Waalimu ndio kada inayopendelewa kuliko wengine ila hamjui tu. Mishahara yenu wala sio midogo ni sawa na watumishi wengine tu hakuna tofauti. Nyinyi mna ziada ya yafuatayo
1. Kazi zenu zinaisha saa nane na nusu na wengine wanakula kona kabla hata ya muda huo,
2. Mna likizo kama nne hivi kwa mwaka pale shule zinapofungwa mnakuwa na muda wa kutosha kufanya mambo yenu
3. Sawa hamna posho nyingi lakini kuna kusimamia mitihani, kusahihisha mitihani, kusimamia uchaguzi za serikali, mambo ya sensa na hizi zote mnalipwa
Tatizo lenu waalimu mnakopa sana, unakuta mtu yuko vikoba 3 vyote kakopa, kakopa bank, au hizi microfinance yaani ni shida. ukiwa unakopa lazima utaona mshahara mdogo sababu ya makato