Kwanini kada ya ualimu inapewa mshahara kidogo?

Kwanini kada ya ualimu inapewa mshahara kidogo?

Naomba niende Moja Kwa Moja kwenye maada hivi ni Kwa nini kada ya ualimu inapewa salary kiduchu kulinganisha na kada nyingine au kazi yao Haina direct impact kwenye jamiii? Naomba kuwasilisha
Tafiti vizuri.
Kada nyingi mshahara unafanana / unakaribiana ndani ya mamlaka za serikali kuu na serikali za mitaa. E.g Ualimu, Afisa Utumishi, Afisa Ustawi wa Jamii, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Habari, Afisa Utamaduni, Afisa Masoko, Mkutubi, Mchumi, Afisa Ushirika etc. Wote hawa wanalingana mshahara kwa ngazi inayofanana i.e TGTS D, TGSS D kwa ngazi ya shahada anapoajiriwa au kwa ngazi ya Stashahada (TGSS C, TGTS C)
 
Waalimu ndio kada inayopendelewa kuliko wengine ila hamjui tu. Mishahara yenu wala sio midogo ni sawa na watumishi wengine tu hakuna tofauti. Nyinyi mna ziada ya yafuatayo
1. Kazi zenu zinaisha saa nane na nusu na wengine wanakula kona kabla hata ya muda huo,
2. Mna likizo kama nne hivi kwa mwaka pale shule zinapofungwa mnakuwa na muda wa kutosha kufanya mambo yenu
3. Sawa hamna posho nyingi lakini kuna kusimamia mitihani, kusahihisha mitihani, kusimamia uchaguzi za serikali, mambo ya sensa na hizi zote mnalipwa

Tatizo lenu waalimu mnakopa sana, unakuta mtu yuko vikoba 3 vyote kakopa, kakopa bank, au hizi microfinance yaani ni shida. ukiwa unakopa lazima utaona mshahara mdogo sababu ya makato
 
Naomba niende Moja Kwa Moja kwenye maada hivi ni Kwa nini kada ya ualimu inapewa salary kiduchu kulinganisha na kada nyingine au kazi yao Haina direct impact kwenye jamiii? Naomba kuwasilisha
Walimu amna akili na ni wapumbavu sana ...labda useme kwanini wapumbavu kwenye kada zingine wanalipwa mshahara mkubwa tofauti na walimu
 
Mleta mada umekariri,twambie huo mshahara mdogo wa kada ya ualimu umelinganisha na kada zipi? Tutajie ndoo tuanzie hapo.Tanzania hakuna kada moja afya ambayo naona wengi ndoo linganisho lao.Tuna kada nyingi sana je unajua mishahara yao?
Mshahara wa mwl Degree anaonza nao TSH 716000/=, diploma TSH 532000, Certificate TSH 442000/= sijajua kwa afya ila nasikia ni kubwa kdogo kulinganisha ni walimu
 
Mshahara wa mwl Degree anaonza nao TSH 716000/=, diploma TSH 532000, Certificate TSH 442000/= sijajua kwa afya ila nasikia ni kubwa kdogo kulinganisha ni walimu
Tatizo Makato, na hawana marupu rupu wala posho. Lol
 
Mshahara wa mwl Degree anaonza nao TSH 716000/=, diploma TSH 532000, Certificate TSH 442000/= sijajua kwa afya ila nasikia ni kubwa kdogo kulinganisha ni walimu
Afya degree except daktari na pharmacy wanakula 1,040,000, daktari ni 1.5m pharmacy around 1.25m

Diploma afya zote wanalamba laki saba kama skosei.

Yani mwenye diploma ya afya analingana na mwenye degree ya ualimu
 
Kada zilizo chini ya tamisemi nying mshahara ni sawa Kwa ngazi zote kuanzia certificate had diploma had degree Kuna wengine ni za chini Zaid labda afya ndio kidogo Wana unafuu
 
Naomba niende Moja Kwa Moja kwenye maada hivi ni Kwa nini kada ya ualimu inapewa salary kiduchu kulinganisha na kada nyingine au kazi yao Haina direct impact kwenye jamiii? Naomba kuwasilisha
Wapo wengi mno ndo maana, lakini ni kada nyingi zinalingana salary scale na walimu labda sekta ya afya ndo wapo juu kidogo
 
Mshahara wa mwl Degree anaonza nao TSH 716000/=, diploma TSH 532000, Certificate TSH 442000/= sijajua kwa afya ila nasikia ni kubwa kdogo kulinganisha ni walimu
Hizo ni take home degree basic ni laki 8 km sikosei
 
Back
Top Bottom