na si ajabu ukaona mtu anakurupuka toka jukwaa la wakubwa akiwa uchi na kwenda kuchangia mada nzito zilizopo kwenye majukwaa makini kama siasa. Wengine wakawa wanalalama kwamba wanaume wa JF hawawatokei, wao wanang'ang'ania siasa tu. Wapo wanaolia kwa kulizwa ndani ya JF.
JF inakua sana. Wengine siku zote walikuwa wanapiga chabo tu, hasa pale matukio makubwa yanapotokea ila wakaishia kuingia ndani. Na wapo ambao wao huja kuandika tu na kukimbia ati sisi ndio tusome. Wengine wametumwa (na vyama vyao au sirikali) kuja kuharibu tu au kukusanya taarifa.
Hii ndio JF yetu, Sijui wewe ulikujaje hapa?