Kila kitu ulichotaja hapo juu kinaelea angali sababu kila kitu kinamvuta mwenzake, chenye mass(kg) kubwa kinavuta zaidi chenye mass(kg) ndogo. Sasa utauliza kwa nini vinavutana lakini havigongani, sababu ni nyingi, sayari zote zinavutwa na jua, lakini zinazunguka jua kwa spidi kubwa kwa hiyo zinacounterbalance, mwezi unazunguka dunia kwa speed kubwa ambayo inatosha pia ku-counterbalance nguvu inayouvuta karibu.
Kama haija-make sense inakuaje kitu kikizunguka kwa kasi kinacounter balance em angalia hii picha hapa chini
Hilo gari likishuka kwa spidi kubwa, litaweza kuzunguka hiyo round kwa ndani bila kuanguka na likapitiliza hadi upande wa pili, lakini likishuka kwa spidi ndogo basi halitoweza kuzunguka litaanguka. Concept kama hiyo.
Kuhusu kuona nyota na mwezi wakati wa usiku peke yake ni kitu simple tu, dunia inajizungusha kwenye mhimili wake, upande ambao unakua hautazamani na jua moja kwa moja ndo inakua usiku, kwa kua mwanga wa jua haufiki basi nyota na mwezi utaviona. Hata mchana hua nyota zinatoa mwanga lakini huzioni mchana sababu mwanga wa jua ni mkali kuliko unaotoka kwenye nyota.. Chukua tochi mchana, mwambia mtu asimame 50M kutoka kwako, ile tochi mwanga wake hutouona sababu mwanga wa jua umezidi, ila usiku utauona.. Hili jambo hata mtoto mdogo anaweza kukuelezea.