Mashindano ya TIFF ya NBC na CRDB yapi ni makubwa na magumu?
Penda mpira kwanza kabla ya kuipenda timu yako, utapata Raha na uwezo wa kuishauri timu yako unayoipenda. Mashabiki wa Yanga wanapenda mpira kuliko Yanga yao, hivyo kama mpira hauchezwi hawana mswalie mtume na kiongozi Wala mchezaji asiyefanya vizuri. Hiyo ni tofauti na Simba ambayo imejaa watu wasioweza kuikosoa timu yao.
Mfano, kama mtajidanganya kuwa timu yenu ni nzuri kwakuwa imecheza finali ya FA ya CAF mmekwisha. Mnajua wenyewe ni kwa vipi timu yenu imefika final ya CAF confederation na imekuwa ya pili kwenye ligi ya NBC.